Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza shabiki mkubwa wa Yanga, Ally Yanga amefariki dunia.
Taarifa zinaeleza, Ally Yanga amefariki dunia katika ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amethibitisha kwamba ajali hiyo imetokea leo mchana na Ally amepoteza maisha.
Ally Yanga anakumbukwa kutokana na mbwembwe zake kila Yanga ilipokuwa inacheza.
Alipenda kujipaka masizi meusi huku akiweka kitambi cha bandia.
mwanachama maarufu wa Yanga ,Ally Yanga amefariki dunia kwa ajali ya gari akiwa katika mbio za mwenge wa Uhuru wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Leo.
Yanga kifo chake kimetokana na gari alilokuwa akisafilia kuacha njia na kupinduka wakati akiwa kwenye shughuli za mbio za mwenge.
Marehemu Ally Yanga alikuwa na wenzake wawili katika gari aina ya Rav 4 ila inasadikika kilichopelekea kifo chake ni baada ya yeye kurushwa nje ya gari wakati wa ajali, wenzake wamejeruhiwa tu.