TANZIA: Mwanasiasa mkongwe na Mwanzilishi wa CUF, James Mapalala afariki dunia

TANZIA: Mwanasiasa mkongwe na Mwanzilishi wa CUF, James Mapalala afariki dunia

Jembe la Tabora hili mitaa ya Nzega - Pumzika pema kamanda chief na muasisi wa siasa za Upinzani Tanzania. Kinachouma zaidi ni kwamba wewe umeondoka na chama ulichokiasisi nacho kimeshaondoka - too sad.
 
Aliporwa madaraka na mzee wa madaraka Maalimu Seif.kwa laana ya Mzee Mapalala na Aboud Jumbe,maalim kawa mtu wa kutanganga''jangwani'' sasa kawa chini ya Zitto.

Hivi kwani Maalim Seif ndie aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF baada ya kuondoka kwa Mapalala?
 
RIP baba wa mageuzi Tangulia nasi twaja lakini nina swali kwa wenyekujua Kwani mzee mapalala Yule mtangazaji pale RFA MWANZA Benady James ni mwanae mapalala?
Hapana sio mtoto wake
Watoto wake wa mwisho ni wa kike
 
Acha kusema uwongo. CUF ilikua ni muungano wa vyama viwili vya Kamahuru na Civic Movement sas huyo Seif alikaribishwa wapi?
Sasa seif si ndio aliomba waungane
Mapalala km mwenyekiti alikubali
So angekataa ingekuwaje?
Kubali seif alikuja na lake lingine la tamaa na ubaguzi
 
Sasa seif si ndio aliomba waungane
Mapalala km mwenyekiti alikubali
So angekataa ingekuwaje?
Kubali seif alikuja na lake lingine la tamaa na ubaguzi

Mbaguzi ni wewe mkuu unaeishi kuchukia watu waliokua hawajakufanya kitu
 
Mwanasiasa mkongwe Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki. Mungu amuweke mahali pema. Mzee Mapalala alizaliwa Februari Mosi, 1936.

Mtoto wa Mzee Mapalala, Bernard James amesema baba yake amefariki dunia leo saa 4:30 asubuhi hospitali ya Kairuki alikokuwa tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua.

Msiba uko nyumbani kwao Kinondoni.



Pia soma










====

Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, James Mapalala amefariki dunia katika hospitali ya Kairuki alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Oktoba 23, 2019 mtoto wa mwanasiasa huyo, Bernard James amesema baba yake amefariki dunia leo saa 4:30 asubuhi.

“Alikuwa hospitali tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua,” amesema James.

Amesema familia imekusanyika nyumbani kwao Kinondoni kupanga ratiba ya mazishi.

Mapalala aliyezaliwa Februari Mosi, 1936 ameacha mke na watoto kadhaa.

Alikuwa miongoni mwa wanasiasa wa kwanza waliojitosa kudai mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini Tanzania.

Kufuatia madai hayo, Mapalala alifungwa miaka miwili mkoani Lindi kuanzia mwaka 1986 hadi 1989 na baada ya kutoka aliwekwa kizuizini kwa kipindi cha mwaka mmoja katika kisiwa cha Mafia baada ya kuanzishwa chama cha siasa wakati sheria ilikuwa hairuhusu.

Alianzisha Chama cha Wananchi (CCW) mwaka 1991 na baadaye kiliungana na chama cha Zanzibar – Kamahuru na mwaka 1993 kuzaliwa Chama cha Wananchi (CUF).
RIP Mzee Mapalala.
 
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwenye amani milele yote. Amina.
 
Back
Top Bottom