joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Hilo ulilolisema la kukataza maandamano ndipo anapokosea, kwa sababu maandamano yameruhusiwa kikatiba, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kwenda kinyume na katiba, yeye angeyaona ni tatizo basi alipaswa kupeleka mswada bungeni hata kwa hati ya dharura kufanya marekebisho ya sheria ili kuondoa hicho kipengele, nchi inapaswa kutawaliwa kwa sheria, sio mtu anavyojisikia tu, vipi kuhusu mikutano ya hadhara mbona hataki ifanyike, mtu kama Lipumba, au Mrema, ambao ni viongozi wa kitaifa wa vyama vyao lakini sio wabunge, wakafanyie wapi mikutano ya hadhara ili wakanadi sera zao wananchi wawasikie?.Mkuu kuhusu Magufuli hajakataza wanasiasa kuongea, wanafanya mikutano kwenye majimbo yao na press conference kila siku na kumtukana Magufuli mpaka huko Bungeni,
Magufuli amekataa maandamano kwa nia njema kwamba ndio utaandamana lakini mwisho wa siku utawasilisha message kwa serikali ambayo pia wangeweza kupata hiyo message bila maandamano
Ambayo kihistoria maandamano Tanzania awamu ya kikwete ndio yaliyoua watu wengi kwenye siasa na kurudisha shughuli za maendeleo nyuma sana.
Kusudi la Rais kukataza maandamano ni kuchochea kuchapa kazi na kuacha siasa za maandamano ambazo hazitatui shida za wananchi hakuna maji, infrastructures, elimu bora, good Healthcare zinazopatikana kwenye maandamano.
Lakini ukumbuke enzi za Kikwete chuki kwa Rais ilikua ni mara tano ya unazozisikia leo kwa Magufuli.
Magufuli akumbuke kwamba japo yeye katika ligi iliyopita amekua mshindi kwa kuchukua kombe la ubingwa kama Chelsea kule uingereza, hapaswi tena yeye kuzipangia timu zingine namna gani ya kujiandaa kwa msimu wa ligi unaofuata, anayepaswa kupanga utaratibu wa maandalizi ya ligi zijazo ni chama cha mpira cha Uingereza kupitia kamati ya usimamizi wa ligi, ni katiba ya nchi kupitia tume ya uchaguzi, sio Magufuli aseme hili halifau, msifanyi hili linawapotezea muda wa kazi, mbona kipindi cha kampeni wa uchaguzi ukifika hatuachi kwenda kazini tunaendelea na kazi na kampeni zinaendelea?
Sent using Jamii Forums mobile app