Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Tutajua ukweli tu, maaana nyie kwa uongo,corona, makinikia, waongo kama shetani,
 
Mali za serikali ziuzwe Kwa minada ya wazi na itangazwe kwenye gazeti la serikali na vyombo vya habari washirika, kuepuka watu kitu cha thamani ya milioni 200 wanajiuzia Kwa milioni 3
kwani unadhani ni sababu zipi zimepelekea tamisemi kutenga bajeti ya magari mapya ya viongozi hayo waliyo nayo unahisi yanakwe da wapi mkuu nchi inachezewa kila dansi
 
Wewe na hao wikileak mnatofauti gani unakuja na maneneo matupu,leta hizo invoice tuzione.
 
Mapato ya serikali kupotea, mapato ya halmashauri nyingi kupotea Kwa wakusanyaji kutumia machine fake za EFD, utolewaji wa control number fake idhibitiwe mifano ni mbeya, makambako kulingana na ripoti ya CAG, liangalieni hili Kwa umakini na lipo halmashauri nyingi
 
Himizeni sana pesa za vijana huko vijijini na miji mbalimbali, vijana wapewe kipaumbele waweze kujiajiri kwenye ufugaji na kilimo, na sio pesa kupewa Kwa kujuana au watu wachache wanafoji nyaraka na kujichotea mikopo hiyo hii ni hasara Kwa nchi
 
Huyu mwamba kwenye utawala wa mama hajibu comments.
Anaejibu ni Nape nae anajibia huko twitter tu na kama tujuavyo bila D mbili huwezi kua jf.

Huyu D mbili anazo ila ndo anazitumia vibaya.
Kama anasoma hizi reply kwenye uzi wake bila shaka atakua kapata jambo labda ashupaze shingo kama kawaida yao.

Hints.
Punguza tozo.
Punguza matumizi yasiyo ya lazima na ya anasa ya ninyi viongozi.
 
Mheshimiwa sisi vijana tunaelewa sana kazi mnayofanya kwenye awamu hii ya sita, hakika Mama anapiga kazi, Nchemba unapiga kazi.
2025 tunaendelea tulipo ishia
ILA Mheshimiwa usisahau kunipa U-DED hata kule Halmashauri za Mkoa wa Mtwara kule ndanindani.
Kama kijana niko na mzuka sana wa kuwatumikia Watanzania.
 
Ni vizuri kuja kujadili na wananchi mambo ya msingi katika kuendesha hiyo wizara muhimu. Wananchi wana mengi ya kukuambia ambayo yataongeza tija katika kukusanya na kutumia mapato yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…