TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

Maskini, Ila Umri wa Biblia umetimia, kafa siku muhimu , kila tukipumzika tutakuwa tunamkumbuka kama Mfanyakazi aliyetukuka katika uongozi ngazi ya Kimataifa na Kitaifa
 
Lockdown jamaniii


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Watanzania ni wajuaji sana! Popote Uendapo, this is the reason why very few only the humble ones have succeeded! Punguzeni Ujuaji! Elimu zenyewe mshikemshike, Maneno tu! Duniani kote kipindi hiki wanakitumia kutiana Moyo! Lakini ninyi vinywa vyenu vimejaa Sumu tu!
 
JokaKuu, Wengine wenye ufahamu na masuala haya hasa magonjwa ya kuambikizwa tulisema wazi hakuna bahati nasibu katika maisha ya watu, na kwamba, wakubwa wa Dunia wameshindwa sembuse sisi wapitisha bakuli.

Hili lilikuwa wazi kabisa kwamba kulikuwa na mzaha hakuna seriousness na hakuna mwenye uthubutu wa kusema ''hili si sawa au tunakokwenda si kwema'' Watu wanaogopa vyeo vyao zaidi kuliko uhai, Corona haijui nyadhifa.

Tulionya ''kauli za tokeni muende kuchapa kazi'' ni za kipuuzi sana. Kuna watu hawajui wala hawataki kusikia habari za dunia. Italy wanazika kwa kutumia jeshi halafu watu wanasema nendeni mkachape kazi!

Tuliuliza hivi unafunga vipi vyuo na shule halafu unaacha makanisa na misikiti? unaacha Bunge?
Hii ni infectious control kutoka dunia gani, yaani tunaonekana kama hatuna watalaam

Tukaambiwa tunategemewa na nchi 8, sasa nchi hizo zinatufungia mipaka!

Tuakakataa kuungana na wenzetu wa EAC ambao sasa wanafanya vizuri sana ingawa walipata maambukizi mapema. Sisi tukatafuta solution za maombi na nyungu! inakula kwetu kikamilifu.

Viongozi wetu wamezembea sana katika hili, hatukupaswa kuwa hapa tulipo.

Mwingine aliyepigia upatu bahati nasibu ya Mzee Mwanakijiji ni Pascal Mayalla
Bahati nasibu imefeli kwa gharama za maisha ya watu, na itaendelea hadi May mwishoni au June.
 
Viongozi wetu wamezembea sana katika hili, hatukupaswa kuwa hapa tulipo.
Hapana, huku ni zaidi ya "kuzembea".

Bila shaka ulitaka kuwa 'modest' tu katika kulitumia hilo neno.

Kwenye nchi ambazo wananchi wake wanajitambua, viongozi hawa wasingestahili kuendelea kuwepo kwenye uongozi.

Hapa kwetu ni kinyume chake kabisa. Raia akisema chochote juu ya huu ugonjwa anaandamwa na polisi.

Haya ndiyo maajabu ya nchi yetu hii sasa.

Kapumzike kwa Amani Mh. Mahiga.
Inakuwa vigumu sasa kwetu wengine kukutupia lawama kwa kunyamazia maovu katika serikali uliyoshiriki kuwemo.
 
May 1, 2020
Nairobi, Kenya

Minister of Constitutional and Legal Affairs of Tanzania Augustine Mahiga dies of COVID-19



Source : KTN NEWS KENYA
 
Back
Top Bottom