TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

kauli hii imo kwenyetuhuma dhidi ya Jumbe iliosemwa na Mwenyekiti
Kauli gani na Mwenyekiti gani aliyeyasema hayo, Nyerere?

Nyerere alisema Jumbe alikuwa anaelekea kumshtaki International Court of Justice na alikuwa ameandaliwa makaratasi na Dourado na attorney General M-Ghana?

Mwenyekiti aliyasemea hayo wapi na lini?
 
Hujui Hoja ya Sheikh Jumbe ndio sababu umejivuruga.

Jumbe hakuwa akipinga Muungano, alikuwa akiukubali sana na ndio sababu katika kuonesha Tanzania ni moja

1) Alikubali kuunganisha Vyama vya siasa ASP na TANU na laiti angekuwa Muoga basi asingekubali.
2) Alifanya ziara nyingi za kuhamasisha Maendeleo hata huku bara ndio sababu hata wakati Nyerere anaitisha kikao cha dharura cha NEC Mzee Jumbe alikuwa anatokea Musoma kwny ziara za kiserikal kuchochea Maendeleo.
3) Kujenga Nyumba Bara ni ishara yake kuonesha hakuwa na dhamira ya kuvunja Muungano bali kuleta Muungano wenye maridhiano na ndio sababu alikuwa akiandaa andiko la Muundo wa Serikal tatu liletwe kwny NEC na lijadiliwe ( aliamini katika kujenga hoja) lakini akafukuzwa kwa kuwa na hoja hiyo kama vile ni haramu kuwaza tofauti na kuleta hoja.
4) kuna Wengine makaja na hoja alikuwa anapambana na kina Seif tena mkawaita wapenda Mabadiliko sasa jiulize kama Jumbe alikuwa ndie
Aliesimamia kuunganisha TANU na ASP Zanzibar
Alieanzisha katiba ya Zanzibar na kuachana na kutumia Amri za Rais kutawala ( decree)
alienzisha Baraza la Wawakilishi na kuachana kutawala kwa kutumia Baraza la Mapinduzi
Alieweka bill of Human rights Zanzibar
Alieamua kuacha desturi ya kuwabagua Wapemba na kuwajumuisha Serikalini

Pamoja na mabadiliko yote aliyofanya bado tunamwita eti hakuwa Mpenda Mabadiliko na kina Seif ndio wapenda Mabadiliko.

Mkuu Pohamba ujaaliwe sanaaaaa tu maana unatujuza Na masuala ambayo wengi wetu tulikuwa hatuyajui Au uonga wakutotaka kuyajua.Kwa kweli nilikuwa sijui kama,Marehemu Abdul Jumbe Mwinyi Mwenye Ez Mungu aiweke roho yake peponi,Alikuwa Ktk kifungo cha ndani Kigamboni.Huu uzi ndio umenijuza.
 
Natanzania na UDINI! Habari ya kifo imegeuzwa kongamano la dini.

Yaani hawa ndugu zetu wakati mwingine wanaharibu mno minakasha kwa kubishana kwenye mambo ya dini. Mnakasha huu ulikuwa ni kutupatia maarifa na taarifa nyingi tena zenye mafunzo, lakini loh! Anno Domino, dini gani ya ukweli, kadha wa kadha mpaka mnakasha unapoteza mwelekeo wake! Tuachieni basi tujifunze wakuu!!

Kaka ...
 
Kaka wengi wetu hatupendi Haya mabishano ya Dini.Haya mabishano yanatudhulumu Elimu yetu kujua habari za Marehemu Abdul Jumbe Mwenye Ez Mungu amrehemu.
Mods tafadhali yazuie mabishano ya dini ambayo hayaleti tija katika Hii mada.
Cc.invisible
Cc.mods
 
TURUDINI KWENYE MADA.....SHEIN KATOA SIKU 7 ZA MAOMBOLEZO NDIYO YALE TULIYOKUWA TUNASEMA....

OVA
 
M/zimungu hutoa nafasi za toba kwa binaadam wake ili kumrudia allah na kuomba msamaha kwa yale tulio mkosea muumba wetu.
Hakika nakiri mbele ya allah huyu mzee ametubu mbele ya allah kwa dhati kabisa.
Muda wote tokea ajiuzulu nyadhifa zote za serikali na chama hakuwa na ziada zaidi ya kufanya ibada na kuomba toba tu.
Yarabbi mjaalie mzee huyu makaazi mema peponi umsameha makosa yake kama alivyo tangulia yeye kukuoba msamaha.
Yarabbi mkubalie maobi yake na toba zake umuondolee ghadhabu zako juu yake na umjaalie maisha ya raha ktk kaburi na siku yahesabu..
AMEEN
 
I rest my case man. Happy Tuesday!
Mwinyi amejengewa nyumba wapi ?????

