Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Attachments

  • kanumba.jpg
    kanumba.jpg
    12.4 KB · Views: 1,479
hawa waandishi wa habari ni wakupiga vibao, muda kama huu ni mzito sana kwa familia ya kanumba hasa mama mzazi alafu hawa wapuuzi wanaenda kuinterview, waache familia iombeleze na Mungu awape nguvu ya kuvuka kipindi hiki kigumu. R.I.P Kanumba

Sioni baya walilolifanya hapo. Kama wanafamilia wangeona kuna ubaya basi wangekataa kuhojiwa na kama hao wanahabari wangeendelea kuwasumbua baada ya kukataliwa hapo ndiyo ningeona kuna tatizo.
 
sasa kama usiku huo walikua wawili ndani tena chumbani,hawakua wamefanya kitu?kama watakua kuna kitu walifanya before je kanumba alipata hata mda wa kutubu kidogo?hamna kitu kibaya kama kufa kwenye dhambi.

Umenishangaza na swali kama hili!
Wewe unajuaje hatma yako kama utapata muda wa kutubu?
Siri ya kifo aijua Mungu peke yake.
Tusiwazidishie machungu wafiwa kwa kuwapa mtihani usiokuwa na majibu
kwa maana hata wewe unadhania tu.Hakuna anayejua kipimo cha maamuzi ya Mungu ukifika mbele ya haki!

R.I.P Kanumba na Mungu akusamehe makosa yako
awajalie wasanii wenzio kutanabahi na kujifunza kutokana na kifo chako cha ghafla.

Msiba huu uwe kama chimbuko la kurudisha maadili kwa wasanii, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa hapa karibuni.Sanaa hasa ya uigizaji imegeuka kama sodoma na gomora. Jifunzeni kuwa na kiasi kwa kila jambo!

Na huyo mtoto/binti Lulu, tumwombee aweze kutubu kwa kusababisha kifo cha mapema cha nyota hii.

Wazazi wote wenye watoto wajifunze kitu kutokana na tukio hili la kusikitisha. Mzazi usipoweza kumkunja mwanao mapema basi atakuja kuvunjwa na dunia!

Wanaume wenye kupenda ndogo ndogo na nyie, jueni namna ya kuhimili mikiki.Ujue wasichana wadogo walioiona dunia ni balaa! Yahitaji uvumilivu maana hawana subira kama wale wa miaka ileee.Ukiwa nao, ujue wewe ni mmoja wa wengi wakware wenye kupenda vitoto vidogo vinavyopevuka ambavyo viko njia panda. Silaumu mtu bali natoa angalizo tu! Ukisema upambane na kuwabana kwa ukali na vipigo, utaishia kwenye usawa wa futi 6 au utaozea jela.

Wenye kutumia mabavu badala ya majadiliano kwenye migogoro, sina haja ya kurudia kuwa hailipi.Rusha ngumi lakini kumbuka unaweza nawe ukarushiwa kombora likakulaza milele.

Tau.
 
Aisee maisha ya Mwanadamu ni kama maua,yanachanua then yananyauka.
 
ni makosa kusema huyu binti 'kamuua' kanumba
tusubiri ripoti kamili

Sio makosa ya hako kabinti...ni makosa ya marehemu mwenyewe. Tusimuhukumu huyu mdogo kabisa, badala yake tumsaidie aendelee kuwa binadamu wa kawaida hata baada ya hili balaa kupita. Ninashaka na uwezo wa akili yake kupambana na pressure za kikubwa na tunaweza kumfanya akaharibu au kuharibikiwa kabisa kama tuhuma zitaelekezwa kwake. Kanumba alikuwa anatembea na msichana mdogo kuliko umri wake. Anemsuburi akue kwanza.
 
Jamaa hawawezi tengeneza filamu hapo? Itabamba sana bongo wakiigiza
 
Bora kama alikuwa anamkumbuka hata za vitenge.
 
Prof Mtakyawa wa geology university of Dar na Bingu wa Mthalika wamekufa Leo! Ajabu msiba wa Kanumba umefunika hata msiba wa prof wa mawe

Wote rest in peace

Rt rev masa
 
Back
Top Bottom