mwaka 2014 mwezi 12 nilinusurika kufa maji msasani beach baada ya maji kurudi nilikuwa mbali kidogo na ukingo wa bahari.nilitumia maarifa na nguvu zangu zote kujiokoa nilikuwa nimevaa vest na boxer cha ajabu ile vest na boxer niliiziona nzito na sijui nilizivua vipi na kubaki uchi nilipiga miguu mpaka msuli wa mguu moja wa kushoto ukanishika niliishiwa nguvu nikiwa naelekea chini huku nimisha kubali kifo bahati nzuri ile nimegota chini nayasikia maji utosini nikaenda mbele kidogo ndipo yakanifikia machoni.
tokea mwaka 2014 sijawahi kurudi baharini tena wala kusogelea maji yoyote kwa ajili ya kuogelea-bahari sasa naiona kama kituo cha polisi.