Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Mbu

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2007
Posts
12,752
Reaction score
7,861
Wajemeni eeh

Kuuliza si ujinga na kuuliza njia ndio kujua njia!

Nahitaji bastola, kwa self defence tu, si vinginevyo! Sababu; najiona vulnerable mno huko 'uswekeni' ninakoishi. Hamna umeme, na majirani wanahesabika, BTW, practicing targets zipo za kutosha huko!

Najua humu kuna wengi tu wanaomiliki silaha kikazi, na wanaomiliki silaha kwa sababu kama zangu mie,..tatizo sijui "a" wala "be" nianzie wapi, meaning sheria na taratibu zikoje Bongo kumiliki silaha, hivi kuna duka la silaha Bongo?

Wapi?

Mfano; nikipata semi auto M92 Beretta yenye uwezo wa rounds 12 au 15 inatosha, au kuna 'limit' ya silaha ya aina gani naruhusiwa kuwa nayo? natamani kuagiza nje lakini nahofia nisijebanwa na sheria za uingizaji silaha...





Sheria ya umiliki wa Bunduki Tanzania

 
Mfano; nikipata semi auto M92 Beretta yenye uwezo wa rounds 12 au 15 inatosha, au kuna 'limit' ya silaha ya aina gani naruhusiwa kuwa nayo? natamani kuagiza nje lakini nahofia nisijebanwa na sheria za uingizaji silaha.

Good reliable gun. Ila stopping power yake sio kubwa, risasi za 9mm zinapenya, stopping power yake sio kubwa sana unless umelenga sehemu nyeti. Silaha ya kujilinda ningeshauri kuwa na bastola inayotumia risasi .45 ACP, k.m. Heckler & Koch USP.
 

Maduka ya kununua bastola dar yapo kama 2 ninayoyafahamu moja lipo pale mitaa ya stesheni, nyuma ya jengo la TRA, linaitwa Tanganyika Arms. Hili ni private(meaning price pia ni kubwa). Pia unaweza kwenda kununua pale Makao Makuu ya Jeshi Upanga kuna duka la Mzinga(bei fresh sana pale ila nyingi ni za kutoka nchi za kisoviet). Vile vile unaweza kuagiza ulaya kama unataka quality like Colt 45 na ikifika unaiclear halafu inahifadhiwa pale Tanganyika Arms mpaka upate kibali(Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear. Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana. Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Kuna watu imewachukua zaidi ya mwaka kwa hii process, lakini wengine inachukua miezi 2, depending on your connection.

Goodluck
 
ya kupigia wanyama au watu?

😀 ...acha maskhara yakhe! Bastola ya kuulia wanyama? ...kwa self defence, wala sio kusudio langu kuua mtu, huko 'porini' nikivamiwa na majambazi ya Kibongo atleast nijue wapi pa kutokea.

si nunua panga au .. uhame tu hapo unapokaa ....mtu mwenyewe kasema hajui lolote kuhusu mtutu sasa mnampeleka tu .. tutampoteza oho .... we haya

No naimaomari, ni taratibu tu za kumiliki silaha bongo. MajambaZI wa Bongo wanapokuja na AK-47 na kufunga mtaa hilo panga wala hutoliona... labda unipe mbinu za 'kinjeketile Ngwale' za kugeuza risasi kuwa maji!
 
Good reliable gun. Ila stopping power yake sio kubwa, risasi za 9mm zinapenya, stopping power yake sio kubwa sana unless umelenga sehemu nyeti. Silaha ya kujilinda ningeshauri kuwa na bastola inayotumia risasi .45 ACP, k.m. Heckler & Koch USP.

Na kweli M42 pia uwe umeshiba wakati unafyatua. Hiyo .45 ACP H&K USP inakitako kikubwa, handling yake mgogoro, sitaki dubwana linalo 'bulge' kwenye nguo.

Nini ushauri wako kuhusu Sig sauer P250 9para, au TAURUS slim 9para? ...all in all ni silaha ya self defence tu... not less than 12 rounds, ukivamiwa na mwenye AK-47 si unajua tena yeye 'ananyeshea mvua' tu mpaka magazine yake iishe.
 


...na kweli ni mtiririko mrefu... unatoa mianya mingi ya rushwa humo 'njiani', anyway,

mtaka cha uvunguni...

...hiyo silaha, nitaruhusiwa kwenda nayo Zanzibar? nasikia huko huruhusiwi mtu yeyote kumiliki silaha?

Thanks for your very useful info.
 
