TANZIA: Ivan Ssemwanga (ex wa Zari) amefariki dunia usiku huu

TANZIA: Ivan Ssemwanga (ex wa Zari) amefariki dunia usiku huu

Alale mahala alipojichagulia akiwa hai tumkumbuke sana Mungu siku zetu za uhai kabla mlango wa mbingu haujafungwa na ukomo wa pumzi tuishi kwa kupenda haki na kuwa na amani na watu wote huku tukisameheana na kuukomboa wakati kwa sala na maombi maana mshitaki wetu ibilisi kutwa anazungukia kututafuta atumeze, pole zari na watoto wako pole family ya ivan tuliobaki tujifunze kutoka kwa mwenzetu aliye tangulia kwamba Hata mtoto akiwa tumboni ni lazima azaliwe tu iwe kwakisu au natural lazima azaliwe na kifo ndio hivo hivo hata uwe tajiri au maskini mtoto au mkubwa kufa lazima ufe ikifika imefika tujenge mwisho mwema kila siku tuishi tukiona kama ni siku yetu ya mwisho tusali na kumtegemea Mungu kwa kila jambo
Mungu tujalie mwisho mwema, Amen.

Ameni
well said.
thank you.
 
R.I.P Ivan da so sad wale wtt tu nawahurumia ulikuwa baba Bora kwa wanao umeacha pengo kubwa kwao
 
Mda mrefu tokea amaechana na zari ukimfatilia ivan sana alikua hana sura ya furaha hata kwenye picha ukiangalia kwa makini unagundua huyu the don ana tatizo daahh rip ivan.nilikua na mpango wa kukupiga kibomu sasa ndoto zangu namm zinakufa hivihivi
 
Hakika kila aliyezaliwa na mwanamke siku zake zinahesabika na ni chache hapa Duniani...Apumzike kwa Amani kaka Ivan
 
Maradhi ya moyo ni hatari sana na asilimia kubwa huchangiwa na msongo wa mawazo unapozidi au kuweka kitu moyoni kitu ambacho kwako kilionekana nij jeraha so kila ukikikumbuka moyo hupata jeraha. Ivan alishindwa kujicontrol pindi alipotengana na Zali na aliona maisha kwake hayana thamani naamini wengi tuko hvyo so kuna wakati tunaowapenda kwa dhati ndio wanasababisha yetu mauti naipa poule familia yote ya Ivan Ssemwanga katika kipindi hiki kigumu cha msiba na Tumuombe Mungu ampunguzie adhabu ya kaburi kwani wote ni waja wake na kwake tutarejea. Bwana anetoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Ameeen. R.I.P Ivan Ssemwanga.
 
VITU VITAKAVYOFANYA IVAN SEMWENGA EX HUSBAND WA ZARI AKUMBUKWE NI HIVI​

 
Rest In Peacei
Jamaa na mihela yote ile hatuko nae duniani daha!! Rest in Peace Money Maker Ivan
Ila hiyo mihela dah...!
 
Utashangaa Mabilione wamekaa kimya na wapo ila kujionyesha nakujurusha kumefupisha maisha ya kijana.
Cc Diamnd
 
Oh! RIP Ivan...

I guess Lawrence atakuwa kwenye msiba mkubwa zaidi kuliko Zari... ndo ile watoto wa mjini wanasema "watoto wa marehemu wamenyamaza kulia, mpambe ndo kwanza analiamsha!!!"
Tuko na majonz ujue usianze vichekesho RIP Ivan. ....
 
Utashangaa Mabilione wamekaa kimya na wapo ila kujionyesha nakujurusha kumefupisha maisha ya kijana.
Cc Diamnd
Japo marehemu si vizuri kumsema sidhani kama hiyo ilikuwa CSR...ni show offs...tabia za kitoto ... ndio maana Zari alimtema...

Kuna clip moja niliwai ona anamwaga ma pound UK...Zari yuko pembeni anatabasamu...(ila ukisoma tabasamu lake halikuwa real)
 
Cha kujiuliza tymejifunza nin kupitia huu msiba wa ivan maan kifo ni mawaidha
 
Cha kujiuliza tymejifunza nin kupitia huu msiba wa ivan maan kifo ni mawaidha
Duniani tunapita hata uwe na hela kiasi gani au uwe maskini kiasi gani ni vizuri kumcha Mungu na kufanya yale yalio mema.
 
Rest in perfect peace Ivan

Umenitoa chozi na sijuani nawe. Video clip ni post ya mwisho akiwa Uganda alirusha tarehe 11 May 2017. Uliwapenda sana sana watoto wenu wa kiume 3 na kuwajali na kuwaheshimu na Mama yao Zari..mfano mzuri kwa wababa.

Zari aliachana na Ivan na baadae kuja kuwa na Diamond Platnumz ambaye wana watoto wawili pamoja.

Moja ya biashara kubwa ni umiliki wa vyuo mbali mbali nchini South Africa, alizianzisha na Zari. Na biashara zingine, ni Tycoon Ivan.

Poleni sana kwa msiba.

View attachment 514047

kutoka online.

Picha wakati wa uhai wake bonyeza mshale kwenda kuziona kwenye post ingine humu...


=====

Mzazi mwenzake na Zari The Bosslady, Ivan Ssemwanga amefariki dunia katika hospitali nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo.

Ivan ambaye alifanikiwa kupata watoto watatu na Zari, baby mama wa Diamond Platnumz, alikimbizwa hospitalini mapema wiki iliyopita baada ya kupoteza fahamu. Kupitia mtandao wa Instagram, Zari amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kuweka picha ya bosi huyo na kuandika ujumbe wa kusikitisha.
satan-2.jpg
 
Back
Top Bottom