Tanzania Yatumbukia Rasmi Kwenye Mtego wa Udini

Tanzania Yatumbukia Rasmi Kwenye Mtego wa Udini

Kwa macho ya kawaida, Tanzania inaonekana shwari. Lakini kwa waliopasua pazia la unafiki, hali si ya kawaida tena. Udini umejitokeza waziwazi, tena kwa ushawishi wa kutisha.

Mawaidha ya Eid mwaka huu yameacha majeraha ya kihisia kwa baadhi ya viongozi wa dini nyingine, waliodai kuwa wamepingwa na kulengwa kwa maneno makali na kejeli.

Kwa bahati mbaya, hata Rais Samia Suluhu Hassan ameonekana kuwa muhanga wa chuki hizi za kidini. Wapo wanaompinga si kwa sera zake, bali kwa sababu ya dini yake. Hawasemi moja kwa moja, lakini kauli zao zinaonesha mzizi wa ubaguzi. Hawamtaki Samia kwa sababu sala zake hazifungwi kwa maneno yao. Hii ni hatari kwa Taifa.

Na kama hiyo haitoshi, Shehe Ponda kujiunga na chama cha siasa wakati huu kumeibua maswali mengi.

Amedumu miaka mingi kama kiongozi wa dini asiyeegemea upande wowote wa kisiasa kwa nini sasa?

Je, kuna mkakati mpana unaoibuka kama jibu kwa mashambulizi ya kifikra dhidi ya Waislamu?

Rafiki zangu, huu si wakati wa kupumbazwa na maneno matamu ya kidini.

Tuamke na tuchuje kila tunachosikia.

Tukumbuke: dini si silaha ya kumdhalilisha mwingine. Na Mungu wetu hawezi kupenda chuki kwa jina lake.

Tufumbue macho. Tuseme ukweli. Tukiwa tunatazamana usoni.
Ww uliona wapi mwanamke ni kiongozi ndugu yangu hicho kitu hakipo,lazima tuingie kwenye udini tu kwa sababu tunaowategemea kutoa ushauri ndio washabiki wa mambo hayo,SAMIA mwenyewe ni chenga tu,uje kikwete ndio kabisa sifuri anaongea kama mtoto Wala huwezi Sema eti anaushauri kama mzee hakuna.Kiongozi kama hawezi kutuongoza tuseme hawezi kama Taifa bila ushabiki,leo tumetumbukia kwenye utekaji na uuaji ni sababu ya kumpa mwanamke usimamizi wa mambo ya msingi,na tabia ya kudhani watu ni wajinga miaka yote,ni makosa.CCM na viongozi wenu tumieni AKILI ninyi ndio viongozi wa Taifa hili nguvu haisaidii ikitumika kama hali ya wananchi ni mbaya ni kupoteza muda.
 
Kuna ukweli!!wakristo wana chuki na Rais akiwa muislam
Hata huu uzushi wa sijui anauza Bandari and such nonsense ni Kwa sababu sio Mkristo.

Ubinafsishaji haujaanza Leo hii hapa Nchini na nilitarajia watuambie baada ya ubinafsishaji hasara zipi na faida zipi zimepatikana,hawatasema.
 
Tukemee utekaji bila kujali anaetekwa ni wa dini gani au utawaka uliopo lakini nakumbuka utekaji toka kipindi cha JPM ulikuepo japokua mimi nilikua namkubali JPM lakini kwenye utekaji tulimkemea bila kujali ni wa dini gani Roman catholic vile vile walikemea Mpaka Askofu Neghamwizi alinyanganywa Passport Katoliki walitoa waraka mkali wa Pasaka Mpaka Bashite akawapiga Majungu Katoliki. Kwa nini sasa ukimea mauaji na Utekaji mnasema Udini kifupi kupoteza Ndugu zetu nao wafamilia sio vizuri fikilia familia ya Soka Ben saa8 Anzroy Gwanda Mzee kibao. Mgimwa watu kama wana makosa Sheria zichukue mkondo wake Tusitake kuleta Udini kwenye Maisha ya Watu
 
Ila hii dunia kuna watu akili zao ni ndogo, yaani kisa mimi mkristo basi nipende rais awe mkristo au nimchukie may be Mama Samia kisa ni muislamu.... Hv rais akiwa mkristo au muislamu hv mimi direct inanisaidia nini km sio useng..e tu usiokuwa na maana....
 
Ila hii dunia kuna watu akili zao ni ndogo, yaani kisa mimi mkristo basi nipende rais awe mkristo au nimchukie may be Mama Samia kisa ni muislamu.... Hv rais akiwa mkristo au muislamu hv mimi direct inanisaidia nini km sio useng..e tu usiokuwa na maana....
Waambie wajitambue hawa wajinga wa JF.

Hususan huyu funza ndio fala kabisa.
 
Tufumbue macho. Tuseme ukweli. Tukiwa tunatazamana usoni.
Ni mstari huu pekee nilio uelewe kwenye mada nzima.
Umepiga mizunguko mingi mno bila ya sababu zozote.

Kwenye swala hili la udini huwezi kamwe kumweka pembeni Samia. Naona wewe umeamua kuwa sehemu ya wahanga. Inashangaza sana.

Na unaposema udini unasahau kwamba hii ni agenda ya kundi maalum; si waTanzania kwa ujumla wao. Kundi hili limempata Samia ambaye kaenea vizuri kwenye mipango yao, kwa hiyo wanamtumia ipasavyo.
Na kama asipokuwa mwangalifu, kundi hili litamsukuma hadi asababishe damu ya waTanzania kumwagwa.
 
Back
Top Bottom