TANZIA: Msanii wa Uganda, Moses Sekibooga a.k.a Radio afariki dunia

TANZIA: Msanii wa Uganda, Moses Sekibooga a.k.a Radio afariki dunia

Aligombana na baunsa kweli,majuzi niliona KTN wakijadili ethics za mabaunsa huko club mpk kuwaweka wenzao in comma wakihusisha na case ya huyo Msanii.
Kuna huyu kasema hivi

"Huyu jamaa alipigwa na watu wasio julikana, akiwa na Producer wake Aliye fanya nae ngoma ya mwisho ila bad haija Toka, ila inasemekana Huyo producer ndio alichora mpango mzima"
 
Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Radio amefariki dunia.

Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel, tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu.

Hapo jana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World.
 
Kufuatia kifo cha msanii wa muziki Radio aliyefariki alfajiri ya leo nchini humo, Rais wa Uganda Yoweri Museven ameonyesha hisia zake kwa kuguswa na kifo cha msanii huyo.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Museven ameandika “Have been told about the untimely death of musician Moses Ssekibogo aka Mowzey Radio. I had only recently made a financial contribution towards his treatment and hoped he would get better. He was a talented young person with a great future ahead of him. May he rest in peace.”

Taarifa za kifo cha msanii huyo zinakuja baada ya siku chache zilizopita Rais Museven kutoa kiasi cha Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo.

Vile vile wasanii mbalimbali kama Navio, Diamond, Eddy Kenzo, Professa Jay na wengineo wametumia kurasa zao za mitandao yao ya kijamii kama Instagram na Twitter kutoa pole kwa familia yake.

Baada ya kutangazwa taarifa za kifo mashabiki wa msanii huyo na wa Goodkife walifika hospitali hapo kushuhudia kinachoendelea.
 
Daah.nakumbuka mwaka 2009,nilikuwa na rafiki yangu anauza duka alikuwa ana mkubali sana jamaa.kuna siku alinipa 5000 akaniambia nenda kanitafutilie albam ya blue 3.
Alikuwa anakipenda kile kipande kinachosema.
"baby unanitesa kichiziiii....
Niliitafuta hyo album nikaikosa nilipomwambia alisikitika sana.gasper popote ulipo.msanii wako hayuko tena duniani.
 
Back
Top Bottom