Tanzania's Tundu Lissu recovering well at Aga Khan Nairobi

Tanzania's Tundu Lissu recovering well at Aga Khan Nairobi

Mkuu kuhusu Magufuli hajakataza wanasiasa kuongea, wanafanya mikutano kwenye majimbo yao na press conference kila siku na kumtukana Magufuli mpaka huko Bungeni,

Magufuli amekataa maandamano kwa nia njema kwamba ndio utaandamana lakini mwisho wa siku utawasilisha message kwa serikali ambayo pia wangeweza kupata hiyo message bila maandamano

Ambayo kihistoria maandamano Tanzania awamu ya kikwete ndio yaliyoua watu wengi kwenye siasa na kurudisha shughuli za maendeleo nyuma sana.

Kusudi la Rais kukataza maandamano ni kuchochea kuchapa kazi na kuacha siasa za maandamano ambazo hazitatui shida za wananchi hakuna maji, infrastructures, elimu bora, good Healthcare zinazopatikana kwenye maandamano.

Lakini ukumbuke enzi za Kikwete chuki kwa Rais ilikua ni mara tano ya unazozisikia leo kwa Magufuli.
Hilo ulilolisema la kukataza maandamano ndipo anapokosea, kwa sababu maandamano yameruhusiwa kikatiba, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kwenda kinyume na katiba, yeye angeyaona ni tatizo basi alipaswa kupeleka mswada bungeni hata kwa hati ya dharura kufanya marekebisho ya sheria ili kuondoa hicho kipengele, nchi inapaswa kutawaliwa kwa sheria, sio mtu anavyojisikia tu, vipi kuhusu mikutano ya hadhara mbona hataki ifanyike, mtu kama Lipumba, au Mrema, ambao ni viongozi wa kitaifa wa vyama vyao lakini sio wabunge, wakafanyie wapi mikutano ya hadhara ili wakanadi sera zao wananchi wawasikie?.

Magufuli akumbuke kwamba japo yeye katika ligi iliyopita amekua mshindi kwa kuchukua kombe la ubingwa kama Chelsea kule uingereza, hapaswi tena yeye kuzipangia timu zingine namna gani ya kujiandaa kwa msimu wa ligi unaofuata, anayepaswa kupanga utaratibu wa maandalizi ya ligi zijazo ni chama cha mpira cha Uingereza kupitia kamati ya usimamizi wa ligi, ni katiba ya nchi kupitia tume ya uchaguzi, sio Magufuli aseme hili halifau, msifanyi hili linawapotezea muda wa kazi, mbona kipindi cha kampeni wa uchaguzi ukifika hatuachi kwenda kazini tunaendelea na kazi na kampeni zinaendelea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli kabisa ila sio swala la wanasiasa pekee yake....what abt when he arrests musicians like Nay wa Mitgeo...kulikuwa na lyrics flani zilizomtaja rais na hazikumpendeza rais hivyo akaamrisha kukamatwa kwa mwanamziki yule...pili, mkurugenzi wa JF pia alikamatwa kwa kosa lipi? wanahabari wanafaa kukubaliwa kuripoti ukweli wa mambo hata iwe haimpendezi rais? au sio mkuu? angalia Marekani, CNN ABC etc wanaripoti mambo mabaya kumhusu Trump ila hawezi akaamrisha kukamatwa kwa yeyote ama kufungwa kwa kampuni yoyote...imagine na yule ni rais wa dunia ....
Mimi ninadhani hili la kuwakamata wanamuziki wanaoimba nyimbo za kumkashifu rais, kwanza sio kwa maagizo toka kwa rais walio wengi wanakamatwa kwa maagizo ya viongozi wa jeshi la polisi na usalama wa taifa kwa kumuogopa Magufuli, kwa mfano alipokatwa Ney wa Mitego, Magufuli alimpigia simu waziri wa sheria akamuambia mbona nimesikiliza mziki wake una maneno mazuri tu, muachieni tena mwambieni aongeze vipengele vya wala rushwa na madawa ya kulevya.

