Hakika Mzee alisimamia kile anachokiamini. Amejitofautisha na wanasiasa tulionao hivi sasa leo unamchagua kama mpinzani kesho amewageuka. Huyu hakuwa kigeugeu, apumzike kwa amaniRIP Mzee wangu Mapalala,ulikuwa na siasa zenye misingi ya itikadi yako tangu enzi za ukoloni,hukubadilika.
Alikuwa CUF ipi ? Hii ya tawi la ccm?Mwanasiasa mkongwe Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki. Mungu amuweke mahali pema. Mzee Mapalala alizaliwa Februari Mosi, 1936.
Mtoto wa Mzee Mapalala, Bernard James amesema baba yake amefariki dunia leo saa 4:30 asubuhi hospitali ya Kairuki alikokuwa tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua.
Msiba uko nyumbani kwao Kinondoni.
Pia soma
James Mapalala: Mwanzilishi wa mageuzi aliyeishia kwenye mikosi
HARAKATI za mageuzi nchini zina historia ndefu, zikianza kabla ya uhuru ambapo wa wananchi kupitia vyama na vuguvugu za aina mbalimbali waliungana ili kuwaondoa wakoloni. Hadi mwaka 1961 chama cha Tanu kilichokuwa kikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere kilishinda uchaguzi na kuunda...www.jamiiforums.com
Mapalala haweshi ndani ya CUF
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi wa Kilwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Magengeni Kilwa Kivinje katika ziara yake ya baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara. Kama CUF iliweza kukaa pamoja na CCM iliyodaiwa...www.jamiiforums.com
James Mapalala: Warioba amewavuruga CCM
FRIDAY, 28 MARCH 2014 James Mapalala (kulia) akiwa na Rais Jakaya Kikwete Mwanasiasa mwenye historia ya kipekee nchini, James Mapalala amesema ufafanuzi wa Rasimu ya Katiba uliotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, umekiacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye wakati mgumu. Mapalala, ambaye...www.jamiiforums.com
Yu wapi James Mapalala mwanzilishi wa CUF?
Huu mzozo aside, Mapalala anasema Hamad Rashid Mohammed ni mtu muhimu sana katika CUF kwa sababu ndiye mtu pekee anayeweza kwenda kutafuta fedha nchi za nje kwa ajili ya chama (kuomba misaada) ? Hawa ndio wanamapinduzi wetu jamani. ---- Ni kweli J. K. Mapalala alikuwa ni mmoja wapo katika...www.jamiiforums.com
Vipi kwa sasa? wanathaminiwa?Apumzike kwa Amani
Miaka ile Cuf ina Nguvu,wakristo walikuwa wanapuuzwa sana Ndani ya chama sijui Kwanini
Hapana kaka.Wanyanwezi wako vizuri toka CUF ianzishwe imebaki mikononi mwa wenyeviti wa taifa wanyanwezi Hadi Leo.Hammad alijitia kuleta za kuleta kumfukuza Lipumba akamrudia akampokonya chama na kukirudisha kwa wanyamwezi.Toka CUF ianzishwe wenyeviti taifa Ni wanyamwezi tu
Wote hao wanyamwezi Shaban mloo mnyamwezi wa Zanziba kule kuna wanyamwezi wengi mmojawapo Ni huyo Shaban Mloo .,Mageni Mnyamwezi wa Tabora,Lipumba Mnyamwezi wa Tabora.Hapana kaka.
Baada ya James Mapalala kupokonywa uenyekiti, mwenyekiti aliyefuatia alikuwa Shabani Hamis Mloo kisha akachukua Musobi Mageni. Baada ya Mageni ndo akaja Ibrahimu Lipumba wa kudumu toka miaka hiyo.
kinondoniMzee wetu wa tbr huyu.Msiba upo wapi ?
Mageni ni wa Kwimba bwana,huyu si ndiyo alikuwa BABA WA MAREHEMU LETICIA NYERERE;Wote hao wanyamwezi Shaban mloo mnyamwezi wa Zanziba kule kuna wanyamwezi wengi mmojawapo Ni huyo Shaban Mloo .,Mageni Mnyamwezi wa Tabora,Lipumba Mnyamwezi wa Tabora.
Hamad alikua mdogo sana kipindi hicho, hapa unazungumzia mtu Kama Shabaan Mloo. Huyo Hamad wa juzi tu.Yule mpemba Hamad yule alimpora mwenzie chama kwa ajili ya tamaa
Sasa nae kaporwa na Lipumba
Ina maana Lipumba kaja kumsaidia ngosha mwenzie
Yule mpemba Hamad yule alimpora mwenzie chama kwa ajili ya tamaa
Sasa nae kaporwa na Lipumba
Ina maana Lipumba kaja kumsaidia ngosha mwenzie