Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Mwenye kufahamu utaratibu atupie hapa, mambo ya kupiga simu polisi sio wala nini
 
Habarini wana JF,

Nahitaji sana kumiliki silaha kwa ajili ya ulinzi binafsi, iwe Bastola au hata SMG.

Sina ufahamu wa kutosha njia the rahisi au fupi ya kuomba(kihalali) na kumiliki silaha hiyo. Ninachofahamu tu kuna maduka ya silaha hizi na kuna urasimu mwingi hadi kuruhusiwa umiliki wa silaha hizi.

Naomba wenye ufahamu, mnisaidie humu namna nyepesi ili kufanikisha umiliki huo.

Ahsanteni, nawakilisha.
16179ef387ccd927d2a6873f04932990.jpg

0b766ee1f26d750181b6418f0f192fc4.jpg
 
Wakuu amani iwe kwenu.

Nimeshawishika kununua bastola maana naona vibaka wanatishia sana amani hii mitaa yetu. Na hali hii imepelekea hadi sisi wanaume wa Dar kudharaulika kuwa tunaogopa vijana wanaojiita taifa jipya. Na mpaka Waziri wa mambo ya ndani naye kashangaa kuona wanaume wa Dar tunakimbilia chumbani pindi tunapowaona hawa vijana wanaojiita taifa jipya na panya roads.
b68824e4948ce05ccd087bd7113c5028.jpg

7424f14d705ab83f0e7c98a956b7e50a.jpg

Naomba mnifahamishe bastola inauzwa bei gani na zinapatikana maduka gani?
Je, kuna masharti gani au vigezo gani natakiwa kukidhi ili kuinunua?

Nawasilisha.
Rais2020
 
Ushauri wa bure tuu ni kwamba unaweza ukawa umekaribisha majambazi waje kuitafuta hiyo silaha. Na ukizigatia taarifa zinazotakiwa kutolewa mpaka kuipata, ni risk sana. Kama kutembea na dhahabu ama pesa nyingi. Ni mawazo yangu tuu lakini.
 
Wakuu amani iwe kwenu.

Nimeshawishika kununua bastola maana naona vibaka wanatishia sana amani hii mitaa yetu. Na hali hii imepelekea hadi sisi wanaume wa Dar kudharaulika kuwa tunaogopa vijana wanaojiita taifa jipya. Na mpaka Waziri wa mambo ya ndani naye kashangaa kuona wanaume wa Dar tunakimbilia chumbani pindi tunapowaona hawa vijana wanaojiita taifa jipya na panya roads.

Naomba mnifahamishe bastola inauzwa bei gani na zinapatikana maduka gani?

Nawasilisha.
Rais2020
Mkuu wee uko wapi[emoji86] [emoji86]
 
Nipo buguruni mkuu. Panya road na taifa jipya wanatishia amani
 
..Naomba mnifahamishe bastola inauzwa bei gani na zinapatikana maduka gani?

Tanganyika Arms, mjini, karibu na station.

Ukitaka vile vya ''kike'' kama show off tu ambavyo hata kwenye mfuko wa nyuma wa jeans vinakaa, vipo vya 2.5M. Ila ukitaka ya kiume ambayo ukifyatua hata muungurumo unasikika, utapata nzuri sana kwa 3.8M. Ukishanunua unaicha palepale then unaanza process ya kuiombea kibali. Unaweza kuchukua mwezi mmoja au mwaka mmoja kumalizia process yote,it depends on a lot of factors na labda serikali ya awamu ya tano imerahisisha urasimu.
 
Nashukru sana mkuu kwa Maelezo yako mazuri. Kuna gharama zozote ambazo natakiwa kuzitoa au kuzilipa baada ya kuimiliki either kwa mwezi au kwa mwaka?
 
Kila mwaka unalipia kile kibali, kama vile unavyolipia road licence ya mkoko. Gharama mpya siifahamu. Ukipita pale Arms watakupa all details
 
Back
Top Bottom