Lakini hata kama angekuwa anatoa maagizo wakamatwe, so long as utaratibu wa kisheria unafutwa, kama walivyokua wanafanya kwa Tundu Lisu, kwamba unakamatwa na ndani ya saa 24 unapelekwa mahakamani, hiyo ni sawa kabisa, tatizo ni pale kuwateka na kuwatesa kama alivyofanyiwa Roma Mkatoliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ulilolisema la kukataza maandamano ndipo anapokosea, kwa sababu maandamano yameruhusiwa kikatiba, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kwenda kinyume na katiba, yeye angeyaona ni tatizo basi alipaswa kupeleka mswada bungeni hata kwa hati ya dharura kufanya marekebisho ya sheria ili kuondoa hicho kipengele, nchi inapaswa kutawaliwa kwa sheria, sio mtu anavyojisikia tu, vipi kuhusu mikutano ya hadhara mbona hataki ifanyike, mtu kama Lipumba, au Mrema, ambao ni viongozi wa kitaifa wa vyama vyao lakini sio wabunge, wakafanyie wapi mikutano ya hadhara ili wakanadi sera zao wananchi wawasikie?.

Magufuli akumbuke kwamba japo yeye katika ligi iliyopita amekua mshindi kwa kuchukua kombe la ubingwa kama Chelsea kule uingereza, hapaswi tena yeye kuzipangia timu zingine namna gani ya kujiandaa kwa msimu wa ligi unaofuata, anayepaswa kupanga utaratibu wa maandalizi ya ligi zijazo ni chama cha mpira cha Uingereza kupitia kamati ya usimamizi wa ligi, ni katiba ya nchi kupitia tume ya uchaguzi, sio Magufuli aseme hili halifau, msifanyi hili linawapotezea muda wa kazi, mbona kipindi cha kampeni wa uchaguzi ukifika hatuachi kwenda kazini tunaendelea na kazi na kampeni zinaendelea?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mahali hapo juu paragraph ya pili from the bottom umesema ili wakanadi SERA zao watu wawasikie, hapo sijakuelewa sera za namna gani tena wakati uchaguzi umeisha.

Pili kuhusu kukataza maandamano na uhalali wa zuio hilo kikatiba sababu ya maandamano kuwepo kikatiba, kama nilivyoeleza kwenye post yangu sababu ya Rais kukataza maandamano, nataka utambue katiba hiyohiyo inampa Rais mamlaka ya kubatilisha hata baadhi ya yaliyomo kwenye katiba ila "kwa maslahi mapana na ustawi wa jamuhuri" ndivyo katiba inavyosema.

Katiba inampa Rais hata uwezo wa kubatilisha hukumu ya jaji iliyotolewa kisheria na kihalali kwa mtuhukumiwa (bila kupingwa au kuhojiwa na mamlaka yoyote) katiba hiyohiyo imempa Rais hayo mamlaka na afanyapo hivyo anakua amefanya kwa mujibu wa katiba ya nchi pasi na hatia na yupo sawa kisheria.
 
Kuna mahali hapo juu paragraph ya pili from the bottom umesema ili wakanadi SERA zao watu wawasikie, hapo sijakuelewa sera za namna gani tena wakati uchaguzi umeisha.

Pili kuhusu kukataza maandamano na uhalali wa zuio hilo kikatiba sababu ya maandamano kuwepo kikatiba, kama nilivyoeleza kwenye post yangu sababu ya Rais kukataza maandamano, nataka utambue katiba hiyohiyo inampa Rais mamlaka ya kubatilisha hata baadhi ya yaliyomo kwenye katiba ila "kwa maslahi mapana na ustawi wa jamuhuri" ndivyo katiba inavyosema.

Katiba inampa Rais hata uwezo wa kubatilisha hukumu ya jaji iliyotolewa kisheria na kihalali kwa mtuhukumiwa katiba hiyohiyo imempa Rais hayo mamlaka na afanyapo hivyo anakua amefanya kwa mujibu wa katiba ya nchi pasi na hatia na yupo sawa kisheria.
Paragraph yako ya kwanza inazungumzia kuhusu kunadi sera, vyama vinadadi sera zaidi kipindi chote tangu siku waliyopewa usajili wa kudumu, lengo ni wananchi wawafahamu ili wajiunge na chama hicho, ni kipindi cha kupata wanachama, ni kipindi cha chama kusikiliza na kujua matatizo ya wanachama, ni kipindi cha chama kufungua matawi na ofisi zao, ni kipindi cha chama kushirikiana na wananchi na serikali kusaidiana ili kutatua matatizo ya wananchi.