Mimi ya kwangu nimeitoa hivi majuzi tuu baada ya process ndeefu. Mane, I feel like bustin' a cap in some nigga's ass! (teh-teh-teh).

...Lucky you!,

...tatizo unaweza ukajiona kama John Wayne wakati dereva wa dalafala anakupa 'mid-finger salute' nawe upo full loaded!

😀

hizo process ndeeeeefu ndio mimi zinaniacha hoi...
 
...na kweli ni mtiririko mrefu... unatoa mianya mingi ya rushwa humo 'njiani', anyway,

mtaka cha uvunguni...

...hiyo silaha, nitaruhusiwa kwenda nayo Zanzibar? nasikia huko huruhusiwi mtu yeyote kumiliki silaha?

Thanks for your very useful info.

Zanzibar hawaruhusiwi kumiliki silaha.

Ukiwa unamiliki bastola lazima ujue kuitumia vizuri, isije ikakudhuru mwenyewe kwa kujipiga risasi, au kuingia katika hali ya kuhatarisha maisha yako. Unapomiliki silaha, hasa ya kujilinda inabidi ujue sheria vizuri, na ni yepi yatakayokusibu ukiwa umejeruhi/kuua mtu.

Hivyo ni vizuri kuifahamu silaha yako vizuri, kwenda range mara kwa mara, na ikiwezekena kujiunga na club za kufanya mazoezi ya kujilinda.

Huko utafundishwa namna ya kufanya pindi utakapojikuta katika hali ambayo itabidi uchomoe bastola yako.
 
Ndugu yangu, mshale wa kisasa ni more effective na efficent kuliko bastola. Na hauna matata kisheria unaweza kumiliki bila kibali, na ni mzuri sana kwa kupambana na majambazi na wezi, very silence! Ukikaa mahali na mishale yako ukifyautua hawezi kujua uko wapi, tofauti na bastola( Labda iwe na silencer) Lakini unatakiwa kujua namna ya kuutumia, Ushauri tu.
 

Hizo bastola ulizotaja ni nzuri, na zinafaa kwa carry conceal, lakini ushauri wangu utafute bastoa inayotumia caliber kubwa ya risasi k.m. .45 ACP. Hii ina stopping power kubwa ambapo ukimpiga adui lazima itamuangusha mara moja. Caliber ya 9mm sio mbaya, ila stopping power yake sio kubwa kama .45 na inaweza kupenya isifanye madhara sana ya kumsimamisha adui mara moja. Ningeshauri bastola ya aina hiyo hiyo kama sig p220 .45 compact
 
na smell smell mtu anataka kudito watu....kijana angaliaaaa!!!!mie ushauri wangu ingia gym kula nondo la nguvu ukitoka kachukue tizi la karate self defense tosha kabsaaaa tuone ka kuna mtu atakusumbua wala kukugusa!!
 
na smell smell mtu anataka kudito watu....kijana angaliaaaa!!!!mie ushauri wangu ingia gym kula nondo la nguvu ukitoka kachukue tizi la karate self defense tosha kabsaaaa tuone ka kuna mtu atakusumbua wala kukugusa!!


...Risasi inapofyatuliwa kuna mawili, moja ukiusikia mlio wa bastola/bunduki jua imemkukosa hiyo! PILI kwa mlio huo huo, utalala chini mwenyewe bila kuambiwa, nilikuwa mahala zikafyatuliwa toka kwenye AK-47, ...palifuatia ukimya kuanzia Binadamu, mbwa mpaka Mbu...!
 

Kitia, ahsante sana kwa ushauri, darasa nimelielewa. Shukran.
 
Ukiona urasimu bongo mkubwa kama ilivyo jadi,sema nikupe bastola ya kijadi.Haina usajili,leseni haina wala hakuna atakayejua kama unayo.Bastola hiyo ni kwa ajili ya kuzuia wezi tu si kuua wala kwenda kuibia.

Ni kimti fulani unaweka home kwako basi,wezi wakija nyumba hawaioni basi,kama una mshiko mkubwa,basi unanusa kijiti chako,vibaka/wezi hawakuoni.Hizo za kisasa balaa.
 

Kila la heri katika jitihada zako za kulijinda wewe na familia yako pia na mali zako. Ombi moja tu ukiipata basi uwe makini sana mahali unapoiweka ili isije ikasababisha madhara makubwa ndani ya familia yako.
 

(Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Je taabu yote hii.

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear. Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana. Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Ni kwasababu ya kupata serial number nyingine ama ndiyo kawaida ya process hata kama serial number ni sahihi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…