Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Mchongoma unaweza kuwa na bastola na bado ukazidiwa ujanja..hujawahi kusikia kisa cha muungwana mmoja alipokonywa bastola yake kwa kisu?
 

...Mid-aged!, u miss ulishampita. Sasa poda tu kwa wingi, kujifukiza, na khanga za mafumbo! mwanamke wa pwani wala hana kuji 'tune' sana, ushauri wa bure; usiache Gym na aerobics za hapa na pale, kina mama wengi wanajisahau na kupoteza mvuto wakishawekwa ndani!

QUOTE]

k.i.s.s
 
Mchongoma unaweza kuwa na bastola na bado ukazidiwa ujanja..hujawahi kusikia kisa cha muungwana mmoja alipokonywa bastola yake kwa kisu?

...aaaaarrrgggh Icadon, acha kutisha wenzio!
 
£50 unapata semi-pistol maeneo haya. Kama jamaa kachacha hata £20. Tunaita asante kosovo.

Personally, I believe a man who walks around with a gun/knife is a pussy!! Seen guys in bongo who are happy to flash it. Yeah, that makes you a man now huh?

Kama unaitumia kwa self-defence nyumbani poa. Ila wife (au binti) asikosee tu siku moja akaji-hairdry mabutu!!
 
Mimi ni mtanzania wa kawaida(sio tajiri wala sio masikini) na ninahitaji kumiliki 'silaha ya moto'. Naomba mtu yeyote anaefahamu taratibu za kufuata ili mtu aweze kumiliki/kumilikishwa bastola au bunduki kihalali (kisheria) kwa ajili ya personal security.

Je ni ofisi (au sehemu) gani hapa Dar es salaam wanashughulikia issue kama hii na je gharama zake kwa wastani ni kiasi gani? Pili, je kuna vielelezo vyovyote vinavyotakiwa kuwakilishwa ili mwananchi aweze kumilikishwa hiyo bastola?
Asanteni wana jf.
 
Mkuu nani kakukera? Huna haja ya bastora kama hutaki show off huku mtaani, wewe nenda kwa babu umtengeneze huyo mbaya wako wala hakuna procedures kama za kumiliki silaha.

Nasikia unahitaji kupa utambulisho kutoka kwa M/kiti wa mtaa, pia ni lazima wakazi wa eneo lako wathibitishe kuwa wewe ni mtu safi huna hasira wala historia ya uhalifu baada ya hapo lazima daktari athibitishe kuwa unaakili timamu then ndio unaenda wizara ya mambo ya ndani kuendelea na process ambazo pia ni cumbersome.Nakushauri we mroge huyo mbaya wako.
 
Mkuu salama kweli? Nenda kituo cha Polisi kilicho jirani yako na waombe wakupe taratibu zote za umilikishwaji silaha. Wao ndio competent authority kwenye mambo ya silaha ofcourse kuna mapendekezo lazima yatoke serikali ya Mtaa/Kijiji unachoishi n.k.
 
Unanunua, unasajili polisi, wanafanya uchunguzi baada ya kama mwezi na kitu unapata kibali halali cha kumiliki silaha.

Yapo maduka ya serikali yenye kuuza ila ni vyema ukaenda ktk kituo chochote cha police watakupa utaratibu wote, uwe makini pia maana kuna lundo la matapeli wanaweza kula pesa yako na usitoe rushwa.

Barreta inaweza kucost kama milioni moja ikiwa ni pamoja na kibali.
 
Miaka 3 iliyopita niliwahi kwenda kwenye lile duka la silaha pale Samora (Behind TRA) ili kujionea Silaha zenyewe. Walinipokea vizuri tu na walikua cooperative sana kunionyesha silaha za aina mbalimbali, kunitajia bei zake na hata kunipa nizishike na kuzikagua endapo ningeipenda.

Waliniambia kama kuna niliyoipenda utaratibu ni kwamba ningetakiwa kulipia Full amount (ilikua ina Rage from 700,000 to 1,500,000 depending on features) Lakini huchukui Silaha.

Baada ya hapo wangenipa Fomu 1 in 4 copies, ambayo ningeenda nayo Serikali za Mitaa, Kamati ya usalama ya Mtaa ingekaa na kunijadili na kuziforward hizo Form katika Kamati ya Usalama ya Wilaya ambapo wangezipitia na Kuziforward Katika Kamati ya usalama ya Mkoani na hatimaye mwishoni zingepelekwa Central Police Station.