You rest your case, case gani uliyoi present hapa ya ku rest? Unakimbia?

Ati marais wote wastaafu hujengewa nyumba.

Mwinyi kajengewa nyumba wapi ???

Na Mkapa amejengewa nyumba wapi???

Kukarabati kathiri la Jumbe is naked misuse and abuse of tax shillings, imetoka fungu gani la bajeti hiyo hela?

Ndio maana makodi mapya hayaishi nchi hii! There is massive waste and abuse of tax money.

Sio kweli

Jumbe alikuwa anakuja Zanzibar kila panapotokea haja.
Tatizo unasahau kamba zako mwenyewe!.

Wewe mwenyewe umesema Jumbe alifungwa kifungo cha maisha cha kutokanyaga Zanzibar. Sasa umeenda hadhithiwa msibani kwamba Jumbe keshawahi kuja Zanzibar? Si ungesema mara ya kwanza ulichemka!

Baraghash, post: 17226276
Rais wetu tuliomchaua kwa kura 84% anauzuliwa na babe mmoja na kufungwa kifungo cha maisha cha asikanyage Zanzibar.
... dhulma, udhalimu na ukatili waliomfanyia Jumbe wakati uhai wake

Rais wetu tuliomchaua kwa kura 84% anauzuliwa na babe mmoja na kufungwa kifungo cha maisha cha asikanyage Zanzibar.

... dhulma, udhalimu na ukatili waliomfanyia Jumbe wakati uhai wake
 
Mwinyi amejengewa nyumba wapi ?????

You rest your case, case gani uliyoi present hapa ya ku rest? Unakimbia?

Ati marais wote wastaafu hujengewa nyumba.

Mwinyi kajengewa nyumba wapi ???

Na Mkapa amejengewa nyumba wapi???

Kukarabati kathiri la Jumbe is naked misuse and abuse of tax shillings, imetoka fungu gani la bajeti hiyo hela?

Ndio maana makodi mapya hayaishi nchi hii! There is massive waste and abuse of tax money.

Hahahaa! Huo wimbo wa "Tax payer's money sisi wote tunaufahamu - tatizo lako jazba nyingi. Mwinyi na Mkapa wamejengewa nyumba Mikocheni, Kikwete Ada Estate. Need I say more?
 
Tatizo unasahau kamba zako mwenyewe!.

Wewe mwenyewe umesema Jumbe alifungwa kifungo cha maisha cha kutokanyaga Zanzibar. Sasa umeenda hadhithiwa msibani kwamba Jumbe keshawahi kuja Zanzibar? Si ungesema mara ya kwanza ulichemka!

Baraghash, post: 17226276
Rais wetu tuliomchaua kwa kura 84% anauzuliwa na babe mmoja na kufungwa kifungo cha maisha cha asikanyage Zanzibar.
... dhulma, udhalimu na ukatili waliomfanyia Jumbe wakati uhai wake

Du! Sijui unaishi dunia ipi mkuu? Jumbe alikuwa anasafiri anakwenda kokote anakotaka as early as 2000. Wenye busara waliona hichi kifungo kilikuwa upuuzi waka tupilia mbali.
 
Hahahaa! Huo wimbo wa "Tax payer's money sisi wote tunaufahamu - tatizo lako jazba nyingi. Mwinyi na Mkapa wamejengewa nyumba Mikocheni, Kikwete Ada Estate. Need I say more?

Hii ya JK unayoizungumzia ni ile ya Migombani ?
Kama ndio hiyo nyumba si alikuwa nayo kabla hajawa Raisi ?
 
Hahahaa! Huo wimbo wa "Tax payer's money sisi wote tunaufahamu - tatizo lako jazba nyingi. Mwinyi na Mkapa wamejengewa nyumba Mikocheni, Kikwete Ada Estate. Need I say more?
Duu, Kikwete kashajengewa nyumba tayari toka awe mstaafu, we mkali!

Ada Estate hakuna nyumba ya Kikwete mjomba acha kamba, nyumba ya serikali ya Kikwete alipewa toka akiwa Waziri, iko Mikocheni.

Mwinyi nyumba yake ya Mikocheni kajenga mwenyewe japo anayo ya serikali ambayo aliishi toka yuko Rais, kama ambavyo wakubwa wa serikali wote miaka ile walipata nyumba, iko Oysterbay mtaa wa Laibon wana share ukuta na kambi ya kijeshi ya Marekani.

Mkapa hajajengewa nyumba na serikali either, japo ana jumba la serikali Masaki ambalo alilipata kama ambavyo wakubwa wote miaka ile walipewa.

Aboud Jumbe kujengewa upya nyumba yake binafsi Kigamboni ni ubadhilifu wa hela za umma.
 
