TANZIA Tanzia nabii Flora Peter, amefariki dunia katika Hospitali ya Kitengule Jijini Dar es salaam

Huko daslam kila mtu ni nabii🙆🙆
Kuna familia naijua kuna nabii mwanamke nae yupo daslam, kawa mweupeee kajikondeshaaa, anaishi mbezi Beach anapenda kutukuzwa kama malkia au mfalme afanyiwe kila kitu na wajinga wapo wanamfanyia, ana kisirani na maringo km ndie Maria mzaa yesu, familia husika kaigawanya sababu ya majungu na kuamka kuita wasiomuamini kuwa ni wachawi yani ni vituko show
 
Aaah hawa manabii kiboko🙆🙆🙆
 
Aise we kweli kiboko unamjua vizuri hayati Nabii florah, Danny hakuwa daktari alikuwa kijana amemaliza feza sekondari tuu. na sasa kapagawa kidogo akili nilimuona anatembea kwa mguu bonde la magomeni kwenda faya anaongea peke yake. Mungu amrehemu nabii florah
 
Kati ya Waumini wake wa Kwanza 11 tuliokuwa tukisali nae pale Mbezi Beach Maguruwe katika Nyumba ya Willy ( Wile ) kati ya mwaka 2011 hadi 2012 ( akitokea Kigamboni alikokuwa akihudumu chini ya Mtumishi mmoja mkubwa tu kule ) nami GENTAMYCINE nilikuwa ni Mmoja wapo. Na labda leo kupitia hapa niseme tu kuwa Marehemu kwa kiasi fulani alinibariki mno kwa Maombi yake Kipindi kile ana Nguvu na alikuwa ni Mtu wangu wa karibu na tulizoeana na alinipenda mno ila baadae Majukumu mengine yalinipata na nikaanza kuwa nae mbali japo kila mara nilipokuwa Mjini nilikuwa nikienda Kumtembelea. Na nakumbuka hata mara ya mwisho nilipokutana nae mwaka 2021 alinilaumu mno kwa Kupotea na Kumtenga huku akiniambia kuwa ilikuwa kidogo Afe kwani alikuwa ndiyo ametoka Kulazwa na kufanyiwa Oparesheni ya Utumbo tatizo ambalo nadhani huenda ndiyo likawa kwa kiasi fulani limechangia kuondoa Uhai wake. Nje ya Majukumu yake ya Kiimani ( kuwa Nabii na Mtumishi ) Flora Peter alikuwa ni Dada Mcheshi, Mkarimu na mwenye Huruma sana hivyo hata kama Watu wengi hapa katika hii Thread watamsema vibaya na Kumchafua ila alikuwa ni Dada wa Kipekee kama ukipata bahati ya kuwa nae Karibu.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake Nabii Flora Peter mahala pema Peponi. Nimepoteza Rafiki mzuri na Dada mwema.
 
Kiongozi umepita mulemule
 
Watoto yatima imekua ngazi ya waanzisha makanisa siku hizi.
 
huu unabii wa karne hii huu mmmhh.wakristo mjitafakari sio kila ukilala ukaamka unajiita nabii,hiv mnajua hata sifa za binadamu kuitwa nabii??
Nasikia shekhe Sharifa majini na Sule wewe ndo unaowashikia vitabu
 
First time unamwongelea mtu positive na kwa unyenyekevu, wee Fuloo ulimpa nini genta
 
Huyu Flora pale kanisani kwake Salasala alikuwa anawaambia waumini wanyanyue Waleti na Pochi Juu ziombewe zipokee Miracle Money.

Wanaosali walisema hela zilikuwa zinajaa kweli ila sina uhakika nao
 
Biblia inasema, usihukumu usije ukahukumiwa.
Nilijikuta nimefika kwa Nabii Frola nikimsindikiza jamaa yangu ambaye alipotelewa na mtoto. Tulifika hapo baada ya kuwa tumemtafuta mtoto siku 2 kila mahali hadi mortuary bila mafanikio. Watu wakawa wameshauri twende kwa Nabii Frola na ndio ikawa first time yangu kwenda pale.

Nilipomuona; kibinadamu nilishangaa kutokana na mavazi yake pia alivyojipamba. Tulimuelezea kuwa kijana amepotea akienda shule. Akaomba sana na akatuambia anamuona kijana yupo hai, tena yupo eneo lenye watu wengi amevaa kofia na nguo chafu chafu tena hajielewi na amekaa chini ya watu. Akasema tuanze kumtafuta kuanzia mwenge hadi external pembeni ya barabara tutamuona. Binafsi sikuwa nimemuamini ila kwa kuwa namsindikiza jamaa yangu; nilimtia moyo tukatoka na kuanza kumtafuta. Kwa mshangao tulimkuta kijana chini ya daraja la Ubungo (wakati ule bado hawajajenga) na kwa juu kulikuwa na watu wengi na biashara mbalimbali zilikuwa zikifanywa kama Nabii alivyosema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…