Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Mheshimiwa sisi vijana tunaelewa sana kazi mnayofanya kwenye awamu hii ya sita, hakika Mama anapiga kazi, Nchemba unapiga kazi.
2025 tunaendelea tulipo ishia
ILA Mheshimiwa usisahau kunipa U-DED hata kule Halmashauri za Mkoa wa Mtwara kule ndanindani.
Kama kijana niko na mzuka sana wa kuwatumikia Watanzania.
Hauna mzuka wowote njaa inakuuwa tuu nyie ndiyo mkipewa madaraka mnaanza ufisadi wenu hatutak machawa kama nyie
 
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya.

ndugu waziri,
Chapa kazi tu,
kama Taifa tuna Imani na Dr. Samia Suluhu Hassan, lakini pia tuna Imani nawe katika kusimamia rasilimali na uchumi wa Taifa letu, kwa maslahi mapana ya waTanzania wote 🐒

daima tutawapuuza wazushi na waongo kama ulivyo shauri..

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kama unadhani Ulaya nchi zinaendelea kwa tozo na kodi basi wewe ni kilaza wa mwisho.
Maendeleo ya sayansi na teknolojia ikichagiza uzalishaji wa mali viwanda ndiyo chachu kuu ya maendeleo ya nchi za Ulaya.
Wewe hauna biashara ya maana unayofanya,una import mpaka sindano unategemea ujenge nchi kwa tozo na kodi si utakua punguani!?
Uliza Ulaya;
-Mauzo ya magari.
-Mauzo ya silaha.
-Mauzo ya mali za kawaida za viwanda kama nguo,fenicha,mipira,vipuli, n.k n.k. Vinawaingizia pato kiasi gani katika mataifa yao.
Wenzenu Ulaya wamefanya mass industrialization kiasi wamepunguza mass importation imefanya kulinda hela kwenda sana nje na wanafanya mass exportation ili kuingiza zaidi pesa za nje.
Wewe unategemea ujenge nchi kwa tozo na kodi ambazo hujatengeneza mazingira wezeshi ya raia kuajiriwa wala kujiajiri/kuwekeza.
AISEE hii nchi ina safari ndefu sana.
Ndiyo vijana wenu hao halafu kesho kutwa amechaguliwa kuwa kiongoz kisa alikuwa anasifu na kuabudu
Mtegemee ataleta mabadiliko
Hii tabia ya uchawa ni mbaya sana
 
Hizi ni taarabu tu kama za khadija kopa na kina leyla Rashidi, sisi tukuamini vipi sasa...
Nyie wanasiasa mlivyo waongo, leta uthibitisho
 
Punguzeni magari kwenye misafara yenu, mnatuumiza.

Swala la ajira kwa vijana litawagharimu sana kama Kenya, muulizeni JK aliwezaje kuajiri kila mwaka, nyie mnafeli wapi?

Na mbona hakuna mradi mpya wa maana mnaoanzisha? Mnatembelea alipopita mwendazake, hamna vision au hamna hela?

Mwisho,mbona tukiwaombea dua mbaya kwa mnavyotutesa haziwashiki ndio kwanza mnazidi kupeta,mnafanyafanyaje
Mganga wao mkali sana.
 
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya.

Watanzania siku hizi Wala hayo hayatuhusu, si tuna focus na yetu, hii nchi si yenu bana, tozo zetu,kikokotoo chetu, ukosefu wa ajira wetu, maisha magumu yetu. Nyie endeleeni kula Bata sisi tupambane na yetu. Kila mtu ashinde mechi yake.
 
Punguzeni magari kwenye misafara yenu, mnatuumiza.

Swala la ajira kwa vijana litawagharimu sana kama Kenya, muulizeni JK aliwezaje kuajiri kila mwaka, nyie mnafeli wapi?

Na mbona hakuna mradi mpya wa maana mnaoanzisha? Mnatembelea alipopita mwendazake, hamna vision au hamna hela?

Mwisho,mbona tukiwaombea dua mbaya kwa mnavyotutesa haziwashiki ndio kwanza mnazidi kupeta,mnafanyafanyaje
😂😂😂 Hapo kwenye Dua mbaya kama kweli vile.
 
Wanatutwisha mizigo ambayo wao wenyewe hawaigusi hata kwa vidole vyao, malipo ya wakandarasi toka mwezi wa tano yamekuwa rejected, wakati huo huo TRA wao wanakaba walipwe, mabosi TRA wanajilimbikizia mali za za kutisha, wanamdanganya raisi wafanyabiashara wanakwepa kodi ili kumpumbaza raisi asiyaone maovu yao, ajabu raisi naye kanasa mtegoni, haya yote hatajibu kwani hayamuumizi yeye, lakini siku zinakuja atayajutia haya yote...😭😭😭😭😭
 
Mbona hamjalipa madeni ya wazabuni miezi 7 sasa
Anayaita madai ya wakandarasi madeni " "MADOGO MADOGO" my brother, munaumiza watu hamlipi, than unatoa kugha za kejeli?! Dharau?! Cha ajabu wapo wakandarasi hususan wa Dar, wanalipwa kiaina sijui wanapita njia/mbinu gani😭😭😭😭
 
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya.

Uko vizuri Dk. Waziri.
 
Nilikuwa sijui Mwigulu Nchemba yuko JF.
Nyie ndio watoto wa juzi na mmeharibu sana JF hii. Awali JF ilikuwa uwanja mpana sana wa majadiliano bila woga na kuheshimiana na karibu Mawaziri wote senior walikuwa humu, wanasiana wote mashuhuri na watendaji wa taasisi zote uzijuazo na taasisi zenyewe zikawa na page zake.
Lakini vijana wa kitanzania wa hovyo mkaingia humu na matusi na kejeli hivyo jukwaa likadharaulika.
Kulikuwa kukishushwa nondo zilizoshiba za kina DR Slaa na ma profesa kadhaa hadi unasahau kazi ili usome hoja.
Sasa wamejaa kina Lucas Mwashambwa & company JF imekuwa kikundi cha kwaya ya mapambio na kuabudu utadhani watu tumekatwa vichwa!
 
Hizi ni taarabu tu kama za khadija kopa na kina leyla Rashidi, sisi tukuamini vipi sasa...
Nyie wanasiasa mlivyo waongo, leta uthibitisho
That's very true mkuu. Huyu waziri kwa maelezo yake tunamtofautisha vipi na jamaa wa TanzaniaLeaks? Unapinga uongo kwa kutuletea porojo tena msomi wa PhD, unataka tukuelewe vipi?
 
Hata Raisi wetu Samia Suluhu Hassan ajiunge na JF sio kusoma tu awe anapangua Hoja zetu kuhusu mambo mbali mbali yanalolihusu hil Taifa letu.
Hii ingekuwa jambo jema sana kwake kwa namna alivyozungukwa na wahuni.
Angejiongezea upeo kurahisisha namna anavyopaswa kuongoza nchi.
 
Back
Top Bottom