Wewe mwenyewe umesema Jumbe alifungwa kifungo cha maisha cha kutokanyaga Zanzibar. Sasa umeenda hadhithiwa msibani kwamba Jumbe keshawahi kuja Zanzibar? Si ungesema mara ya kwanza ulichemka
Usijichanganye na naamini lugha ya kiswahili unielewa. Kuja Zanzibar kuzika watoto wake mwenyewe au aliporudi matibabu ikambidi kurudi na kupata uangalizi wa mwanae haimaanishi kuwa hayuko kwenye kifungo cha maisha nyumbani.

Kumbuka pia alipokwenda India lkwa matibabu alifuatanana mwanawe mkubwa Dr. Jumbe na ikatokea Dr Jumbe aliigua ghafla na kufariki hukohuko India. Rais Jumbe alirudi Zanzibar akiwa bado mgonjwa lakini kuja kumzika mwanawe.

Ukifungwa tofauti ukiwa huru. Ukiwa huru unapotaka kwenda pahali ndani ya nchi huhitaji kibali cha mtu!
 
Du! Sijui unaishi dunia ipi mkuu? Jumbe alikuwa anasafiri anakwenda kokote anakotaka as early as 2000. Wenye busara waliona hichi kifungo kilikuwa upuuzi waka tupilia mbali.
Sio kweli mkuu. Ilikuwa lazima alikuwa apate kibali kwa wale waliomdhibiti. Rais Jumbe alikuwa anapenda sana kusafiri nje ya nchi lakini tokea alipokuwa kifungoni kasafiri kwenda India tu kwa matibabu. Hivi alikuwa haalikwi kwenye mikutano nje ya nchi au hata za kikanda kama wapatavyo akina Mkapa na Kikwete.

Usijaribu kuhalalaisha udhalimu kwa kuupaka vipodozi na marashi! Mbona hajapata kibali cha alau kuwaaga wazanzibari au kumsikia mwenyewe akitamka kuwa amejiuzulu Rais wa Zanzibar mpaka kifo kilipomfika?
 
Sijui unamaana gani unapotumia neno udhalimu? Serikali zote duniani ni serikali za kidhalimu hata hizo serikali zenu za Saudia na ile mnayoipenda sana ya Oman wote wadhalimu.

Mzee Jumbe as early as 2000 hakuwa kifungoni. Alikuwa ana miaka 80, mzee wa miaka 80 angeenda wapi? Angeenda surfing Maui, Hawaii? Aliamua achana na siasa/anasa za dunia na akawa mcha Mungu miaka mingi. Safari zake zilihusu masuala ya dini na alikuwa anahudhuria shughuli za kidini bara na visiwani. Humu JF kuna watu wamekuwa naye kwenye shughuli za kidini mara nyingi tu.

Speaking of wadhalimu kama unavyodai, hao wadhalimu ndiyo walikuwa wakimuhudumia. Mwanae wa kuzaa amewashukuru hao wadhalimu wa bara na visiwani kwa kumhudumia. Rais Karume amesema Jumbe alikuwa baba yake baada ya baba yake kufariki, Karume angeacha baba yake afe kwa taabu wakati yeye ni rais wa Zanzibar? Kama ni wadhalimu si angekataa huduma toka kwa wadhalimu akaomba toka Oman? Acheni ushabiki nyie...
 
Duu, Kikwete kashajengewa nyumba tayari toka awe mstaafu, we mkali!

Ada Estate hakuna nyumba ya Kikwete mjomba acha kamba, nyumba ya serikali ya Kikwete alipewa toka akiwa Waziri, iko Mikocheni.

Mwinyi nyumba yake ya Mikocheni kajenga mwenyewe japo anayo ya serikali ambayo aliishi toka yuko Rais, kama ambavyo wakubwa wa serikali wote miaka ile walipata nyumba, iko Oysterbay mtaa wa Laibon wana share ukuta na kambi ya kijeshi ya Marekani.

Mkapa hajajengewa nyumba na serikali either, japo ana jumba la serikali Masaki ambalo alilipata kama ambavyo wakubwa wote miaka ile walipewa.

Aboud Jumbe kujengewa upya nyumba yake binafsi Kigamboni ni ubadhilifu wa hela za umma.

You are too naive...
 
Naona sasa posho za maasikali waliokua wakimlinda nyumbani kwake pale kigamboni asitoke zimefikia ukingoni.

Hatuwezi kushangaa hao walinzi nao wakalazwa.Miaka 32 wako pamoja Na mlindwa unafikiri hajawaambia yaliyo tokea.
 
Mungu amlaze mahali pem peponi...sitasahau siku ile dodoma na tukiwa njian kurudi dsm..
Nini kilitokea mkuu!!?

Ni nani alimsaliti Mzee Aboud Jumbe!!?hope unijibu hili coz halina effect yeyote Kwa siasa za Sasa hata tukijua yaliyojiri!!
 
Back
Top Bottom