TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

Namkumbuka akiwa RC wa Mkoa wa Kilimanjaro, he was a heavyweight, tufike mahali viongozi wetu wenye uzito mkubwa hadi kuwa threath kwa afya na maisha yao, waingizwe kwenye weigh loss program za lazima kwa usalama wao!.

NB. Hii sio sababu ya kifo hiki but ni just thinking aloud kuhusu vifo vya ghafla vya watu na viongozi wetu wenye uzito mkubwa akiwemo Capt. John Komba.

RIP Mhe. Leonidas Gama
It's real brother too much fat is harmful
 
View attachment 636895

TAARIFA YA AWALI:


Wadau nimepata taarifa muda huu zinasema mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama hatunaye tena....

UPDATE:

JamiiForums imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.
Pia alikuwa kiongozi wa MBIO ZA MWENGE Mwaka 1990..
 
RIP- Mungu ampe hukumu ya haki! kwa humu alimopita akitimiza "wajibu wake"....
Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.
 
R.I.P

Nakumbuka lile daraja la mnepo pale Kiyungi, Kilimanjaro ukatufungulia daraja lipya na bado jina lako naliona kwenye ile beacon

Nakukumbuka tena kule Anwarite ukitoa vyeti na bado gazeti hilo ninalo dahhh

Tangulia sisi twaja
 
R.I.P Mzee Gama.... Nitakukumbuka sana wakati ukiwa RC Kilimanjaro... Nakumbuka sana mchango wako wakati ukiwa Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Mkoa.... Tangua mzee zote tu njia moja
Tatizo ni unatanguliaje? Kutangulia haina shida, ni unatanguliaje, umeacha maumivu/Neema/ upendo gani NYUMA
 
kifo kipo nasi kila sekunde kila pumzi, tujitahidi kutenda mema kila wakati. Poleni sana.
 
Hujamuelewa! Hajasema hakijamgusa bali "hakijamstua" akimaanisha kwa wenye maumbo kama yale huwa anawafikilia kuwa ktk hatari ya vifo vya ghafla kama hivi,,, BP.
Kuna Diwani mmoja kasema amesema Marehemu ametoka India siku za karibuni sana kwa matibabu,
 
Ni katika Hospitali ya Peramiho, Songea alikokuwa amelazwa kwa Matibabu
Tatizo ni unatanguliaje? Kutangulia haina shida, we will all follow suit, ni unatanguliaje, umeacha maumivu/Neema/ upendo gani NYUMA
 
Poleni sana ndugu na jamaa wa marehemu
 
Safi.Mwenyezi Mungu amuweke mahali pale panapostaili wale jamaa


Swissme
 
Back
Top Bottom