Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

Kuna Truvks nyingi za Kenya zinafanya kazi Tanzania.Zinabeba hadi kokoto,makaa ya mawe nk
Naona hii inatishia mstakabali wa EAC.
Nakuambia Wakenya wana ROHO MBAYA SANA na UBINAFSI

Wao wanafaidi sana huku TZ ila hawataki vitu vyao viguswe

Nenda Moshi hasa barabara ya chekereni Mwanga mpaka Tanga kuna Malori mengi sana ya Kenya kila siku sio chini ya 100 yanabeba Makaa ya mawe kutoka Mtwara, Gesi na pia Vitunguu kutoka Chekereni na Kahe

Wanaenda kupackage na kuuza nje

Wanapaswa kupigwa Blockage

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: apk
Wakenya ni hatari sana wao utakuta gari zao zipo Ruvuma zinapakia mahindi ila wao hawataki gari zetu ziingie ndani ndani kupakia kitu chochote wangeachana na huo upuuzi aisee kila kukicha mambo ya kizamani tuu..
JPM aliwahi kuwapiga ban kama hii akaonekana anaharibu mahusiano, kafunga nchi, hawa si watu wa kuwachekea!!. Kweli tutamkumbuka.
Wao hawakujua kwamba Kenya ndiyo wawekezaji wakubwa tz kwa nchi za afrika Mashariki? Mbali na bidhaa zao kupatikana kwenye kila duka la bidhaa muhimu mitaani. Kimbo, colgate, cadbury, omo, blueband, ice creams, panadol, menthodex, unilever, lifebuoy, palmolive, mchuzi mix, maziwa brookeside. Tukizuia na hizi watajuta kutunyìma leseni.
Bado wananunua kwetu maharage, mchele, korosho, mahindi, mpaka wanakodi mashamba ya vitunguu!! Wakileta ngebe tunachoma na vifaranga tena!
 
Angalau hapa mwanasheria nguli wa TCAA msomi Hamza Johari amefanya uzalendo unaukubalika, kutetea maslahi ya Tanzania.

Na katazo hili liwe siyo tu baina ya Nairobi na Dar es Salaam tu bali Kenya na viwanja vyote vikubwa vya kimataifa vya nchini Tanzania.

Tanzania blocks Kenya Airways flights in reciprocity dispute​

thecitizen.co.tz
https://www.thecitizen.co.tz › national
Tanzania blocks Kenya Airways flights in reciprocity dispute | The Citizen

37 minutes ago — Tanzania blocks Kenya Airways flights in reciprocity dispute. Monday, January 15, 2024.
Missing
Funga na route ya NBO - ZNZ
 
Hii imekaa poa zaidi.
Wakianza tu, hapo hapo na sisi tunamalizia, tit for tat.
 
Wakenya ni hatari sana wao utakuta gari zao zipo Ruvuma zinapakia mahindi ila wao hawataki gari zetu ziingie ndani ndani kupakia kitu chochote wangeachana na huo upuuzi aisee kila kukicha mambo ya kizamani tuu..
Tatizo hayo Mahindi kwetu hayauziki au wanapangiwa bei ya chini kiasi kwamba mkulima hapati kitu
 
Hakuna haki bila wajibu. Ukifunguliwa nawe fungua wako.
Mimi nilidhani kwa kuwa bibi yenu amefungua nchi hatuwezi kufika huko maana tungeyamaliza kimya kimya chini ya uongozi shupavu wa mwana diplomasia nguli
 
Muungano kama EU wana mashariti magumu sana kupokea wanachama
Kabisa..
Nimeshangaa kusikia juzi hapa eti EAC imepokea Somalia kama mwanachama mpya. Unajiuliza, Somalia wana nini cha kuleta mezani?

Hata hivyo ingependeza kujua upande wa pili wa stori, yaani kwanini Kenya walizuia ATCL..
 
Nani wa kuwakataa sasa, maana kwa Africa mashariki wangalau Kenya kwa mbali ndio hupata viongozi kwa uhalali. Hawa wengine wote wako madarakani kwa chaguzi za kihayawani. Hivyo wakija viongozi wengine wahuni hakuna wa kumuuliza mwenzake.
Ukitaka kujua uhalali wa uongozi wa Kenya muulize odinga na sio kuja na Porojo zako
 
Tuwafukuze na wakenya wanao fanya kazi Tz ,Ili nalo lifanyiwe kazi
Tutaanza na Wapare pamoja na Wamasai, Wapare tuwarudishe pale Taveta na Wamasai tuwarudishe pembezoni mwa Ziwa Turkana, hapo vipi unaonaje?
 
Ukitaka kujua uhalali wa uongozi wa Kenya muulize odinga na sio kuja na Porojo zako
Mahakama zao ziko huru, na Odinga alienda mahakamani. Sasa nikamuulize nini tena huyo Odinga?
 
Back
Top Bottom