Tumeona katika sehemu iliyopita kwamba nchi inaweza ikatajirika au kinyume chake kuondokana na umasikini kwa kufanya mambo kadhaa. Baadhi yake yalikuwa:
. kuongezeka kwa rasilimali zilizopo nchini,
. kugundulika kwa teknolojia mpya,
. kuongezeka kwa kiwango cha matumizi ya rasilimali nchini,
. kuongezeka kwa mgawanyo wa kazi na uzamili, na
. kupanuka na kuboreshwa kwa mgawanyo wa rasilimali katika nchi.
Kwa yakini ukitaka kutathmini mafanikio ya serikali yoyote duniani basi unastahili kuanzia hapa.
Hata hivyo, sintojiingiza sasa hivi katika kutathmini utendaji kazi wa serikali iliyoko madarakani. Hilo kwa sasa nakuachia wewe kwa kuangalia kama serikali yako imemudu kiasi gani kufanya hayo hapo juu yawezekane hapa nchini.
Kwa leo, ninapenda kuuliza je, hizo hapo juu ndio njia pekee ambazo nchi inaweza ikaongeza utajiri wake au kupunguza umasikini wake? Nina hakika jibu lenu litakuwa la hasha!
Hebu tujiulize ni njia gani nyingine ambazo tunaweza kuongeza uzalishaji mali, huduma na hivyo utajiri nchini na wakati huo huo kupunguza kabisa umasikini wa kutisha?
Unaweza ukauliza swali au maswali juu ya hili kwa kutumiia muundo wa serikali au maeneo ya kijiografia au maeneo ya uchaguzi au kisekta, kwa maana ya kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda, biashara, ajiranchizanje, huduma na bila kusahau michezo na muziki.
Hata hivyo, mimi nitauliza kijumla jumla tu kwa kuuliza, je, tunaweza kuongeza uzalishaji mali, utoaji huduma na biashara na hivyo kuongeza utajiri wetu kwa njia hizi:
. kuigeuza serikali a 'Learning Organization' yaani tufanye mamboyetu yaendeshe vizuri kiasi cha kutamanisha serikali zingine kutuma watumishi wao kuja kujifunza uendeshaji serikali nchini kwetu?
. Kugeuza baadhi ya Wizara nchini kuwa Agencies ili sio tu kuongeza ufanisi bali kupunguza gharama za uendeshaji serikali na pengine kuwa katika nafasi ya kuliingizia taifa kipato cha uhakika? Masuala ya kiutawala kama ya Muungano/Afrika Mashariki,Serikali za mikoa na mitaa, Utumishi, Bunge na Mazingira mathalani yanaweza kuendeshwa na agencies kwa ufanisi zaidi kuliko kuwa Wizara kama ilivyo sasa?
. Kutumia balozi zetu kama vituo vya 'intelligence' kuhusu mbinu mpya za kiuchumi, biashara, fedha na rasilimali watu ili tufyonze vilivyo muhimu na kuvitumia haraka kwa maendeleo yetu?
. kutumia balozi zetu kama 'branch' za kibiashara katika kusaidia Watanzania bila upendeleo au ujanja ujanja ili waweze kununua na kuuza vitu nje kwa urahisi?
. Kuzihamasisha benki zetu kufungua matawi nje ya nchi?
. Kurahisisha taratibu za uanzishwaji SACCOS kwa kuondoa masharti magumu wakati wa uanzishwaji SACCOS. Wengi wanakata tamaa kwa sababu wanachama waanzilishi wanashindwa kuweka fedha benki mpaka wapate hati ya SACCOS. Je, hivi ni big deal kuwa na Akaunti ya Muda ili watu waendelee kuaminiana na kulipa au kuweka wanachostahili kwenye akaunti ya SACCOS tarajiwa?
. Kutoa upendeleo kwa benki zinazowakopesha wakulima, wafugaji, wavuvi, wafuga nyuki, wachimbaji madini wadogowadogo na wafanyabiashara na nchi za nje wadogowadogo?
. Uanzsihwaji wa viwanda vidogo vijijini?
. Kununua bidhaa na vifaa toka nje na kuviuza kwa majirani zetu na hususan Kongo, zambia, Malawi, Rwanda, Burundi na kadhalika,
. Kuwashirikisha watu kwa kuwalipa na kuhakikisha wanacholima hakikwami njiani au mashambani bali kinasafirishwa kwa urahisi hadi masoko ya ndani au nje?
