TANZIA TANZIA: Mchungaji Dkt. Peter Mitimingi wa Warehouse Christian Centre (WCC), afariki dunia

TANZIA TANZIA: Mchungaji Dkt. Peter Mitimingi wa Warehouse Christian Centre (WCC), afariki dunia

Kiukweli kama hii Corona ipo basi Mungu atupe watanzania wepesi wa kuelewa maelekezo tunayopewa na wataalamu wa afya.

Misongamano imekatazwa lakini hapa nashuhudia lundo la watu wakiwa wamejazana kanisani kumuaga marehemu mchungaji Mitimingi
Tatizo siyo kuaga mpendwa wao bali namna ambavyo hawachukui tahadhari katika mkusanyiko mkubwa kama huo.

Rip mchungaji Peter Mitimingi!
Leo akili imerudi lazima umekunywa alkasusu,wenzako wako chato wanafanya fumigation

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mchungaji na mwalimu Dkt. Peter Mitimingi wa Kanisa la Ghala la Chakula au kwa kimombo “Warehouse Christian Centre(WCC)” amefariki dunia, usiku huu. Mchungaji Mitimingi alizaliwa mwaka 1975.

Kabla ya kuanzisha kanisa lake hilo, alihudumu TAG kama mchungaji msaidizi na baadaye kuanzisha huduma ya injili vijijini.

Mch. Mitimingi anadaiwa alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili na Kafariki saa Tisa za alasiri

Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo Samwel, amethibitisha. “alikuwa anaumwa Sukari ilipanda, ikaanza homa ya mapafu kwasababu alikuwa Arusha akapigwa na mvua kukawa na baridi kali ikamsumbua”

Kaacha Mke na Watoto Wanne.


WASIFU WA MAREHEMU

KUZALIWA

Machi 03, 1975 -mkoani Tabora

ELIMU
Stashahada (Diploma) ya Elimu ya Kikristo - ICM Seminary Kenya.

Shahada (Bachelor) ya Biblia na Theolojia - Africa Theological Seminary - Kenya

Shahada uzamili (Masters) ya Ushauri na Saikolojia - Uganda Christian University

Shahada ya Uzamivu (PHD) - Africa Graduate Universty - Sierra Leone

KAZI
  • Mchungaji
  • Mkufunzi
  • Mwandishi wa Vitabu (ameandika vitabu zaidi ya 40)
  • Mshauri wa saikolojia na Biblia
  • Mhadhiri wa Chuo Kikuu

KUFARIKI
May 3, 2020 - Hospitali ya Muhimbili Familia

FAMILIA
Ameacha Mke na watoto wa 4

--
VIDEO: Kauli yake kuhusiana na Ugonjwa wa Corona


Marehemu Mchungaji Mitomingi, wiki tano zilizopita alipakia picha mbalimbali kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa anafanya ziara nje ya nchi ambapo alikaa kwa siku kadhaa na kurudi nchini. Baada ya kurudi nchini pia alipakia picha akionesha kuwa ameamua kujitenga(Karantini) ili kuweza kujua mwenendo wa afya yake kuhusu maambukizi ya Virusi vya Corona. Baadaye aliendelea kutoa huduma ya kiroho kwa waumini wake mpaka hapo alianza kuumwa na umauti kumkuta akiwa anapatiwa matibabu ya homa ya mapafu.

Baadhi ya mada zilizoanzishwa JF kuhusu alichokuwa anakifanya


Kuanzisha “Warehouse Christian Centre(WCC)”

Baada ya kutumika katika kanisa la Tanzania Asseblies of God (TAG ) zaidi ya miaka ishirini Mchungaji Mitimingi alizindua kanisa lake Jijini Dar es salaam ambapo alinukuliwa na vyombo vya habari kueleza kuwa hakuondoka kwa ugomvi.

"Sijatoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa ugomvi kama watu wanavyozusha bali nilikwenda kwa viongozi wa juu wa Kanisa. Nilianza na nyumbani Mwenge TAG ambapo nilikuwa mchungaji msaidizi, nikaenda kwa mchungaji wa wilaya, nikaenda kwa Makamu wa Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dkt. Magnus Mhiche. Wote hawa walinikubali, wakaniombea na kuniwekea mikono tayari kwa kutumika." Alisema Mitimingi.


UPDATE: 06 Mei, 2020 - MAZISHI

View attachment 1441582

PhD ya Sierra Leone?
 
Back
Top Bottom