TANZIA: Mchezaji wa Mbao FC afariki baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Mwadui FC

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Mchezaji wa mbao FC, Ismail Khalfani Mrisho afariki baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui FC kwenye mtanange uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba kwa wachezaji walio chini ya miaka 20 (U20).


Photo Credit; Faustine Ruta

KWEZISHO, Ismal Mrisho Alfan, amesafirishwa na gari iliyotolewa na uongozi wa manispaa ya Bukoba kusafirisha mwili wa kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 kwenda Mwanza wilayani Ilemela kwa maziko.

Alikuwa amehitimu kidato cha nne, alikuwa anavaa jezi namba nne, alikuwa amefunga goli la nne katika mashindano ya U-20, alitarajiwa kujiunga na academy nchini Marekani baada ya kufuzu katika majaribio, ingawa alirudi nchini kumalizia masomo yake ya sekondari, na ameaga dunia tarehe ya nne ya mwezi 12/2016.
==================

UPDATE

Mechi hiyo ilikuwa inachezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambako michuano ya vijana chini ya miaka 20 inaendelea.

Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC wakati wakiwania mpira na kuanguka na juhudi za kuokoa maisha yake zilionekana kukakwama.

Wakati mauti yanamkuta Ismail, dakika chache kabla alikuwa amefunga bao dhidi ya Mwadui.

Pamoja na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Kagera, taarifa baadaye zilizopatikana zilieleza, Ismail alifariki palepale uwanjani.
 
Kifo ni kitu kidogo sana make nimeona video ni kama ishu ya kawaida sana lakini ndo ilikuwa mwisho wa huyu dogo. Imeumiza sana kwakweli, Poleni familia ya michezo na ndugu na jamaa.
 
Tunawakatia rufaa Congo wakati under 20 ..watu wanaleta mijitu mizima MRI itumike.. ..R. I. P Ismai
 
Waandaaji wana vichwa vigumu sana!!!
Unapelekaje masgindano eneo linaloangaliwa kwa jicho la husda?

Magu apeleke michango yetu aondoe Gundu!!!!
 
pamoja na yote, nadhani kuna haja ya kuwa makini katika kupima afya ya wachezaji na kufuatilia maendeleo yao kiafya kila wakati ili kujiridhisha kama wako fit kwa mechi....

Lilikua tukio la kawaida sana katika mchezo jambo ambalo linanishawishi kwamba labda hali yake ya afya haikuwa nzuri.

Pole kwa familia, pole kwa Mbao Fc pole kwa wapenda soka wote..
R.I.P
 
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea, poleni sana wafiwa,ndugu,jamaa na marafiki poleni sana.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…