Some would dare say the real average of real GDP Per capita for "real" Tanzanians hovers around $ 300, bila kusahau vitoto lukuki vile ambavyo havijafikia umri wa uzalishaji na vizee vilivyokwishatoka katika uzalishaji, wamachinga wasio uzalishaji au wenye uzalishaji mdogo na un/underemployment.
Some would say that, and I will have a hard time disputing that.
You made real points; but only one issue: Uongozi ni Mbaya kupindukia hasa wakati wa Mwinyi na Kikwete; tenganisha: Mwinyi alivuruga all macroeconomy Mkapa akatengeneza (ingawa baadaye aliiba); kikwete hatuelewi anafanya nini! Kumbuka kuwa Mwinyi alivuruga na kuiba (ingawa kuiba kwake hatukuoni). Bob be fair on this!
Heheheheheheeeee....Pundit economics makes me laugh.....
Nimefurahishwa na post ya Masanja na reaction yake. I just wish if all Tanzanians were aggressive like him hata kwa maneno tu inatosha. Speaking of maisha vijijini, sijui wangapi mmekulia au mmetembela vijijini. Kwa wale wa Kilimanjaro na vijiji vingine vyenye maendeleo nisingependa mjihesabie kwamba mmekulia vijijini maana huko kuna umeme, maji, zahanati etc. Mimi nimebahatika kutembelea kanda ya ziwa, hasa maeneo ya mkoa was Shinyanga. Huku nafikiri ndio mtu unapata picha halisi ya umaskini. Hili eneo ni kama sana wakati wa kiangazi. Wanyama hukonda sana kwa kukosa maeneo ya kuchungia kutokana na ukame uliokithiri. Huduma za kijamii katika vijiji vingine hazipo kabisa. Mfano, unakuta bwawa la maji ya mvua, ndio ng'ombe wanakunywa maji na kunya humo humo, wanakijiji wanafua, kuoga na kuchota maji hayo hayo kwaajili ya kunywa na matumizi mengine nyumbani. Na baada ya kiangazi kifupi tu, mabwawa haya hukauka na wananchi hulazimiki kufuata maji umbali mrefu. Huduma za afya ndio balaa. Zahanati ziko mbali sana na vijiji. Watu wanasafiri for more than 100kms kwa kutumia baiskeli au mkokoteni wa kuvutwa na punda kwenda kwenye zahanati ambazo hazina dawa.
Nina mengi ya kuandika hapa, maana kazi yangu ya utafiti madini inanipeleka katika vijiji vingi na kujionea hali ilivyo ya kutisha. Tuzidi kusali sana!
Nimefurahishwa na post ya Masanja na reaction yake. I just wish if all Tanzanians were aggressive like him hata kwa maneno tu inatosha. Speaking of maisha vijijini, sijui wangapi mmekulia au mmetembela vijijini. Kwa wale wa Kilimanjaro na vijiji vingine vyenye maendeleo nisingependa mjihesabie kwamba mmekulia vijijini maana huko kuna umeme, maji, zahanati etc. Mimi nimebahatika kutembelea kanda ya ziwa, hasa maeneo ya mkoa was Shinyanga. Huku nafikiri ndio mtu unapata picha halisi ya umaskini. Hili eneo ni kama sana wakati wa kiangazi. Wanyama hukonda sana kwa kukosa maeneo ya kuchungia kutokana na ukame uliokithiri. Huduma za kijamii katika vijiji vingine hazipo kabisa. Mfano, unakuta bwawa la maji ya mvua, ndio ng'ombe wanakunywa maji na kunya humo humo, wanakijiji wanafua, kuoga na kuchota maji hayo hayo kwaajili ya kunywa na matumizi mengine nyumbani. Na baada ya kiangazi kifupi tu, mabwawa haya hukauka na wananchi hulazimiki kufuata maji umbali mrefu. Huduma za afya ndio balaa. Zahanati ziko mbali sana na vijiji. Watu wanasafiri for more than 100kms kwa kutumia baiskeli au mkokoteni wa kuvutwa na punda kwenda kwenye zahanati ambazo hazina dawa.