Kipindi cha kampeni lengo kubwa ni kutafuta kura na wala si vinginevyo, kama wananchi hawajawahi kukuona huko nyuma unategemea watakuelewa kwa kupitia mkutano wa saa moja?.

Madaraka yote aliyonayo rais ameyapata na yameainishwa vizuri sana ndani ya katiba, kila kitu ambacho rais anaweza kukifanya bila kumshauri mtu kwa lengo la kuwa na maslahi ya nchi yametolewa na katiba, lakini wakati yanatolewa, bara nyingi kuna neno linalotumika......bila kuathiri kifungu....cha katiba hii.....rais anaweza kufanya ili na lile.

Kwa kifupi mamlaka yote aliyopewa na katiba, amepewa bila ya kuathiri hata kifungu kimoja cha katiba ya nchi, ndiyo sababu kumeweka mahakama ya katiba, ili kufungua kesi zinazohusiana na ukiukaji wa katiba kuepuka ukanganyiko huo wa kuitafsiri vibaya katiba. Hakuna mtu yeyote aliyepo juu ya katiba, hata kubadili herufi hata moja bila kupitia bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli I Hate U, Tena Urudishe Na Kura Nliyokupa
Siyo haki kuchukia wagonjwa wa akili hata wewe unaweza kupata matatizo ya kiakili [emoji15] [emoji15] tatizo ni position aliyopo huyo mgonjwa mfano mgonjwa wa akili akiwa dereva au rubani au polisi NK inaweza kuwa na madhara
 
Huh ,ati "alichopata ni onyo tu" what the f^$K??? ,Wewe unashangilia kuchukua sheria mkononi na kuchukua maisha ya mtu juu tu ya siasa? Demokrasia na haki za binadamu gani hizo?

Haki za binadamu ndio nini? Ujinga na utoto anaofanya Tundu mimi ndio ningekuwa Rais ningeshamuondoa siku nyingi.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Hilo ulilolisema la kukataza maandamano ndipo anapokosea, kwa sababu maandamano yameruhusiwa kikatiba, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kwenda kinyume na katiba, yeye angeyaona ni tatizo basi alipaswa kupeleka mswada bungeni hata kwa hati ya dharura kufanya marekebisho ya sheria ili kuondoa hicho kipengele, nchi inapaswa kutawaliwa kwa sheria, sio mtu anavyojisikia tu, vipi kuhusu mikutano ya hadhara mbona hataki ifanyike, mtu kama Lipumba, au Mrema, ambao ni viongozi wa kitaifa wa vyama vyao lakini sio wabunge, wakafanyie wapi mikutano ya hadhara ili wakanadi sera zao wananchi wawasikie?.

Magufuli akumbuke kwamba japo yeye katika ligi iliyopita amekua mshindi kwa kuchukua kombe la ubingwa kama Chelsea kule uingereza, hapaswi tena yeye kuzipangia timu zingine namna gani ya kujiandaa kwa msimu wa ligi unaofuata, anayepaswa kupanga utaratibu wa maandalizi ya ligi zijazo ni chama cha mpira cha Uingereza kupitia kamati ya usimamizi wa ligi, ni katiba ya nchi kupitia tume ya uchaguzi, sio Magufuli aseme hili halifau, msifanyi hili linawapotezea muda wa kazi, mbona kipindi cha kampeni wa uchaguzi ukifika hatuachi kwenda kazini tunaendelea na kazi na kampeni zinaendelea?

Sent using Jamii Forums mobile app

Maandamano yote ya kisiasa yaliyokuwa yanafanyika yaliishia kwa vurugu kubwa. Wafanyabiashara walilazimika kufunga biashara mara kwa mara sababu za maandamano. Sasa hivi kuna utulivu mkubwa nchini kulinganisha na enzi za maandamano ya kila siku.

