Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imeshafanikiwa kwasababu SSH amesaidia sana kuwashtua Watanganyika!Hii ndiyo kazi kubwa inayofanyika.
Sasa sina shaka tena, naomba tu ifanikiwe, tena kwa haraka.
Walifanya hivyo walipodhani kuwa wana mafuta. Lakini mpaka sasa hayajapatikana ya kuweza kuvunwa. Sitashangaa wakidai kuwa mafuta/gesi asilia zirudishwe kwenye Muungano ili wafaidike na yaliyopatikana Tanganyika...Znz walifanya jitihada kubwa mpaka wakaondoa mafuta kwenye masuala ya muungano.
..Sasa sidhani kama kuna uwezekano wa wao kurudisha mafuta yao kwenye mikono ya muungano.
Sisi Watanganyika ni Majuha. Tunaendeshwa na wazanzibari milioni moja.Kwa nini wasaini bila kutushirikisha sisi wananchi?kipindi zanzibar walipotaka kuchimba mafuta waliyaondoa kwenye mambo ya muungano kwa kuhofia tanganyika itanufaika na rasilimali yao ya mafuta.kwa nini kwa sasa tena wanarudisha?Au kwa kuwa wameona maliasili tanganyika ni nyingi ndiyo maana wamesaini hiyo mukataba ya kimangungo?.Tunataka tanganyika yetu siyo upuuzipuuzi wa mikataba isiyona kichwa wala miguu.
Lakini hii imetokea kwa mara ya kwanza in a history of this country. Kuna precedence inaelekea kuwa set. Wacha tusubiri.Tanzania na Zanzibar?
TF is that?
Tuna limuungano la kijuha sana.
Sielewi kabisa.Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili zilizopo katika upande wa Muungano ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta manufaa kwa pande zote mbili.
Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam Dkt. Biteko amewataka watendaji wa wizara hizo kusimamia utekelezaji wa makubaliano
“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalitupa dira mpya katika kuendeleza mashirikiano yetu, hivyo tulichosaini leo sio kwa ajili ya kupiga picha bali ni kwa ajili ya kazi tuliyojipatia, natamani kuona mambo tuliyosaini hapa yanakuwa mfano na yanafanyika kwa weledi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili,” amesema Dkt. Biteko
Aidha, Dkt. Biteko amewataka watendaji wakuu wa pande zote mbili kusimamia masuala hayo ili yaweza kutokea huku akitaka kuanza kusimamia masuala ambayo hayahitaji rasilimali fedha kubwa ikiwemo kufanya tafiti hivyo yale yanayowezeka yaanziwe kufanyiwa kazi leo na sio kungoja.
Pia, amewataka Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza timu ndogo ya kusimamia makubaliano hayo ili kuhakikisha ushirikiano huo unadumu na kuwa wa mafanikio katika pande hizo mbili.
Naye, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan amesema utiaji wa saini wa makubaliano hayo usiishie kwenye makaratasi bali ufanisi na utendaji unaotakiwa kuonekana ukaonekane.
“Kitendo kinachofanyika leo ni kitendo muhimu sana kwa kwa pande zote mbili ambapo viongozi wetu wa juu wamekuwa wakitusisitiza kuendeleza mashirikiano ambapo tunategemea kushirikiana hasa katika suala la utaalamu hususan katika kufanya tafiti kwa pamoja,” amesema Hassan.
Pia, Hassan amesema ushirikiano huo utazaa toka kwa pande zote mbili za muungano na kuwataka watendaji wa wizara yake kufanya kile kinachowezekana kunyika leo na wasingoje kesho.
Jumla ya Hati Tano za Makubaliano zimesaniwa kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Mafuta, Madini na Gesi Asilia, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Kituo cha Jemolojia na Tanzania (TGC)
sana tena sana, aliokuwa anauelewa ni nyerere tu, labda na pengo.Tanzania, zanzibar? Siyo Tanganyika, Zanzibar?
Huu muungano mugumu kuutafsiri.
Zenji si Wana Wese ?..Zanzibar hawana hata sehemu ya kuchimba mchanga, halafu Tanganyika inasaini nao mkataba wa mashirikiano ktk sekta ya madini?
Walioungananao niTanganyika hiyo Tanganyika yenyewe haionekani inayoonekana ni Tanzania kwa hiyo zanzibar kasaini hayo mashirikiano na huyo anaeonekana ambae ni TanzaniaSasa itabidi tuweke utaratibu wa namna hiyo kwa kila mkoa.
Huu ni ujinga wa kipekee kabisa.
Hawa watu kazi imewashinda kila mahali.
Sina shaka hilo nalo waziri kapewa kama agizo toka kwa Samia, ili kuipa uzito mkubwa Zanzibar, ionekane kuwa na hadhi sawa na serikali ya Tanzania.
Watu hawayaoni matendo haya na kuyaelewa vizuri, ili wayape uzito unaostahili.
Matukio yote haya ni alama za Samia kuutengeneza muungano uwe wanavyoutaka wao, Zanzibar.
Na mijitu ya Tanganyika ipo inakenua tu meno (nawazungumzia viongozi waliomo ndani ya CCM,mawaziri na mibunge).
Zanzibar, kupitia kwa Samia sasa hivi inatengeneza muundo wa muungano wanaoutaka wao bila ya kuwashirikisha walioungana nao.
Hawa wanaamrishwa kutekeleza tu!