Nina mengi ya kuandika hapa, maana kazi yangu ya utafiti madini inanipeleka katika vijiji vingi na kujionea hali ilivyo ya kutisha. Tuzidi kusali sana!
Inasikitisha sana
Kungekuwa na indicators nzuri tungeona "negative GDP" kila mwaka.
INGAWA itakuwa vigumu kubadili tabia za waandishi wetu wanakula na kunywa siasa lakini madhali fursa hii ipo acha nianze kuitumia. Na pengine kuna wawili watatu watakaoniiga na tukaanza kugonga hodi kwenye vichwa vya Watanzania kuwa mabadiliko ya hali zetu za maisha kutoka kwenye umasikini kwa walio wengi wa kutisha kwenda kwenye nafuu hayatakuja kwa kuwa mwanachama wa chama hiki au yule; au kwa kumpenda na kumpigia debe fulani awe rais; au kwa ahadi na mbwembwe za kisiasa bali kutokana na mikakati inayoweza kufuatiliwa na mimi na wewe ili kuiondoa nchi yetu kwenye GDP per capita ya kitoto ya $600 kisha tuipeleke kwenye $1,000 halafu $ 2,000 halafu $ 4,000 na ifikapo 2020 tuwe tupo kwenye ktu kama $12,000 hivi.
Zipo njia mbalimbali za kulipigia debe hili. Mimi nitaanza kwa kuziangalia wizara nyingi za nchi hii ambazo nafikiri zinajua zaidi ofisi zenye airconditioner kuliko challenges au changamoto za kukuza GDP per capita kwa kuangalia mambo yanayoangukia chini ya wizara zao.
Nifuatilie na katu hutosikitika kusoma maendeleo ya makala haya ya Tuzungumze Uchumi katika JF.
Karibu sana,
Tuanze na wizara gani? nawapeni challenge kwa hili. Semeni na mimi nitaonesha kwamba kila wizara inaweza kuwa na mchango kwa GDP per capita na hivyo maendeleo ya Watanzania wote. Ila nitoe onyo: Lazima ufisadi uwe nje, ubinafsi nje, kujitajirisha na kujilimbikizia mali kiasi unaziacha zote ukifa zitumiwe na wahuni na wakora na mpaka wabaya wako nje; ahadi zisizo na fikra nje; uvivu nje; misaada toka nje, nje na longolongo zote nje.
TUFIKIRIE tU kuongeza GDP per capita kwa kile tulicho nacho, akili, maarifa, rasilimali chache zilizopo bila kuweka matumaini ya kusaidiwa na nchi hi au ile.
Ninashauri muangalie website hizi:
A. Human Development Index
SOMA Basics za Human developmen t Index-[Ikitumiwa vizuri tunaweza kunyanyua DDP Per Capita yetu]
B. Mo Ibrahim Index of African Governance
TUZO LA MO IBRAHIM [Ukiwa Rais huna haja ya kuiba tena labda umezaliwa mwizi na utakufa mwizi!]
Mo Ibrahim anatoa zawadi kwa kiongozi wa Afrika anayetawala vizuri na kuleta maendeleo ya kweli nchini mwake. Zawadi hii inamzuia kabisa mtu mcha-Mungu, mpenda watu wake na anayegombea uongozi sio kwa faida yake bali kwa sababu za kuitoa nchi yake kwenye aibu ya umasikini wakati nchi ina kila sababu ya kuwa tajiri KUTOKUWA NA SABABU YA KUIBA NA KUJILIMBIKIZIA MALI KABISA KABISA! Ila tu kama kiongozi huyo ni mtu aliyezaliwamwizi na atakufa mwizi!
Je, mmepata mwanga wa vitu gani tunavyoweza kuviangalia ili kuhakikisha harakati za kuongeza GDP per capita kwa maneno bora zaidi UHURU KWA GDP per capita kwa Mtanzania uje ni zipi?
