TANZIA: Mwanasiasa mkongwe na Mwanzilishi wa CUF, James Mapalala afariki dunia

TANZIA: Mwanasiasa mkongwe na Mwanzilishi wa CUF, James Mapalala afariki dunia

RIP mzee Mapalala. Umeacha historia.
Nakumbuka Lyatonga alivyokusumbua miaka ya 90 lakini bado uliendelea kukomaa tu.
 
Nadhani mtt wake benard mapalala umemsoma vitabu vyake form two, sijui kumbukumbu zangu zipo sawa
WanaJamiiForums,

Baada ya kupitia comments za wanaJF nimebaini James Mapalala (RIP) ni mtu-tajwa, al maaruf, mtoto wa mjini, mwanasiasa mkongwe n.k

Mfanyieni haki Mzee Mapalala kwa kutuwekea historia ya mapito yake yote tujifunze. Maana nimepita YouTube, Google kuona historia yake lakini kuna citation fupi fupi tu.

Wenye kumfahamu Mzee huyu mkazi wa muda mrefu Dar es Salaam tupieni habari ndefu. Ila wazee kama hawa maarufu ni muhimu wao wenyewe kuwa na tabia ya kuandika vitabu au kukubali mahojiano na waandishi wa habari ili historia muhimu ya nchi hii isipotee.
 
James Mapalala,pumzika kwa amani...... Nakumbuka miaka ileee wakati vuguvugu la siasa za vyama vingi linaanza Tz.......
 
Alikuwa mwanzilishi wa CUF,pia ni mwenyekiti wa kwanza wa CUF Tanzania bara.Sema wakamletea figisu kuwa ni msaliti na anashirikiana na CCM.Maalim Seif ndo alianza figisu kusema kuwa wafadhili hawataki kutoa misaada,wafadhili hapa nasemea Waarabu,kisa eti James ambae ni Mkristo ni Kafiri.Yaani chuki zilianzishwa na viongozi wa Zanzbar ambao ni maalim Seif na genge lake.Walifikishana kwa msajili wa vyama kipindi hicho akiwa George Liundi.Mwaka 1994 Ndo alitolewa uenyekiti;Alishinda mwaka 1993 hivyo hata hakukaa sana.
Ndo ukawa mwisho wa James Mapalala kuwa Mwenyekiti CUF Bara.

Hivi weye mwana Lumumba na version yako yakipropaganda za uzushi wa CCM unaweza kutuletea uthibitsho wa hao wanaoitwa wafadhili kugoma kwao kutoa misaada kwa sababu mwenyekiti kuwa ni mkristo?
 
Tatizo halikuwa dini ila chama kilikuwa hakitambui mapinduzi matukufu ya 1964, chama kilishikilia serikali ya Sultani ya 1963 ilikuwa halali!!!!nenda kwenye makataba(library/archive) utapata historia!!

SIo kilishikilia tu, mpaka chama cha CUF kinavujika huo ndio ulikua msimamo wao, Na sasa unaendelea ndani ya ACT. Na sio CUF/ACT tu Dunia nzima ndivyo inavyotambua kuwa Uhuru wa Zanzibar ni 1963 isipokua CCM.
 
kwa Bwana kila goti litapigwa. Bwana ametoa Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Mwanga wa milele umuangazie mzee wetu na Mwanamageuzi halisi aliyeasisi chama cha Kamahuru kilichounganishwa kikawa CUF

Kamahuru kilikua chama cha wafuasi wa Seif mkuu sio mapalala, vuta kumbukumbu vizuri
 
Mwanasiasa mkongwe Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki. Mungu amuweke mahali pema. Mzee Mapalala alizaliwa Februari Mosi, 1936.

Mtoto wa Mzee Mapalala, Bernard James amesema baba yake amefariki dunia leo saa 4:30 asubuhi hospitali ya Kairuki alikokuwa tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua.

Msiba uko nyumbani kwao Kinondoni.

Pia soma

RI Peace Hayati Mh.James Mapalala,

nakumbukua Nkiwa mdogo sana shaggz kwetu enzi hizo siasa za mageuzi zinaingia kushika hatamu nchini ....

nilikua kijijini alipitaga na kufanya mkutano wa siasa kwenye mnumbaga alikua amesubiriwa kwa hamu sana akaja akaongea alikuaga na nywele nyeupe mvi hizo wananchi wakatoka hapo wanasema atakua na busara sana huyo kijiji karibia nusu wakachanja kadi za mageuzi.
 
Sad enough sidhani kama alikua full acknowledged kama mwanzilishi wa CUF...ingawa na uelewa wangu naona na kuhisi alifanya kazi kubwa sana kueneza upinzani

ni kama historia ya chama ilimfuta....wahenga watuambie
 
Hamad alikua mdogo sana kipindi hicho, hapa unazungumzia mtu Kama Shabaan Mloo. Huyo Hamad wa juzi tu.

Walikua Pamoja katika harakati.Wakati Maalim Seif Waziri Kiongozi Zanzibar , Shaaban H Mloo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Na walitimuliwa wote CCM baada ya ile hali mbaya ya kisiasa kule Zanzibar.
 
Hivi weye mwana Lumumba na version yako yakipropaganda za uzushi wa CCM unaweza kutuletea uthibitsho wa hao wanaoitwa wafadhili kugoma kwao kutoa misaada kwa sababu mwenyekiti kuwa ni mkristo?
Hayo ndo yalikuwa madai ya Maalim Seif. Alipokuwa anampiga vita James mapalala. Note:Mimi nimesoma makablasha tu na kusikia story kutoka kwa wanasiasa wa kipindi hicho.
 
Hayo ndo yalikuwa madai ya Maalim Seif. Alipokuwa anampiga vita James mapalala. Note:Mimi nimesoma makablasha tu na kusikia story kutoka kwa wanasiasa wa kipindi hicho.

Madai ya Maalim Seif yalikua ni kwamba Mapalala alikua anatumiwa na CCM. Kama ilvyokua kwa Lipumba
 
Mwanasiasa mkongwe Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki. Mungu amuweke mahali pema. Mzee Mapalala alizaliwa Februari Mosi, 1936.

Mtoto wa Mzee Mapalala, Bernard James amesema baba yake amefariki dunia leo saa 4:30 asubuhi hospitali ya Kairuki alikokuwa tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua.

Msiba uko nyumbani kwao Kinondoni.

Pia soma

Kama kitu hujui uliza. CUF ilianzishwa na Mwl Kassala aliyekuwa akitundisha IFM na ilianzishwa katika Function Hall ya IFM. Upo hapo!
 
Hayo ndo yalikuwa madai ya Maalim Seif. Alipokuwa anampiga vita James mapalala. Note:Mimi nimesoma makablasha tu na kusikia story kutoka kwa wanasiasa wa kipindi hicho.
Mtafute Mwl Kassala aliyetunga katiba ya kwanza ya CUF, na ni homeboy wa Mapalala
 
Huyu ndio Mwasisi wa Usaliti Tanzania , namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali inapostahili kutokana na Matendo yake , Amina
 
Back
Top Bottom