TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

muda wote huu wakuja Geita na Kuvuka maji wewe upo pembeni unamwanagalia? umemabiwa au umemuona akifanya hivyo?

mimi nilikuwepo Geita kwenye hilo kongamano. nilimuona. sio kuambiwa. Nadhani alikuwa na matatizo ya miguu kutokana na umri wake maana alikuwa akitembea kwa taratibu sana.
 
Mzee Jumbe ausia asizikwe kiserikali - Islam Tanzania

====

Huu wosia wake utafanziwa kazi??

"MIMI Aboud Jumbe Mwinyi, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunibariki kuzaliwa ndani ya Uislamu na namuomba aniruzuku kufa na kufufuliwa ndani ya Uislamu".

Hayo ni sehemu ya yaliyomo katika Wasia wa Rais Mstaafu wa wa Zanzibar Alhaj Aboud Jumbe ambaye hivi sasa ametimiza umri wa miaka 80.

Akiwa na akili timamu kabisa Mzee Jumbe ameandika wasia huo wiki hii ambao nakala zake zimesambazwa kwa watu mbalimbali likiwemo gazeti hili.

Wasia huo wenye kuashiria kutahadharisha juu ya yale yanayoweza kuja kufanywa kinyume na ridhaa yake, umekuja siku chache baada ya kifo cha Rais mwingine Mstaafu wa Zanzibar Sheikh Idris Abdul Wakil.

"Ni matumaini yangu kwamba kama Mwenye Enzi Mungu alivyonirehemu kuwa Muislamu, atanijaalia nikifa kukoshwa, kuvishwa sanda, kutiwa katika jeneza, kusaliwa na kuzikwa kwa mujibu wa sunna ya Mtume Muhammad (sa.w.)", umeagiza wasia huo uliosainiwa kwa niaba

yake na Msaidizi wake Bwana Abubakar.

Agizo hilo linahusisha pia jeneza lake kutofunikwa bendera ya Taifa au ya CCM, kuwepo na utabaka katika kubeba jeneza na ufukiaji wa kaburi.

Akiwashuhudisha Mufti wa Zanzibar, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Naibu Kadhi Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Sharrif Juneid, Masheikh wengine na wanawe, Alhaj Jumbe amesisitiza kuwa kufanyiwa si ombi bali ni haki yake kama binadamu, kama Muislamu na kama Mtanzania.

Amesema haki ya uhuru wa kuabudu imeelezwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 19 (1) na (2).

Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu mtu anapokufa ni haramu kwa ndugu au jamaa zake kuomboleza kwa nyimbo, kunyoa vipara, kuvaa vitambaa au nguo nyeusi wala kulia kupita kiasi.

Aidha, imesuniwa kuwafariji (taa'zia) wafiwa kwa muda wa siku mbili tu.

"Atta'azia marrataan" ameagiza Mtume (s.a.w) akiwa maana ya kuwafariji wafiwa ni mara (siku) mbili.

Katika wasia wake Alhaj Jumbe amesema maana ya kuumbwa mauti na uhai sababu na lengo lake ni kuwafanyia wanaadamu mtihani kupimwa miongoni mwao mwenye vitendo vizuri.

"Nikiwa hai, dhamana ya vitendo vyangu inaniangukia mimi mwenyewe, nikifa dhamana ikiwa vitendo vyema au vibaya nitakavyofanyiwa itawaangukia waandalizi, watendaji na wenye kushiriki katika vitendo hivyo", amesisitiza mzee huyo aliyekuwa pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akimshudisha Mwenyezi Mungu katika wasia huo amekataa maziko yake kufanywa kinyume na taratibu za Kiislamu.

"Sitaki bendi, sitaki mizinga, sitaki maombolezo wala lolote lingine lenye hata chembe ya kufuru", ameandika kwa mkazo mzee huyo.

Aidha, amewaapiza kwa kumshuhudia Mwenyezi Mungu wale watakaojaribu kufanya kinyume na anavyoagiza.

"Sitaki hivyo nikiwa hai, nitakapoondoka katika dunia Mwenye Enzi Mungu anatosheka kuwa shahidi wangu, duniani na akhera", mzee Jumbe amemaliza wasia wake alioutanguliza aya ya Qur'an isemayo "Enyi wenye kuamini, mcheni Mwenyezi Mungu vile ipasavyo waja kumcha, wala msife ila Ilhali ni miongoni mwa Waislamu. (3:101)
Hii mbona kama vile hataki serikali katika mazishi yake
 
Kama kweli alifungwa, nani wa kulaumiwa maana aliyemfunga mwenyewe alishakufa long time ago. Nadhani it is better, tusilaum mtu katika hili. Kumbuka yawezekana kama asingefungwa angekuwa kashakufa- wanaofungwa huwa wanakaa miaka mingi sana mfn. Mandela na yeye Jumbe na wengineo.

