TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

bagamoyo,
Duh hawa wakenya wameshajua ugonjwa uliomuua waziri? Nani amewatangazia kwamba ni corona?

Au wanajipendekeza kwa watu flani flani! Sina uhakika kama wako sahihi kidiplomasia.
 
Rest in Peace Dr Mahiga, umeacha alama katika nchi aliyokupa Mungu wetu.
 
Alikuwa MTU hodari, kiongozi wa kidunia asiye na makuu aliyelitumikia taifa kwa weledi na heshma kubwa ndani na nje ya nchi...aliheshimika kimataifa!!

nakumbuka alijiwa juu namukuulu mapreshaa kisa eti mkewe kupingana na askari trafiki (hawa tunaowajua tunaogombana nao kilaleo) barabarani.
RIP kiongozi wetu mpendwa...
 
Nimepiga nae kazi kitengo alikuwepo mtu poa sana[emoji23]
 
Hivi najiuliza mtu miaka 75 ni waziri kweli hivi hakuna vijana Raisi wakusaidie. Jamani mimi nikifika hata 62 usinipe cheo kwanza natamani nipumzike Nile pension yangu jamani.Huyu balozi kazaliwa 1945 kweli kweli bado ni waziri duuuuuuu
 
Kweli tenda mema utalipwa mema, Leo taarifa zote za wachangiaji iwe chama tawala au vyama mbadala vimempongeza mwanadiplomasia nguli Augustine Mahiga.

Balozi za ulaya, Somalia na taarifa za habari za BBC zote zinampongeza Marehamu kama alikuwa msikivu na mwenye busara

Mtangazaji wa BBC Mariam Omar amesimulia kuwa wakati wanaanzisha kipindi cha Focus on Africa walikuwa wanamuomba Dr Mahiga awasaidie kwenye pilot stage na alifanya hivyo hata iwe usiku wa manane au yupo safarini

Hapa JF ni mara chache watu kusifia mtu, kwa marehamu Mahiga comment zote ni nzuri na positive.

Je, kwanini wanasiasa Wengine wa nashindwa?
Je, nini kimefanya watu wengi wamsifie sana na sio kumkashifu kwenye mitandao ya kijamii na mitaani?

Hakuna mtu ambaye ameandika tofauti kwenye uzi huu: TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia - JamiiForums
 
Back
Top Bottom