Tanzania, Zanzibar zasaini Hati ya Makubaliano Sekta ya Madini
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili zilizopo katika upande wa Muungano ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta manufaa kwa pande zote mbili.

Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam Dkt. Biteko amewataka watendaji wa wizara hizo kusimamia utekelezaji wa makubaliano

“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalitupa dira mpya katika kuendeleza mashirikiano yetu, hivyo tulichosaini leo sio kwa ajili ya kupiga picha bali ni kwa ajili ya kazi tuliyojipatia, natamani kuona mambo tuliyosaini hapa yanakuwa mfano na yanafanyika kwa weledi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili,” amesema Dkt. Biteko

Aidha, Dkt. Biteko amewataka watendaji wakuu wa pande zote mbili kusimamia masuala hayo ili yaweza kutokea huku akitaka kuanza kusimamia masuala ambayo hayahitaji rasilimali fedha kubwa ikiwemo kufanya tafiti hivyo yale yanayowezeka yaanziwe kufanyiwa kazi leo na sio kungoja.

Pia, amewataka Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza timu ndogo ya kusimamia makubaliano hayo ili kuhakikisha ushirikiano huo unadumu na kuwa wa mafanikio katika pande hizo mbili.

Naye, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan amesema utiaji wa saini wa makubaliano hayo usiishie kwenye makaratasi bali ufanisi na utendaji unaotakiwa kuonekana ukaonekane.

“Kitendo kinachofanyika leo ni kitendo muhimu sana kwa kwa pande zote mbili ambapo viongozi wetu wa juu wamekuwa wakitusisitiza kuendeleza mashirikiano ambapo tunategemea kushirikiana hasa katika suala la utaalamu hususan katika kufanya tafiti kwa pamoja,” amesema Hassan.

Pia, Hassan amesema ushirikiano huo utazaa toka kwa pande zote mbili za muungano na kuwataka watendaji wa wizara yake kufanya kile kinachowezekana kunyika leo na wasingoje kesho.

Jumla ya Hati Tano za Makubaliano zimesaniwa kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Mafuta, Madini na Gesi Asilia, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Kituo cha Jemolojia na Tanzania (TGC)
Tuna safari ndefu.
 
Walioungananao niTanganyika hiyo Tanganyika yenyewe haionekani inayoonekana ni Tanzania kwa hiyo zanzibar kasaini hayo mashirikiano na huyo anaeonekana ambae ni Tanzania

Sent from my ATU-L31 using JamiiForums mobile app
Zanzibar yeye hayumo kwenye hiyo "Tanzania" unayoizungumzia hapa?

Kwa hiyo Zanzibar kaungana na Tanzania ya wapi?
 
Safi sana, mambo ni IGA tu. Hakuna cha mjomba wala shangazi.
 
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?"
 
Mambo mengine yanafikirisha sana ujue, Katika pita pita zangu Leo nikakuta eti serikali inasaini mkataba a.k.a hati ya Makubaliano ya madini na serikali ya Zanzibar.

Nikawazaaaa nikashindwa kujiuliza, ni lini Tanganyika nao watasaini mkataba au Makubaliano yoyote tu na serikali ya Tanzania??

IMG-20230720-WA0061.jpg
 
Wakati Majirani wetu wanajitayarisha na Utengano. Tujiulize....


Ni Lini serikali ya Tanganyika itasaini hati ya Makubaliano (wowote) na serikali ya Tanzania kama walivyofanya serikali ya Zanzibar?​

👆✍️🤝
Natamani utungwe mdundo wa Mdumange, Singeli, na Hata Mdundiko unaoendana na Hoja hiyo!
 
Tuseme ukweli, Mwalimu Nyerere ni Moja ya akili kubwa mno kuwahi kutokea duniani na sio rahisi kueleweka Kwa watu wasiotazama mbali na siku upinzani wakimulewa Kwa walau asilimia 30 ,siku hiyo watakuwa wamekomaa kisiasa na watastahili kuongoza nchi Lakini Cha kusikitisha mpaka Sasa hakuna yeyote aliyepo upinzani aliyepata kumuelewa Mwalimu Kwa walau asilimia 5.
 
Tuseme ukweli, Mwalimu Nyerere ni Moja ya akili kubwa mno kuwahi kutokea duniani na sio rahisi kueleweka Kwa watu wasiotazama mbali na siku upinzani wakimulewa Kwa walau asilimia 30 ,siku hiyo watakuwa wamekomaa kisiasa na watastahili kuongoza nchi Lakini Cha kusikitisha mpaka Sasa hakuna yeyote aliyepo upinzani aliyepata kumuelewa Mwalimu Kwa walau asilimia 5.
"Tuseme ukweli, Mwalimu Nyerere ni moja ya akili kubwa mno kuwahi kutokea duniani"- takataka hii
fetchimage.jpg
 
Akili kubwa sana. Swali hili halijibiki kwa akili ndogo ya CCM
Unakosea sana, tena sana. Manake unachotaka kusema ni kwamba hakuna wana CCM wanaopinga Mikataba mibovu! Kwamba ni juhudi za Vyama vya Upinzani tu ndivyo vinavyo tetea Masilahi ya Watanzania.

Hapana. Usifanye hivyo.

Jaribu kusoma nyakati, hili ni suala la Watanganyika wote! Watanzania wote, Watu wote!

Walioibua swala la Mkataba wa Bandari ni Wana CCM, waliojitokeza kudadavua na kuuchambua Mkataba ule ni wana CCM na Wengine wa Vyama vya kisiasa. Mkataba huu wa sasa na hoja hii ya sasa(mada hii) ni matokeo ya moja kwa moja na suala la Bandari....bila kusahau hoja ya Utanganyika. Unachofanya ni kupunguza nguvu za Mshikamano uliojitokeza kupinga, na Kurekebisha suala zima la Muungano na UTanganyika...
 
Back
Top Bottom