Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mchezaji wa mbao FC, Ismail Khalfani Mrisho afariki baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui FC kwenye mtanange uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba kwa wachezaji walio chini ya miaka 20 (U20).
Photo Credit; Faustine Ruta
KWEZISHO, Ismal Mrisho Alfan, amesafirishwa na gari iliyotolewa na uongozi wa manispaa ya Bukoba kusafirisha mwili wa kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 kwenda Mwanza wilayani Ilemela kwa maziko.
Alikuwa amehitimu kidato cha nne, alikuwa anavaa jezi namba nne, alikuwa amefunga goli la nne katika mashindano ya U-20, alitarajiwa kujiunga na academy nchini Marekani baada ya kufuzu katika majaribio, ingawa alirudi nchini kumalizia masomo yake ya sekondari, na ameaga dunia tarehe ya nne ya mwezi 12/2016.
==================
UPDATE
Mechi hiyo ilikuwa inachezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambako michuano ya vijana chini ya miaka 20 inaendelea.
Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC wakati wakiwania mpira na kuanguka na juhudi za kuokoa maisha yake zilionekana kukakwama.
Wakati mauti yanamkuta Ismail, dakika chache kabla alikuwa amefunga bao dhidi ya Mwadui.
Pamoja na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Kagera, taarifa baadaye zilizopatikana zilieleza, Ismail alifariki palepale uwanjani.