Sasa itabidi tuweke utaratibu wa namna hiyo kwa kila mkoa.
Nimeuliza wapi makubaliano ya 'Tanzania na Kigoma' kuhusu kilimo cha Mawese?
Wapi makubaliano ya Tanzania na Mwanza kuhusu dhahabu na Almasi?
Wapi makubaliano ya Tanzania na Rukwa kuhusu Mahindi?
Huu ni ujinga wa kipekee kabisa.
SSH ameamua liwalo na liwe, na kafanikiwa sana si kuutikisa muungano bali kuuvunjilia mbali
So far kule Kisonge wanashangaa kama huyu ni 'mwenzetu au ni Mwenzao'
Hawa watu kazi imewashinda kila mahali.
Hawa wanaosaini ni matumbo tu hakuna anayejali mtoto wake na kijukuu kitaku na amali gani.
Tunawajua, ni VP , PM na Speaker. Halafu wapambe wao mawaziri. Siku Tanganyika ikirudi hatutaki kuwasikia
Mafao yenu mtayapata Tanzania !
Sina shaka hilo nalo waziri kapewa kama agizo toka kwa Samia, ili kuipa uzito mkubwa Zanzibar, ionekane kuwa na hadhi sawa na serikali ya Tanzania.
Kuna waziri mmoja mwanamana aliondolewa kwasababu tu alishauri jambo kinyume na 'maagizo' kutoka juu
Watu hawayaoni matendo haya na kuyaelewa vizuri, ili wayape uzito unaostahili.
Bandari imesaidia sana kuwaonyesha Watanganyika matundu mengi, hata hili linaonekana kwasababu kila anachokifanya SSH watu wanakifuatilia. Unakumbuka bill za umeme zimefutwa kwa maagizo ! Makamba alitenda tu lakini maagizo yalitoka juu. Kwamba Wazanzibar walipiwe bill za umeme na mama ntilie wa Ilala! sad
Matukio yote haya ni alama za Samia kuutengeneza muungano uwe wanavyoutaka wao, Zanzibar.
Na ndicho kinaendelea. Zile kero 20 za Wazanzibar kazimaliza yeye na Rais Mwinyi. Think about that
Na mijitu ya Tanganyika ipo inakenua tu meno (nawazungumzia viongozi waliomo ndani ya CCM,mawaziri na mibunge).
Tunawaona na tuna majina yao, ipo siku tutawauliza kuhusu haya. Ipo siku watoto wao wataogopa kunasabishwa na majina ya baba zao kwasababu majina tu yatakuwa ''sumu''
Zanzibar, kupitia kwa Samia sasa hivi inatengeneza muundo wa muungano wanaoutaka wao bila ya kuwashirikisha walioungana nao.
Hawa wanaamrishwa kutekeleza tu!
Bila kuwashirikisha waliobeba muungano kwa gharama kubwa. Samia anachofanya ni kuwapa tu wanachotaka bila kuwawajibisha. Sasa hivi mizigo inaingia bure Zanzibar inaletwa bara, halafu Mtanganyika anatozwa kodi kwasababu hakuna mapato. Zanzibar ni uchochoro wa kupitishia bidhaa tu kuja bara. Hiyo ni kazi yake na amefanikiwa
SSH amemaliza kero ya Muungano kwa kuua. Ahsante