Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

Jumuiya yetu hii kuna mda huwa najiuliza kabisa kwamba tulijiandaa vya kutosha kuungana? Ni miongoni mwa jumuiya zenye matatizo makubwa sana ya kutokuwelewana kabisa,

Juzi tumetoa kusikia Burundi kafunga mpaka wake na Rwanda

Congo na Rwanda wenye ni shida tupu shutuma kila kukicha

Uganda na Kenya wenyewe mashaka ni makubwa

Congo na Kenya niliona Congo anaishutumu Kenya kwa kuruhusu yule jamaa Mkongo/mpinzani wakati wanakaribia uchaguzi nadhani aliyenda kuongea na vyombo vya habari Kenya

Tanzania na Kenya hapa sasa ndo ngachoka

Somalia na Kenya wenyewe ni shida

Jumuiya ya kinafiki hii acha tu
 
EAC ni muungano wa kihuni sana na utasambaratikaga kihuni sana,Rwanda na Burundi wana bifu,Rwanda na Congo bifu,Uganda na Kenya bifu ya biashara ya mafuta na sasa Kenya na Tanzania tena. Muungano kama EU wana mashariti magumu sana kupokea wanachama,ndio maana huwezi sikia wanakwaruzana wao kwa wao.EAC ni muungano wa kihuni

Bado Somalia hajaanza ujinga wake.
 
Kenya hufanya hujuma sana za kichini chini kufanya abiria wanaokuja Tanzania kupitia JKIA Jomo Kenyatta International Airport Nairobi kwa kuwaweka masaa kibao ili abiria hao waseme usafiri kwenda Tanzania ni mgumu sana hivyo kama masuala ya kiutalii, biashara n.k bora wamalizie Nairobi Kenya badala ya kwenda 'shamba kijijini' Tanzania ambapo usafiri wa ndege ni mgumu sana...

Umesema kweli kabisa. Unafika JKIA saa mbili usiku unaondoka saa kumi na mbili Asubuhi Kuja Dar, aiseeh ni mateso. Leo ndio umenifungua macho.
 
Back
Top Bottom