READ THIS TOO:
GDP dollar estimates for all countries are derived from purchasing power parity (PPP) calculations rather than from conversions at official currency exchange rates. The PPP method involves the use of standardized international dollar price weights, which are applied to the quantities of final goods and services produced in a given economy. The data derived from the PPP method provide the best available starting point for comparisons of economic strength and well-being between countries. The division of a GDP estimate in domestic currency by the corresponding PPP estimate in dollars gives the PPP conversion rate. Whereas PPP estimates for OECD countries are quite reliable, PPP estimates for developing countries are often rough approximations. Most of the GDP estimates are based on extrapolation of PPP numbers published by the UN International Comparison Program (UNICP) and by Professors Robert Summers and Alan Heston of the University of Pennsylvania and their colleagues. In contrast, the currency exchange rate method involves a variety of international and domestic financial forces that often have little relation to domestic output. In developing countries with weak currencies the exchange rate estimate of GDP in dollars is typically one-fourth to one-half the PPP estimate. Furthermore, exchange rates may suddenly go up or down by 10% or more because of market forces or official fiat whereas real output has remained unchanged. On 12 January 1994, for example, the 14 countries of the African Financial Community (whose currencies are tied to the French franc) devalued their currencies by 50%. This move, of course, did not cut the real output of these countries by half. One important caution: the proportion of, say, defense expenditures as a percentage of GDP in local currency accounts may differ substantially from the proportion when GDP accounts are expressed in PPP terms, as, for example, when an observer tries to estimate the dollar level of Russian or Japanese military expenditures. Note: the numbers for GDP and other economic data can not be chained together from successive volumes of the Factbook because of changes in the US dollar measuring rod, revisions of data by statistical agencies, use of new or different sources of information, and changes in national statistical methods and practices.
Sammy,
Ahsante kwa maada yako murua.
Lakini napenda kusema kwamba, kama huonglei siasa kwa maan ya "si-hasa" ambapo nitakuelewa, nafikiri ni makosa kutaka kutenganisha uchumi na siasa, kwa sababu mfumo wa uchumi unategemea siasa (wajamaa wanafanya umiliki wa njia kuu za uchumi ziwe kwa watu wote, watu wa soko huria wanaamini katika umiliki binafsi wa mali na njia kuu za uchumi). Vile vile tunaona jinsi uchumi unavyoweza kuongoza matokeo ya siasa.
Ukiangalia kwa mfano sehemu ya serikali na mipango yake ya kiuchumi, kwa mujibu wa mifumo ya John Milton Keynes, ambayo mingi hufanywa kwa kufuata manifesto za kiuchumi zinazojengwa kwa nadharia na dira za kisiasa, utaona kutenganisha siasa na uchumi ni sawasawa na kutenganisha upande mmoja wa shilingi na mwingine, kama utaweza kutenganisha haitabakia kuwa shilingi.
Mimi naona, badala ya kutaka kutenganisha uchumi na siasa, tuweke mkazo zaidi wa kuwa na siasa zilizojikita katika uchumi, zinazoongozwa na sera madhubuti, zinazofuata matakwa ya wengi na zenye maono ya muda mrefu.
Pia ukiongea GDP per capita kimsingi unaongelea mchango wa kila mmoja, kwa hiyo ningependa kuona mkakati wa kuwahusisha wananchi kutoka chini kwenda juu, zaidi ya mkakati utakaoanza na kuangalia wizara na kupanga mambo kutoka juu kwenda chini.Kwa maoni yangu mpaka sasa tupo hapa katika umasikini kwa sababu watu wa juu hawajui matatizo ya wachini, na wachini hawawezi kuwafikia wa juu kuwaeleza matatizo ya kweli. Ikifikia muda mtu wa chini amefika juu anakuwa kashachoka na kukata tamaa kwamba matatizo yetu hayatatuliki na mwishowe anaishia kujitafutia maisha yeye na familia yake, ndiyo maana ufisadi unakuwa sugu.
Kuna mengi lakini kwa sasa ni hayo.