TANZIA: Msanii wa Uganda, Moses Sekibooga a.k.a Radio afariki dunia

TANZIA: Msanii wa Uganda, Moses Sekibooga a.k.a Radio afariki dunia

RIP radio nakukumbuka kwenye nyimbo ya ability hii Ngoma ndio Ngoma niliyo iskiza kwa kurudia rudia mara nyingi kuliko Ngoma zote dunian nikiwa nipo juu ya ghorofa la sita hostel ya makelele iliyopo njia ya kwenda mukono .......nikiwa naliona jiji la kampala kwa chini daaah inatia uzuni
 
Kuna mada nimesoma humu et amepigana na baunsa wa club akapigwa na kitu kizito kichwani, which is which?
Aligombana na baunsa kweli,majuzi niliona KTN wakijadili ethics za mabaunsa huko club mpk kuwaweka wenzao in comma wakihusisha na case ya huyo Msanii.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi...Jina la bwana lihimidiwe mwenzetu ameondoka ila Fasihi aliyo tuachia haiwezi kufa itabaki milele kama kumbukumbu ya uwepo wake hapa duniani
 
alafu huyo dogo alikuw mdogo wake chamilion

All in all alale mahala pema peponi Amen

huyu jamaa misala yake ilikuwa ya ugomvi tu kupiga wasanii wenzake alishawah kumdunda bebecool na bouncer wke pia alishawahi kumpiga kaka yake chamilion kwa kile alichodai kwamba aliwaskia wakimsema vibaya yeye na mama yake ndipo akabisha hodi na kulianzisha vag

Rest In Peace kijana
 
ni kwamba jamaa alipata ajali ya gar s kutokana na ugomvi
 
alafu huyo dogo alikuw mdogo wake chamilion

All in all alale mahala pema peponi Amen

huyu jamaa misala yake ilikuwa ya ugomvi tu kupiga wasanii wenzake alishawah kumdunda bebecool na bouncer wke pia alishawahi kumpiga kaka yake chamilion kwa kile alichodai kwamba aliwaskia wakimsema vibaya yeye na mama yake ndipo akabisha hodi na kulianzisha vag

Rest In Peace kijana
nadhani umechanganya mkuu....mdogo ake chamileon anautwa weasel na sio radio
 
aise..namkubali sana huyu jamaa..ana voice flani ivi amazing..radio n wissle RIP you are going to bread n butter in hevean now
Acha unafiki ulikuwa unampenda mbona haukuwahi kupost post yoyote ya kuonyesha unampenda enzi za uhai wake,ndio maana kuna mistari ya marehemu langa kileo aliandika usisubiri mpaka nife ndio ukubari am the best
 
Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Radio amefariki dunia.

Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel, tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu.

Hapo jana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World.
 
Kufuatia kifo cha msanii wa muziki Radio aliyefariki alfajiri ya leo nchini humo, Rais wa Uganda Yoweri Museven ameonyesha hisia zake kwa kuguswa na kifo cha msanii huyo.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Museven ameandika “Have been told about the untimely death of musician Moses Ssekibogo aka Mowzey Radio. I had only recently made a financial contribution towards his treatment and hoped he would get better. He was a talented young person with a great future ahead of him. May he rest in peace.”

Taarifa za kifo cha msanii huyo zinakuja baada ya siku chache zilizopita Rais Museven kutoa kiasi cha Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo.

Vile vile wasanii mbalimbali kama Navio, Diamond, Eddy Kenzo, Professa Jay na wengineo wametumia kurasa zao za mitandao yao ya kijamii kama Instagram na Twitter kutoa pole kwa familia yake.

Baada ya kutangazwa taarifa za kifo mashabiki wa msanii huyo na wa Goodkife walifika hospitali hapo kushuhudia kinachoendelea.
 
Pole wazazi, pole waganda, pole Lillian mbabazi kumpoteza mzazi mwenzio tangulia ukapumzike paradiso mozey dunia mapito tu japo kua kuna waliojisahau nakujiona miungu watu mbele ya binadamu wenzao najua ulikua na mipango mingi juu ya carrier yako na kundi lako la Goodlife lakini Almighty God ndio master planner wa pumzi yetu ya kesho, hakika pumzi siri yake anayo Mungu alie tupatia tuipumue buree, hata uwe nani duniani pumzi ikikata mwili haufai kitu utaoza na kunuka na kutupwa shimoni
Tupendane binadamu Africa tupendane Tanzania tupendane utofauti wa wa siasa vyama usituondolee utu hakuna mwenye hatimiliki ya PUMZI

Rest in eternal peace mozey radio, Amen[emoji120]
 
alafu huyo dogo alikuw mdogo wake chamilion

All in all alale mahala pema peponi Amen

huyu jamaa misala yake ilikuwa ya ugomvi tu kupiga wasanii wenzake alishawah kumdunda bebecool na bouncer wke pia alishawahi kumpiga kaka yake chamilion kwa kile alichodai kwamba aliwaskia wakimsema vibaya yeye na mama yake ndipo akabisha hodi na kulianzisha vag

Rest In Peace kijana
Mdogo wake na chameleon ni Weasel na Sio Radio
 
Back
Top Bottom