Kila Stage itakapopitia copy moja ya hizo fomu hubaki huko kwa kumbukumbu. Vilevile walisema the main uzito mkubwa uko katika mapendekezo ya kamati ya usalama ya mtaa na Wilaya, Zikipita stage hiyo Mkoani na taifani hakuna shida kwa sababu hawakufahamu.

Baada ya Fomu kufika Central Policy Station, wao watakuita na kama wameridhika na recommendation za ngazi zote watatoa idhini ya wewe kwenda kuchukua hiyo silaha yako uliyolipia, Pamoja na Kitabu cha Silaha hiyo ambacho kitatumika wakati wa ukaguzi wa Silaha unaofanyika kila mwaka.

Unless wewe ni mwanajeshi au Polisi, Utatakiwa kulipia gharama za mtu kukupeleka Range kwa ajili ya kujifunza kutumia Silaha.

Process nzima kuanzia ulipolipia hadi kukabidhiwa silaha yako inaweza chukua miezi mitatu

Baada ya hapo unakua Mmiliki halali wa Silaha.
 
Enheee, sasa kweli watu wamechoka amani wenzetu huko...duniani...wanajaribu kuyafanya maisha yawe ya amani mijini mwao kwa kupunguza umilikaji silaha kiholela wenzetu wengine huko mnazitafuta.Nakumbuka wakati Ali Ameir Mohd alipokuwa waziri wa mambo ya ndani, aliwahi ku-raise suala la umilikaji silaha za moto...mjadala mkali ukazuka kutoka kwa wanajamii..sujuwi iliishia wapi habari ile.
 
Miaka 3 iliyopita niliwahi kwenda kwenye lile duka la silaha pale Samora (Behind TRA) ili kujionea Silaha zenyewe. Walinipokea vizuri tu na walikua cooperative sana kunionyesha silaha za aina mbalimbali, kunitajia bei zake na hata kunipa nizishike na kuzikagua endapo ningeipenda.

Waliniambia kama kuna niliyoipenda utaratibu ni kwamba ningetakiwa kulipia Full amount (ilikua ina Rage from 700,000 to 1,500,000 depending on features) Lakini huchukui Silaha.

Baada ya hapo wangenipa Fomu 1 in 4 copies, ambayo ningeenda nayo Serikali za Mitaa, Kamati ya usalama ya Mtaa ingekaa na kunijadili na kuziforward hizo Form katika Kamati ya Usalama ya Wilaya ambapo wangezipitia na Kuziforward Katika Kamati ya usalama ya Mkoani na hatimaye mwishoni zingepelekwa Central Police Station.

Kila Stage itakapopitia copy moja ya hizo fomu hubaki huko kwa kumbukumbu. Vilevile walisema the main uzito mkubwa uko katika mapendekezo ya kamati ya usalama ya mtaa na Wilaya, Zikipita stage hiyo Mkoani na taifani hakuna shida kwa sababu hawakufahamu.

Baada ya Fomu kufika Central Policy Station, wao watakuita na kama wameridhika na recommendation za ngazi zote watatoa idhini ya wewe kwenda kuchukua hiyo silaha yako uliyolipia, Pamoja na Kitabu cha Silaha hiyo ambacho kitatumika wakati wa ukaguzi wa Silaha unaofanyika kila mwaka.

Unless wewe ni mwanajeshi au Polisi, Utatakiwa kulipia gharama za mtu kukupeleka Range kwa ajili ya kujifunza kutumia Silaha.

Process nzima kuanzia ulipolipia hadi kukabidhiwa silaha yako inaweza chukua miezi mitatu

Baada ya hapo unakua Mmiliki halali wa Silaha.

Mkuu asante kwa maelezo yako. Hiyo ndiyo process yenyewe lakini umesahau kusema kwamba lazima kamati ya ulinzi ya kitongoji ikuhoji kabla ya kwenda serikali ya mtaa ambao nao wanakuwekea kikao na kukuhoji maswali. Wakijiridhisha, ndipo documents zinapelekwa kwenye ofisi ya polisi iliyokaribu ambako mkuu wa kituo naye anatia mkono wake. Docs zikitoka hapo zinapelekwa kamati ya ulinzi ya wilaya ambako nako unaitwa kuhojiwa. Kama ni bunduki kubwa, basi kutoka wilayani docs zinakwenda moja kwa moja makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani,. Kama ni bastola, lazima maombi yapitiwe na kamati ya usalama ya mkoa. Wanaweza kukuita kukuhoji vile vile ikibidi.

