TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

Daaahh Pigo kubwa sana kwa Baraza LA Mawaziri,
Yaaani ni Waziri Pekee niliyekuwa na matumaini naye ktk kumshauri Magufuli.
Hakuwa MTU wakutetea tonge kama Kabudi,Alikuwa Mzee na kweli Alikuwa na Busara na Hekima.
Ni moja ya watu (viongozi)wachache ambao Tanzania ilipata bahati kuwa nao ktk Dunia hii.
Alale mahali panapo mstahili Mzee Mahiga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha majungu dogo
Hii corona naona imeingia Ikulu live mchana kweupe.
Ifike wakati viongozi wa Tanzania wajifunze kujiuzuru pale ushauri wao unapopuuzwa.

Waziri Mkuu na Waziri wa afya ilibidi wawe wamejiuzulu toka siku nyingi.

Sidhani kama msimamo wa Rais ndio msimamo wao, hawana namna sababu ya kulinda vibarua vyao.

Uhai ndio kila kitu hivyo vyeo mnakufa mnaviacha, kama kiongozi mkubwa hataki kufuata ushauri wa wataalamu ni kumwachia serikali aongoze peke yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ngoma ikifika mwezi wa sita ndiyo kipindi cha serikali kutoa kafara, watu tutakufa zaidi ya Italy, ikifika mwezi wa sita UN itaingilia kati kuisaidia Tanzania...
 
R.I.P Mahiga

Ama kwa Hakika Taifa limepoteza mtu makini na mwerevu.


Sasa ni wakati kwa Serikali itambue kwamba viongozi wa Juu ambao tunaamini wao ndio wapo katika nafasi nzuri ya kupata matibabu na kinga wanapopoteza maisha wakati huu huku Serikali kutoonesha nia ya dhati kupambana na hili Janga basi huu ni Ujumbe tosha kwa Dunia kwamba Mamlaka zimeshindwa kulinda watu wake na hivyo Nchi haipo salama sasa hivi na siku zijazo hata majanga mengine yatakapotokea.

Hakuna mamlaka itakayokulinda na corona. Nawa mikono. Tumia barakoa. Kaa nyumbani. Weka distance ya mita moja na zaidi. Hakikisha ukikohoa unaziba na tissue au koholea kwenye kiwiko. Hakuna la Ziada mkuu. Serikali kazi yake Ni kuimarisha huduma za Hospital.

Mkuu Punguza umbeya. Wajerumani wanamsemo „ Die Kirchen in Nachbars Garten schmecken immer ein bisschen süßer.“ Penda cha kwako na play your Part. Mna ugonjwa wa kutafuta sana matatizo kuliko furaha.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
R.I.P Mahiga

Ama kwa Hakika Taifa limepoteza mtu makini na mwerevu.


Sasa ni wakati kwa Serikali itambue kwamba viongozi wa Juu ambao tunaamini wao ndio wapo katika nafasi nzuri ya kupata matibabu na kinga wanapopoteza maisha wakati huu huku Serikali kutoonesha nia ya dhati kupambana na hili Janga basi huu ni Ujumbe tosha kwa Dunia kwamba Mamlaka zimeshindwa kulinda watu wake na hivyo Nchi haipo salama sasa hivi na siku zijazo hata majanga mengine yatakapotokea.
Mzee; unaleta siasa hata kwenye misiba kabla hata hujajua nini kimemkuta marehemu? Alikuwa anaingia miaka 75, zaidi ya umri wa watu wengine wengi waliotangulia ikiwa ni pamoja na Mwalimu Nyerere, Steve Jobs, Steven Kanumba na wengineo weng.Omboleza bila kuweka siasa, siyo kila baya linapotokea nchini ni kwa sababu ya serikali; mwishowe utalalamika kuwa mvua kunyesha au kutonyesha ni kosa la serikali pia.
 
Pole sana familia ya Mahigha. Binafsi nafahamiana wa watoto wake. Pumzika kwa amani mzee wetu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Tunapompigia kelele Magufuli achukue hatua za kuwalinda watanzania huwa mnatubeza sana na kutuita majina ya ajabu ajabu.
Ona sasa tunaomboleza!!!
 
Hii system chafu ya ccm mpaka iondoke ndipo tutajua ukweli wote kuhusu Tanzania halisi vinginevyo huu ukoo wa panya utaendelea kutufanyia mazingaombwe....
 
Yaani RIP waziri.Poleni familia.Nawaza kuna mahali nilituma ushauri kuwa raisi angezuia mukusanyiko isiyo ya lazima kama kanisani na misikitini ile pasaka ndio outbreak imeanza.Sasa let us swallow our pride now
 
Mungu wangu huyu si alikuwa mzima juzi tu hapa..

Naanza kupata wasiwasi na wale wote walioshiriki kikao cha kupokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) pale chamwino dodoma hasa mawaziri na viongozi wengine wakubwa wa nchi...

Kwa maslahi ya afya zao ni vyema wakaanza kuchukua hatua mapema...

COVID-19 is real guys. Apumzike kwa Amani bwana Balozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si Ulisikia CAG naye hali tete?
 
SIO MASIHARA HII NDIO INAITWA.....
WHO NEXT??
UKIKOHOA KIDOGO TU NDIO UNAOGOPA ZAIDI...
NAJIKUTA NAANZA KUWAZA HUENDA KUNA
IMPLANTED CORONA BUNGENI DODOMA WASIPO CHUKUA TAHADHALI NAOGOPA TUSIJE POTEZA ICON NYINGI ZA TAIFA KWA MKUPUO.
WALIO KARIBU NA VIONGOZI WAWAFIKISHIE HUU UJUMBE
Huku Mtaani ambapo vifo ni vingi kuna nini au wao wanasitahili kufa!
 
Back
Top Bottom