Hazina tofauti.
Kuna mtu nimeona ameziita interceptor kama kuzitofautisha na Fighters yaani F-15,F-16 nk lakini nadhani ni kutojua kwa nini J-7G zinaitwa pia interceptor. J-7G ni version ya MIGs na ziliitwa hivyo wakati wa Cold War kwani zilikuwa na kazi kubwa ya ku intercept fighters za NATO. Lakini kiukweli nazo pia ni fighters kama zilivyo F series na zote zina uwezo mkubwa wa ku perform bullfighting. Tena hizi Mig zinasifiwa sana kwa Air Defence and Air superiority in general mpaka sasa. Kundi lingine la ndege linaitwa Attackers au A series,mfano A-10 attacking planes.Hizi kazi yake kubwa ni ku attack specified ground targets kama majengo,magari,vifaru,meli nk. Huwa si special for aerial/air to air fighting. Lakini habari zinasema kuna wataalamu wameshaunda ndege ambayo ni combination ya fighters na attackers zinaitwa F/As series. Kwa maelezo haya nadhani bado tuko vizuri tu kama tumechukua new J-7G sababu what we need more is superior air defence!