Tanzania, Zanzibar zasaini Hati ya Makubaliano Sekta ya Madini
Aliyeelewa haya makubaliano kati ya Tanzania na Zanzibar ninaomba anieleweshe.

Ninaona Tanganyika tunaonekana ni watu wajinga na tusio elewa.

Zanxibar na Tanganyika ziliunda muungano unaoitwa Tanzania.
Sasa Tanzania inafanya makubaliano na Zanzibar??? Kinaitwa nini??
 
Attachments

  • IMG-20230720-WA0010.jpg
    IMG-20230720-WA0010.jpg
    44 KB · Views: 1
..Zanzibar hawana hata sehemu ya kuchimba mchanga, halafu Tanganyika inasaini nao mkataba wa mashirikiano ktk sekta ya madini?

Mambo ya ajabu kabisa ! Sasa nina matumaini makubwa hiki kiini macho cha muungano kinaenda fia ndani ya utawala wa huyu bibi wa kizanzubari ! Nauona uchungu mkubwa wa sisi watanganyika !
 
Mafuta sio madini ?....maana huitwa dhahabu nyeusi....yakipatikana huko Zenji huenda yakajumuishwa kwenye hayo makubaliano ?

Nguruvi3 Kalamu Pascal Mayalla zitto junior
Sasa itabidi tuweke utaratibu wa namna hiyo kwa kila mkoa.

Huu ni ujinga wa kipekee kabisa.

Hawa watu kazi imewashinda kila mahali.

Sina shaka hilo nalo waziri kapewa kama agizo toka kwa Samia, ili kuipa uzito mkubwa Zanzibar, ionekane kuwa na hadhi sawa na serikali ya Tanzania.

Watu hawayaoni matendo haya na kuyaelewa vizuri, ili wayape uzito unaostahili.

Matukio yote haya ni alama za Samia kuutengeneza muungano uwe wanavyoutaka wao, Zanzibar.

Na mijitu ya Tanganyika ipo inakenua tu meno (nawazungumzia viongozi waliomo ndani ya CCM,mawaziri na mibunge).

Zanzibar, kupitia kwa Samia sasa hivi inatengeneza muundo wa muungano wanaoutaka wao bila ya kuwashirikisha walioungana nao.
Hawa wanaamrishwa kutekeleza tu!
 
Aliyeelewa haya makubaliano kati ya Tanzania na Zanzibar ninaomba anieleweshe.

Ninaona Tanganyika tunaonekana ni watu wajinga na tusio elewa.

Zanxibar na Tanganyika ziliunda muungano unaoitwa Tanzania.
Sasa Tanzania inafanya makubaliano na Zanzibar??? Kinaitwa nini??
hapo sasa
 
k
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili zilizopo katika upande wa Muungano ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta manufaa kwa pande zote mbili.

Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam Dkt. Biteko amewataka watendaji wa wizara hizo kusimamia utekelezaji wa makubaliano

“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalitupa dira mpya katika kuendeleza mashirikiano yetu, hivyo tulichosaini leo sio kwa ajili ya kupiga picha bali ni kwa ajili ya kazi tuliyojipatia, natamani kuona mambo tuliyosaini hapa yanakuwa mfano na yanafanyika kwa weledi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili,” amesema Dkt. Biteko

Aidha, Dkt. Biteko amewataka watendaji wakuu wa pande zote mbili kusimamia masuala hayo ili yaweza kutokea huku akitaka kuanza kusimamia masuala ambayo hayahitaji rasilimali fedha kubwa ikiwemo kufanya tafiti hivyo yale yanayowezeka yaanziwe kufanyiwa kazi leo na sio kungoja.

Pia, amewataka Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza timu ndogo ya kusimamia makubaliano hayo ili kuhakikisha ushirikiano huo unadumu na kuwa wa mafanikio katika pande hizo mbili.

Naye, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan amesema utiaji wa saini wa makubaliano hayo usiishie kwenye makaratasi bali ufanisi na utendaji unaotakiwa kuonekana ukaonekane.

“Kitendo kinachofanyika leo ni kitendo muhimu sana kwa kwa pande zote mbili ambapo viongozi wetu wa juu wamekuwa wakitusisitiza kuendeleza mashirikiano ambapo tunategemea kushirikiana hasa katika suala la utaalamu hususan katika kufanya tafiti kwa pamoja,” amesema Hassan.

Pia, Hassan amesema ushirikiano huo utazaa toka kwa pande zote mbili za muungano na kuwataka watendaji wa wizara yake kufanya kile kinachowezekana kunyika leo na wasingoje kesho.

Jumla ya Hati Tano za Makubaliano zimesaniwa kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Mafuta, Madini na Gesi Asilia, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Kituo cha Jemolojia na Tanzania (TGC)

Hili limepania kuivyonza tanganyika hadi tone la mwisho! mind you
 
Huu Muungano tutaibiwa kila kitu, tutauziwa kila kitu.
Tusipoamka na kuwakimbiza tutakosa bara na pwani
 
Natamani kuichangia hii thread kwa kina. Ila kama kuna mtu anaefuatilia masoko ya madini embu atupe tathmin fupi ya soko la matumbawe huko dunian inauzwaje? Maana ndo madin pekee yanayopatikana visiwan! Kokoto tu za ujenz zinatoka bara!
 
Tanzania na Zanzibar?

TF is that?

Tuna limuungano la kijuha sana.
Unajua tunapopiga kelele kwamba kuna tatizo watu hawaelewi. Sasa Tanzania ni ipi na Zanzibar ni ipi!
Unakuwaje na Tanzania bila Zanzibar. Halafu Mbarawa anakuwa Waziri wa Tanzania !!

Huu ni ujinga wa kuficha neno Tanganyika. Hiyo Tanganyika ndiyo Tanzania na ndiyo Muungano

SSH anafanya mambo 'nzuri' sana. Hili linafanyika makusudi ili kuhakikisha kuwa rasilimali za Tanganyika zinagawanywa Zanzibar kwa njia ya ''halali' inayoitwa makubaliano.
Jiulize hivi Zanzibar wana madini gani kiasi cha kufanya makubaliano na Tanganyika?

Kwasasa tu madini yote ya Tanganyika yanafaidisha Zanzibar kupitia BoT ambako kila sh 100 ya madini 4.5% inakwenda Zanzibar. Kana kwamba hiyo haitoshi sasa anaweka makubaliano ya nchi moja

Watanganyika wakidai vitu kutoka Zanzibar viwekewe kodi, Zanzibar wanalalamika sisi ni nchi moja. Sasa nchi moja inaweza kuwa makubaliano ya madini? Hivi Tanzania inaweza kusaini makubaliano ya Mawese na Kigoma!
Tanzania inaweza kusaini makubaliano ya gesi na Mtwara!

Tunaona SSH analeta hoja ya 'MKATABA' ya ACT Wazalendo, no wonder wanamshangilia sana utadhani si CCM

Kuna habari njema, SSH anaua muungano na hadi sasa amefanikiwa sana. Watanganyika wanayaona haya na ndiyo maana ikitokea kama la Bandari wanakuwa wakali sana!

Pascal Mayalla JokaKuu Tindo
 
Back
Top Bottom