Saa nyingine ni vizuri kutumia akili kuliko kijitabu kidogo kinachoitwa katiba pekee bila busara.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Lakini kwani hii Agha Khan inalipisha pesa ngapi hadi hivi michango kufanywa huko Tanzania kwa matibabu yake? Ama ni CHADEMA hawana pesa kabisa??? Lakuhuzunisha hili!

View attachment 585399
Kwa taarifa yako watu wenye mapenzi mema na bwana Lissu waliomba washiriki kuchangia kuokoa maisha yake.
 
Haki za binadamu ndio nini? Ujinga na utoto anaofanya Tundu mimi ndio ningekuwa Rais ningeshamuondoa siku nyingi.
and you will never be one, even i your dreams
 
Maandamano yote ya kisiasa yaliyokuwa yanafanyika yaliishia kwa vurugu kubwa. Wafanyabiashara walilazimika kufunga biashara mara kwa mara sababu za maandamano. Sasa hivi kuna utulivu mkubwa nchini kulinganisha na enzi za maandamano ya kila siku.

Saa nyingine ni vizuri kutumia akili kuliko kijitabu kidogo kinachoitwa katiba pekee bila busara.
Inaweza kuwa kweli hilo ulilosema, kama kuna hoja nzuri kama hiyo, ninahisi hata wabunge wangeliona hilo na haraka sana wakaipitisha hoja ya kipengele hicho kwenye katiba japo kwa hati ya dharura, kama tulivyofanya juzi juzi tulipozibadilisha sheria zilizokua zinaruhusu nchi kuingia mikataba mibovu ya madini, mbona yeye Magufuli mbele ya hadhara alijinasibu na kumwambia speaker wa bunge kwamba atapeleka bungeni haraka muswada wa kupitia upya sheria ya mikataba na alitegemea bunge lipitishe kwa haraka, huo ndiyo utawala wa sheria, katiba sio biblia wala msahafu, inaweza kupitiwa na kurekebishwa wakati wowote inapoonekana uka umuhimu wa kifanya hivyo, lakini lifamyike ndani ya sheria za nchi.

Nchi yoyote ya watu wastaarabu lazima wazitii na kuziheshimu sheria na tatatibu mlizojiwekea, wakitokea watu wakaanza kujifanyia mambo nje ya taratibu kwa sababu zozote zile haikubaliki. Watu wanataka kuishi wakiwa wanajua nini kitatokea kesho, tabia ya kufanya mambo bila mujibu wa sheria na taratibu za nchi ni hatari sana, juzi juzi hapa Mwakyembe aliamka tu na kusema hakuna mtu atarihusiwa kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa, Mungu akasaidia busara za Magifuli zikamtuma kutengua hilo agizo, sasa nchi haiwezi kuendeshwa hivyo kutegemea busara za mtu mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu kweli namchukia kutokana na mambo yake ya kitoto ila sipo upande wowote. Sijashikiwa akili na mtu yeyote.
Hata Mimi simpendi yule Jamaa, sishangai kwamba kuna ma extremists yamemwagia marisasi.

Bora hajafa lakini, arekebishe approach zake.
 
nikuulize mbona JF juwa wanatoa post flani toka server zake....wanatambua wana deal na dikteta na wanaweza waka kamatwa saa yoyote...muulize mkurugenzi....duh! hii ni nchi ama korokoroni? mmeanza kukaribia KOREA KASKAZINI KWA UCHWARA
Jay, pamoja na hzi changamoto zinazojitokeza, bado tunawazidi kwenye demokrasia! Naam, kenya haijawahi kuwa above tz kwenye democracy hata mwaka mmoja, labda ranking za mwakani ndo tusubiri lakini hata hapo kwenu huu uchaguzi hauwaachi salama!

Achana na hizi sifa zinazotoka hapa jf watu wakiisifu kenya eti ina demokrasia kubwa! Hazihesabiki kokote hizi!

Pamoja na hayo, vitendo kama hivi navilaani sana, kwa waliofanya na walioandaa mazingira ya vitendo kama hivi kutokea!
 
