Sawa waziri tumekuelewa na kukusikia ,,, lakin tukiachana na hayo ,,
Mwaka 2016 pale mlimani city ,,, ndiyo ilikuwa mwaka unatunikiwa udocta pale katika mambo hayo ya uchumi ..
Nakumbuka vizuri ,, kabisa mlitangulia ninyi ambayo kiidadi mlikuwa wachache sana ,,, afu sisi wa degree tukafuata ,, hakika alikuwa siku nzuri sana iliyofana sana ,, nikikumbuka zile ndelemo na vifijo tulizo piga mule ndani ni wazi wote tulikuwa na furaha sana bila shaka wote kati yetu hakuna apendaye kumbukumbu hii nzuri ifutike kichwani mwake ..
Lakini ,, mkuu wew unaona sawa kweli ?? Wenzio toka ule mwaka 2016 ,, toka tumeachana siku ile pale mlimani city ,, hatujawahi kupata kazi mwaka wa 8 huu mkuu tunaangaika vibaya mno mtaani huku ,,, maisha yamekuwa magumu vibayo mno mpaka yamepelekea baadhi ya jamaa tuliokuwa nao siku ile pale mlimani kupoteza maisha ,, japo nipo hai lakini pengine wiki au mwezi mmoja mbele na mimi pia nikawa miongoni mwa watakaongeza idadi tokana hali ngumu tunazopitia huku ...
Mkuu mimi naamini kwa nafasi uliyonayo ,,, ushawashi ulionao kwa namna fulani unaweza kuishawishi serikali kitoa ajira ,,, mkuu hali huku mtaani siyo nzuri ,,, bora kwa wanawake anaweza pata bwana tajiri akaolewa ,,, lakin kwa sisi wanaume hali ni ngumu sanaa.. muheshimiwa wewe ukiwa kama waziri ,, ukiwa kama mwanaume mwenzangu ,,, lakini pia mimi nikiwa kama mdogo wako ,,, tafadhari tusaidieni wenzeni Ajira ,,, umri unatutupa mkono hatuna mbele wala nyuma ,, hatuna familia hatuna kazi ,, tafadhari tuoneeni huruma wenzenu ..