Tanzia: KakaKiiza (JF Member) afiwa na Mkewe!

Tanzia: KakaKiiza (JF Member) afiwa na Mkewe!

mungu akupe mkuu kiiza

sijui ni lini haya matatizo ya wajawazito kufa yataisha lini hapa bongo,nchi za wenzetu ni ndoto sana kusikia ujauzito umetoa uhai wa mtu.hata kama ipo ni nadra ukilinganisha na hapa kwetu
R.I.P SHEMEJI YETU
 
Pole sana Kaka Kiiza kwa msiba mkubwa uliokupata. Tunakuombea Mungu akupe nguvu katika kukabiliana na msiba huu.

Sisi ni wa Mwenyezimungu na kwake tutatarajea
 
R.I.P Shemeji,Mwenyezi Mungu akutie nguvu mpiganaji wetu Kaka Kiiza.
 
Pole,and may the Almight give relatives and friends the strength and courage through this hard time.
 
Pole sana kaka kiiza...Mungu akutie moyo upite kwenye kipindi hiki salama...
 
Wana Bodi,

Nasikitika sana kuwapa taarifa za msiba wa Mke wake na Kaka Kiiza, kilichotokea sasa hivi. Nimepata ujumbe wake kwa njia ya sms juu ya taarifa hizi za kusikitisha.

Naungana na ndugu na jamaa wa ndugu yetu katika maombolezo ya msiba huu mkubwa.

Kaka Kiiza, Asured kwamba mawazo yetu na sala zetu yapo na nawe katika kipindi hiki chote cha msiba! Jipe Moyo Mkuu kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa hata kidogo...

Binafsi sikupata details zaidi!! nitakapopata nitaziweeka hapa

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Libarikiwe!

Kwa wale watakao weza kuhudhuria msiba safadhali tukamtie mwenzetu Moyo!

Kiresua

More info!!

Mwasiliano na Kaka Kiiza ni 0752 30 78 78

Mama Kiiza amefikwa na mauti kwa sababu za ujauzito!

Pole sana KakaKiiza! Mwenyezi Mungu akupe uvumilivu mkuu ktk kipindi hiki kigumu kwako, wewe pia ndugu na jamaa zako. APEPE Shemeji yetu!
 
Pole sana KKKiza, Muhumba ana njia nyingi za kukupatia uvumilivu na faraja - R.I.P Shemeji YETU - wote njia yetu ni moja yeye katangulia.
 
Pole sana KakaKiiza kwa msiba mzito. Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sasa KK, Mungu wa faraja zote akupe kustahimili
 
Naomba nikutie nguvu ktk kipindi hiki kigum kaka kiiza MUNGU ndiye kiongozi wa kila jambo mtegemee yeye mwisho utayaona mapenzi yake Bwana alitoa na Bwana ametwaa na jina la bwana libalikiwe
 
rest in peace mrs kiiza bwana ametwaa na bwana alitoa jina lake lihimidiwe
 
pole sana ...
Mwenyenzi Mungu awe nawe pamoja na familia yako..
 
Jana nilimtembelea KakaKiiza na kuzungumza naye kwa kirefu sana, ukweli ni kwamba mwenzetu amepata pigo kubwa sana kwa kuondokewa na mkewe kipenzi. kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatatu jioni katika makaburi ya Kindondoni.

Ni vyema kwa wale wana JF walioko jijini Dar kuungana na mwenzetu kumsindikiza mkewe katika safari yake ya mwisho.

Mwenye enzi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi .................amina

Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
 
Last edited by a moderator:

Asante sana Mtambuzi kwa hii taarifa, asante pia kwa kumtembelea na kumtia moyo, kwa kweli anahitaji sana watu wa kumfariji kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Kaka Kiiza MUNGU akupe nguvu.
JF tupo nawe katika kipindi hiki kigumu.

MUNGU ailaze mahali pema roho ya marehemu.
 
Back
Top Bottom