Siongopi, ila nimetumia ushahidi wa tafiti za kimataifa, ingia hapa, www.rsg.org , ulinganishe kati ya Kenya na TZ, na imekua hivyo tangu nchi hizi mbili zilipopata uhuru, ukilinganisha hii ripoti ya mwaka 2017 na ile ya mwaka 2016 utaona Tanzania imeporomoka, hii ni kutokana na Magufuli kuanza kukandamiza wapinzani, lakini bado Tanzania ipo juu ya Kenya tofauti ya nafasi 12

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wengine hivi vitu hawafuatilii, wao huangalia maoni ya mitandao ya tz tu basi! Kama sa hizi, kila mtu anaisifu kenya, lakini mwakani ranking zikitoka zinazoreflect mwaka huu, watu wanaweza wasiamini, au kama kawaida wasifuatilie wakajua takwimu zikoje
 
kweli kabisa ila sio swala la wanasiasa pekee yake....what abt when he arrests musicians like Nay wa Mitgeo...kulikuwa na lyrics flani zilizomtaja rais na hazikumpendeza rais hivyo akaamrisha kukamatwa kwa mwanamziki yule...pili, mkurugenzi wa JF pia alikamatwa kwa kosa lipi? wanahabari wanafaa kukubaliwa kuripoti ukweli wa mambo hata iwe haimpendezi rais? au sio mkuu? angalia Marekani, CNN ABC etc wanaripoti mambo mabaya kumhusu Trump ila hawezi akaamrisha kukamatwa kwa yeyote ama kufungwa kwa kampuni yoyote...imagine na yule ni rais wa dunia ....
Jay nikuongezee kitu hapo kwenye kukamatwa kwa ney. Sidhani kama kuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa JPM aliagiza kukamatwa kwa ney, Kilichotokea ni athali za uoga kwa viongozi wa umma, yaani polisi na basata kwa kudhani kuwa wasipomkamata ney kutokana na mashairi ya wimbo ule, basi JPM anaweza akawawajibishwa kwa kushindwa kumkamata mtu anayeimba mashairi ya namna ile. Kumbe haikuwa kweli! Mda mfupi baada ya kumkamata yeye mwenyewe akaamuru aachiwe mara moja.

Nadhani hizo ndizo, pamoja na mambo mengine changamoto za utawala wake! Kuwa ametia hofu miongoni mwa watumishi wa umma hivyo hawa watumishi wanafanya baadhi ya mambo kwa kuogopa kutumbuliwa badala ya kufuata taratibu!

Ngoja twende naye maana ni rais wetu, ajitahidi tu kuwa flexible kwenye masuala kama! Otherwise nampenda kwenye mapambano dhidi ya wahujumu uchumi!

Suala la melo, hilo, wala sio kosa la magufuli! Ni kosa la sheria ya mitandao ambayo ilisainiwa na kikwete. Ndo maana inawapa uhuru polisi kudukua taarifa za watu mitandaoni! Melo alikataa jf kidukuliwa so akakamatwa! Kwa hili magu hausiki maana hiyo sheria haikitungwa kwenye uongozi wake

Kule marekani Trump au police hawawezi kukamatwa maana sheria yao hairuhusu mambo kama hayo!

Hapa kwetu wabunge wetu walikosea sana kuunda sheria ya namna ile, na rais kikwete akakosea zaidi kuisaini! Najua lengo ilikuwa ni kuwawezesha kushinda uchaguzi, lakini madhara yake kwa jamii ni makubwa sana!

Ndo maana huwa nawalaani sana wanasiasa, huwa wanaangalia maslahi yao tu! Uchu wa kushinda uchaguzi ulisababisha wapitishe sheria ile haraka haraka bila kuona athari zake kwa wapiga kura wao! Damn
 
Siyo haki kuchukia wagonjwa wa akili hata wewe unaweza kupata matatizo ya kiakili [emoji15] [emoji15] tatizo ni position aliyopo huyo mgonjwa mfano mgonjwa wa akili akiwa dereva au rubani au polisi NK inaweza kuwa na madhara
This is most beautiful comment ever
 
Back
Top Bottom