engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,149
- 1,441
Wana Bodi,
Nasikitika sana kuwapa taarifa za msiba wa Mke wake na Kaka Kiiza, kilichotokea sasa hivi. Nimepata ujumbe wake kwa njia ya sms juu ya taarifa hizi za kusikitisha.
Naungana na ndugu na jamaa wa ndugu yetu katika maombolezo ya msiba huu mkubwa.
Kaka Kiiza, Asured kwamba mawazo yetu na sala zetu yapo na nawe katika kipindi hiki chote cha msiba! Jipe Moyo Mkuu kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa hata kidogo...
Binafsi sikupata details zaidi!! nitakapopata nitaziweeka hapa
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Libarikiwe!
Kwa wale watakao weza kuhudhuria msiba safadhali tukamtie mwenzetu Moyo!
Kiresua
More info!!
Mwasiliano na Kaka Kiiza ni 0752 30 78 78
Mama Kiiza amefikwa na mauti kwa sababu za ujauzito!
Asante sana Mtambuzi kwa hii taarifa, asante pia kwa kumtembelea na kumtia moyo, kwa kweli anahitaji sana watu wa kumfariji kwa sasa.Jana nilimtembelea KakaKiiza na kuzungumza naye kwa kirefu sana, ukweli ni kwamba mwenzetu amepata pigo kubwa sana kwa kuondokewa na mkewe kipenzi. kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatatu jioni katika makaburi ya Kindondoni.
Ni vyema kwa wale wana JF walioko jijini Dar kuungana na mwenzetu kumsindikiza mkewe katika safari yake ya mwisho.
Mwenye enzi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi .................amina
Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.