. Kuwa na wakala wa maendeleo ya viwanda, wakala wa maendeleo ya biashara ya ndani na nje?
. ATC kuachana na ndege za abirria na kuwa na mijidege mikubwa ya kusafirisha mizigo toka Uarabuni na uchina kuja Tanzania na kinyume chake?
. Kuigeuza Tanzania na hasa miji yetu ya mipakani kama Holili, Horohoro, Mtukula, Isaka, Tunduma, Mbamba Bay, Taveta, Namanga na kadhalika kuwa MASOKO makubwa ya kimataifa kwa kugeuza border posts zetu kuwa kama vile viwanja vya ndege vya kimataifa kwa kuwa na majengo makubwa ya maduka na bohari?
. Kuwa na Wakala wa Umwagiliaji Maji?
. Kurahisisha ubia kati ya wakulima nchini na watu au wakulima wa nje?
. Kuwa na meli za kisasa za uvuvi katika mito, maziwa na bahari zetu?
. Kwa Kampuni za dhahabu, almasi, tanzanite, ruby na kadhalika kulipa royalty kubwa zaidi inayotosha kuipa BOT/Hazina uwezo wa kukidhi mahitaji madogo madogo kama gharama za elimu kwa watoto wetu na ziada ya kuwakopesha wazawa?
. Kufanya miji na vijiji vyetu safi zaidi na hivyo kufanya watalii kukubali kuvitembelea kwa urahisi zaidi,
. Kuhakikisha mali asili yetu inauzwa kwa bei nzuri na kuna uwazi katika biashara hii,
. Hotelii na huduma zingine za kiswahili kama vile usafiri vinaimarishwa na hivyo kuipa nchi hadhi bora zaidi machoni mwa wageni na hususan watalii,
. kuanzisha shughuli za utafiti & Maendeleo kwa madhumuni ya kugundua, kuzalisha na kusambaza nishati mbadala vijijini?
. Kuhakikisha fedha zinazotojka mabarabarani zinarudi kukarabati barabara na sio vinginevyo?
. Kuhakikisha tunakuwa na bandari tatu kama sio nne zinazofanya kazi usiku na mchana bila wizi wala kuinyima serikali mapato ya kodi?
. Kuongeza matumizi ya teknohama kiwango cha kufikia kuwa tunaweza kupunguza gharama zinazotokana na safari, barua na mikutano isiyo na sababu za kutosha,
. Kuanzisha SAMPULI za miradi ya sayansi & teknolojia ili vijana wetu waweze kuiga na kupitia elimu ya ujasiliamali na menejimenti ya biahsara waweze kuanzisha shughuli za kiuchumi zinazoendana na vitu hivyo?
. Kuongeza ubora wa maisha ya walimu na wahadhiri na ubora wa vyuo na shule zetu ili tupate wanafunzi toka nchi za nje?
. Kuongeza ubora wa maisha ya madaktari, manesi na wafanyakazi wa mahospitali na ubora wa vifaa, mitambo na huduma za hospitali zetu ili tuweze kupata wagonjwa toka nchi za nje kwa wingi zaidi?
. Kurahisisha ujenzi wa nyumba kwa kila familia ya Kitanzania?
. Kuifanya miji yetu iwe mizuri na safi zaidi siku zote?
. Kuhakikisha vyombo vyetu vya habari-redio na magazeti vinasikika hadi nje ya nchi na hivyo kupata uwezekano wa matangazo toka nchi za nje?
. Kuwa na magazeti na vitabu vinavyoweza kuuzwa hadi nchi za nje?
. Kuuza au kuruhusu kwenda nje wanamichezo na wanamuziki wengi iwezekanavyo nchi za nje?
. Kuangalia vipengee mbalimbali vya utamaduni wetu vinavyoweza kutumika kutuongezea heshima na mapato zaidi vikitumika kifundi na kwa ustaarabu zaidi?
. Kuhakikisha wahalifu au wenye kufanya makosa mbalimbali barabarani na kwingineko wanalipishwa faini zitakazochangia mifuko yetu ya maendeleo?
. Tunaboresha mbinu za ufugaji na uvivu na hivyo kuwa na biashara nzuri zaidi katika sekta hii?