Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
CHADEMA Tanzania said:Tumepata taarifa za kushtua na kusikitisha sana za mauaji ya Katibu wa CHADEMA Manyoni Mash. Ndugu Alex Jonas yaliyotokea usiku wa jana, Mwembeni, Manyoni Mjini. Chama kinafuatilia kujua kilichotokea, kisha tutatoa taarifa juu ya tukio hilo.
Taarifa za awali zinaonesha kuwa mwili wa Katibu wa CHADEMA Manyoni Mash. Ndg Alex Jonas umekutwa ukiwa umekatwakatwa maeneo mbalimbali ya mwili, kichwani na mikononi. Tunalaani vikali tukio hilo na ukatili dhidi ya kiongozi huyo wa kisiasa
Soma: https://www.jamiiforums.com/threads...kini-hata-bodaboda-wanahitaji-ulinzi.1695913/
TANZIA, Katibu wa CHADEMA Manyoni Mashariki kamanda Alex Jonas (kushoto ) ameuawa kwa kupingwa mapanga usiku wa kuamkia leo