miss strong
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 7,012
- 3,700
R.I.P. Msanii.
Mwenye picha yake tafadhali.!
George Tyson
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mongozaji wa filamu maarufu nchini George Otieno Tyson (Pichani) amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Morogoro.Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu.Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.
Wanabodi, Baada ya msiba wa producer Adam Kuambiana na baadae msaani Recho, leo gazeti la MWANANCHI 31/05/14 07:59 limetuma sms kuwa
MWANDAAJI WA FILAMU AFARIKI: Mkurugenzi wa filamu George Tyson amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Gairo akitokea Dodoma usiku wa kuamkia leo.
My Take.
Kwa maoni yangu, George Tyson ndiye the best local movies producer tuliyenaye so far.
Alikuwa ni Mume wa kwanza wa Msanii wa Bongo Movies Monalisa.
Poleni sana Bongo Movies.
Poleni wafiwa.
RIP George Tyson.
Pasco.
Muheshimiwa ndo kwanza unaamka nini? tayari kuna uzi wa habari hiyo humu tangu saa 9 usiku.Msanii na gwiji wa kutengeneza filamu,mume wa zamani wa Monalisa na muanzilishi wa kipindi cha Mboni talk show,George Otieno Tyson amefariki kwa ajali ya gari Morogoro leo. Source:ITV habari mpasuko.