Wapo WALIOKATISHWA MAISHA Kwa sababu ya muungano, yeye alifungwa-HUONI HIYO NI BAHATI SANA KWAKE????

Poleni sana Wazanzibar, jitokezeni kwa wingi katika mazishi ya mzee Jumbe.
 
Jumbe hakua kizuizini, ameishi kwa Uhuru miaka yote akiwa mji mwema, akienda kokote anakotaka, Kuna wakati alisafiri kwenda arabuni, sijawahi kujua hii dhana ya kizuizini ililetwa na nani na watu wakaishupalia

Tuambie kwanini alikuwa haudhurii kwenye sherehe zote za kitaifa za Zanzibar na Tanzania, wakati karibia Marais waliopita wote wa Muungano na wa Zanzibar walikuwa wakihudhuria?
Humu siyo wote watoto miaka ya tisini.
 
Maalim Faiza,
Hakika ni msiba mkubwa kwangu na Tamim kwani alikuwa mzee wetu
sana na mtu tuliyekuwanae karibu mno.

Walikuwapo katika kundi letu Prof. Hamza Njozi na Dr. Ramadhani
Dau
.

Mzee Jumbe alimpenda sana Tamim kwa ajili ya ile '' hard to imagine
exceptional intelligence'' yake aliyojaaliwa na Allah na Tamim alifanyakazi
kubwa sana ya uhariri wa kitabu cha Mzee Jumbe, ''The Partnership,''
zaidi akimzuia Mzee Jumbe abakishe baadhi ya mambo akimwambia,
Mzee Jumbe imetosha kuwa sisi tushayajua.

https://lh3.googleusercontent.com/-e6IuugxqMt0/Vw01YeJFGZI/AAAAAAAAoYg/6AE2kNfkxk0IcsuXJT8FRYAfjdA0
-Nx6w/w506-h383/2016%2B-%2B1

Hii picha tulipiga mwaka wa 2000.
Aboud AJumbe alimsomesha mzee wangu mika kabla ya Mapinduzi..akimsifia sana ..naweza kumuita Mzee Jumbe ni Uamsho wa kwanza alie jitolea kuwaamsha Wazanzibari juu ya Dude Mungano na atahri zake.
Alikua mhanga wa wazi kabisa katika viongozi...
 
Rais ametuma salamu za rambirambi kwa WANANCHI wa Zanzibar?
Hivi suala la uraia si la muungano au? Kuna raia wa Zanzibar na wa wapi kwingine?
Anyways, pumzika vyema Mzee Jumbe

Hee imekua rambi rambi za zanzibar? Si alikua makamu wa nyerere na makamu wa ccm ? Makubwa
 
Hakuna mtanzania atakaye sema wasifu wa kweli kuhusu taabu alizopitia huyo MZEE, ila ndiyo haya tunayasema kila siku, "UKITAKA KUWA MKWELI, JIANDAE KUTENGWA"". Amepitia mengi na magumu, Mwache akapumzike, Roho na Nafsi yake Mungu akafanyie wepesi.

#RestInPeaceDktAboudJumbe
 
Bila huyu, leo kusingekuwepo na CCM, kwani alikubali chama cha ASP kiungane na TANU na kuzaliwa CCM.

Alipohoji kuhusu Muungano, akapokonywa madaraka yote na kuwekwa Kizuizini Kigamboni toka mwaka 1984.

Pumzika kwa amani Jumbe, daima wewe ni shujaa wetu na jina lako litaishi milele.
Hakuna mtanzania atakaye sema wasifu wa kweli kuhusu taabu alizopitia huyo MZEE, ila ndiyo haya tunayasema kila siku, "UKITAKA KUWA MKWELI, JIANDAE KUTENGWA"". Amepitia mengi na magumu, Mwache akapumzike, Roho na Nafsi yake Mungu akafanyie wepesi.

#RestInPeaceDktAboudJumbe
 
rip ligend,ulipigania maslahi mapana ya zanzibar japo masnitch walikuwa wengi
 
Back
Top Bottom