Kule wizarani ndiko vitabu vya kumiliki silaha vinapotolewa sio central. Kwenye hicho kitabu wanaandika na idadi ya risasi unazopashwa kuwa nazo kwa wakati mmoja. Ukishapewa kitabu ambacho kinakuwa na details zote za silaha unayotaka kumilikishwa, then unakwenda dukani uliponunua ili wakukabidhi silaha yako.

Miezi mitatu uliyozungumzia ni kidogo sana. It can even take a year or so.

Enjoy kujilinda mwenyewe mkuu!!!!!

tiba
 
Tanzania tuna matatizo mawili makubwa: (a) tunapenda sana kuiga mambo ya nchi za nje hasa marekani, (b) tunawaogopa sana viongozi wetu kiasi kuwa wakitoa tamko hata kama ni wazo lao binafsi tunalichukulia kama ni sheria.

Swala la umiliki wa silaha za moto (bunduki) ni jambo ambalo siamini kuwa liliwahi kujadiliwa kwa kina na bunge letu bali lilitolewa kama agizo kutoka kwa Waziri mkuu (Sumaye) wakati ule. Matokeo ya umiliki hovyo wa bunduki, na hasa bastola, umesababisha mambo mengi ya ukiukwaji wa amani kwa raia wa kawaida, hasa yakiwahusisha watu wa ngazi za juu katika jamii: viongozi na wafanya biashara.

Marehemu Mzuzuri anakumbukuwa sana kwa hili, ila kuna watu wengi sana kama watoto wa wanasiasa wakongwe Kingunge na Mungai, na viongozi wengine mbalimbali pamoja na wafanya biashara wa viwango tofauti kama vile Mbilinyi Hartmann na steven Kanumba.

Umiliki wa silaha za moto kwa nchi kama Marekani ni swala tete sana ambapo makampuni ya utengenezaji wa bunduki yanatumia nguvu kujihakikishia soko la bidhaa zao hizo. Hata hivyo, Marekani bado wamegawanyika kuhusu umiliki wa silaha hizo ingawa vile vile wana sheria ngumu sana kuhusu utumiaji wa silaha za moto. Kuna mlolongo wa background check kabla mtu hajaruhusiwa kununua bastola, na state nyingine , kwa mfano Florida, wana sheria inaitwa 10-20-life kama inavyoelezwa hapa. Chini ya sheria hiyo, kutoa vitisho kwa kutumia silaha ya moto kunampeleka mtu jela miaka kumi na zaidi. Halafu kama ataua basi ajue naye atanyongwa bila cha swaleh mtume. Florida ni state ya pili kwa unnyongaji huko Marekani. Pamoja na kuwepo kwa hatua hizo, Marekani wamekuwa wansumbuliwa sana na mauaji ya hovyo ya utumiaji wa bunduki zinazonunuliwa mitaani, kwa mfano yale mauajia ya Virginia Tech na yale yaliyofanywa na Major Nidal Malik Hasan huko Texas hivi majuzi.

Kinachonifanya nianzishe thread hii, ni ukuaji wa vitisho na matumizi ya silaha za moto nchini kwetu kwa ubishi mdogo tu kama eti kugombea "demu."
Jana niliongea na ndugu yangu mmoja kule Tabora akaniambia kuwa mtoto wa Profesa Kapuya aliua kijana mwenzie kwa kumpiga risasi kwa bastola eti wakigombea DEMU: sijapata data zaidi kuhusu tukio hilo, ila hiyo ni trendi inayoonekana kuwa ya kawaida kwani wiki chache zilizopita kulikuwa na uvumi wa mwana sinema Hartmann kuwatishia mahasimu wake kwa bastola kwa vile eti walimnyang'anya DEMU.

Swali langu ni kuwa je Tanzania tulinogewa wapi na uzuri wa bunduki hadi kuwa na sheria za kuwaruhusu watu kumiliki bundukuki kiholela? Kwa utaratibu wa sasa tuna mwanya mdogo sana wa kujua tofauti kati ya jambazi na raia mwema tukiwaona wakiwa na bunduki.

