TANZIA: Mchezaji wa Mbao FC afariki baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Mwadui FC

Inasikitisha sana....Mauti yalivyomkuta Mrisho Khalfan wa Mbao FC.... ANGALIA pia BAO alilofunga na alivyoshangilia dakika chache kabla ya mauti.... Hakika Mungu ni mkubwa....

https://www.facebook.com/video.php?v=1350999384945561

Hivi mnajua kuwa kuangalia video hizi za Facebook ni lazima uwe na account huko? Akaunti yangu ya Facebook niliifutilia mbali mwaka 2015 baada ya kuchoshwa na "axante beb gd9 2taxem kxho" na kuamua kujiunga JF. Video za YouTube ndo poa bana.

Mrisho Khalfan apumzike salama. Kama amefia uwanjani basi aangalau ameondoka wakati akifanya kitu akipendacho na hakuteseka. Sisi tuliobaki hatujui tutaondokaje. Jina la Bwana na lihimidiwe!
 
Duh hizi first aid za bongo. Kila mtu anavuta mguu wake
 
Duh hizi first aid za bongo. Kila mtu anavuta mguu wake
Ingawa kifo au ajali anapanga muumba lakini upo umuhimu wa kuhakikisha hao watoa huduma wanakuwa na utaalamu wa kutosha pamoja na vifaa stahiki. Hivi unafahamu marehemu alipelekwa hospitali na gari la zima moto?
 
Inadaiwa Ambulance haikuwapo uwanjani, alipelekwa na gari ya fire, pole kwa familia

Apumzike kwa amani ndogo wetu
Nchi ya hovyo hii, hata mie kila siku naliona fire ila sijawahi kuliona ambulance uwanjani
 
Huu ndio uanaume wenyewe unakufa ukiwa Kazini!!!!. Mwenyezi Mungu ampe pumziko lenye Heri na Amani ndugu @IsmailKhalfanMrisho
 
Nimeona video clip yake nimeshindwa kuirudia.... R.I.p Ismail
 
Rip Ismail hakuna kifo kinachokosa sababu wengine watakihusisha na nguvu za giza
 
Au goli limemcost,maana bongo kuna ndumba banaa kwenye soccer
 
Mkuu hii hali huwa inatokea sana kwenye michezo kwa mfano hata Marc Vivien Foe hakuwa amegongana na mtu ila alianguka tu peke yake na kifo kilimkuta pale pale .

Kwahiyo hata wakiwapima vipimo vya aina gani bado haitasaida chochote kwa sababu wakati mwingine ni kufeli kwa mishipa ya damu kufanya kazi yake katika hali ya kawaida.

Kifo kipo karibu sana na binadamu kuliko kitu chochote mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…