Tulizoea bunduki kubwa (shortgun+ rifle) kama silaha za kuwindia tu. Bastola ni silaha ya kuua mtu, siyo silaha ya kuacha kila mtu ajibebee mfukoni na kwenda nayo kwanye vilabu.


Naomba Bunge letu liangalie tena sheria yoyote inayohusu umiliki holela wa silaha za moto kama bastola. Ningefurahi kama wataweka sheria ya kusimamia matumizi ya silaha hizo kama ile ya 10-20-life inayotumika Florida
 
kaka umenusurika nini kutoka mdomoni mwa hao uliowaita watoto wa vigogo, lakini hata mimi nahihitaji sana hiyo kitu kwa kwa mwaka huu tu unaoishia nimelizwa kuku 20, suruali 10 tena nilizotoka nazo England, shambani kwangu kibaha naibiwa matikiti, mikungu ya ndizi, passion zangu, kubwa zaidi nahiitaji ili kurekebisha kauli za Makonda na Madereva waendesha ovyo tena wenye midomo michafu.
 
watu ppppppppppppppppppppppppiiiiiiiiiiiiiippppppppppppppppppppppppooooooooo

tutauana mwaka huuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

Hata wewe unataka kulimiki silaha kisa kuku???????????????????????????????
 
kumiliki siraha ni HAKI ya mtu. ukitaka kufahamu kama kuna uchunguzi katika kupewa kibali cha kununua silaha, nenda kaombe! kitu kibaya ni kwamba, haiwezekani kumfahamu mtu kama ni mwema au la.....au atlisti ni ngumu.

Hata MAJAMBAZI wengine wanamiliki bunduki kihalali kabisa!!! ww kama unahitaji kujilinda ww na pesa yako tu ya kazi gani uombe kununua machinegun kama mfugaji? bastola kazi yake ni kujilinda na adui binadamu, ss watoto wanazitumia vibaya kugombea wanawake, mwingine katoka njombe kwenda iringa kumuua demu wake denti!! kaaaz kweli kweli! pamoja na hayo yooooote, bado haki yangu mimi kama raia mwema kumiliki siraha iko PALEPALE!
 
kumiliki siraha ni HAKI ya mtu. ukitaka kufahamu kama kuna uchunguzi katika kupewa kibali cha kununua silaha, nenda kaombe! kitu kibaya ni kwamba, haiwezekani kumfahamu mtu kama ni mwema au la.....au atlisti ni ngumu...Hata MAJAMBAZI wengine wanamiliki bunduki kihalali kabisa!!! ww kama unahitaji kujilinda ww na pesa yako tu ya kazi gani uombe kununua machinegun kama mfugaji? bastola kazi yake ni kujilinda na adui binadamu, ss watoto wanazitumia vibaya kugombea wanawake, mwingine katoka njombe kwenda iringa kumuua demu wake denti!! kaaaz kweli kweli! pamoja na hayo yooooote, bado haki yangu mimi kama raia mwema kumiliki siraha iko PALEPALE!

(1) Sidhani kama katiba yetu ina kifungu kiachosema ni haki ya mtu kumiliki silaha. Katiba ya marekani chini ya marekebisho ya pili inaruhusu raia kumiliki bunduki ili kujilinda na mali zao kama sehemu ya jeshi lka mgambo. Hilo hao kwetu ni maendelezo ya kuiga tu.


(2) Nadhani kinachotakiwa hapa ni kuwa na sheia zinazosimamia matumizi holela ya silaha hizo. Kama umesoma ile sheria ya 10-20-life niliyoweka link yake hapo juu; kumtishia mtu kwa silaha kunakupeleka jela miaka 10 na kama ukiifyatua unakaa jela miaka 20 na kama utamjeruhi mtu basi unakaa jela maisha.
10-20-life.GIF

Sheria za namna hiyo zitafanya watu wawe makini na kutumia silaha hizo kujikinga siyo kutishia watu
 
habari zenu wana jamii forum,naomba mtu anaejua taratibu na sheria za kumiliki silaha tanzania anifahamishe, napenda kujua ni procedures gani natakiwa kufuata, sifa gani natakiwa kuwa nazo ili niqualify kumiliki silaha?

Mfano nikiingia nchini na bastola yangu taratibu zikoje kuisajili, vilevile ningependa kujua kama kuna sehemu wanatoa mafunzo ya kulenga shabaha hapa tanzania(dar)

Asanteni.
 
Back
Top Bottom