Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Vibali havitolewi hadi 2025 hivyo vumilieni.
Hakuna shortcut mtaliwa hela na hao wanaojiita usalama wa wilaya......
Utapita huko utakwama kwa Mkuu wa Mkoa
Kwanini havitolewi?
 
we pumbww nini ujilinde na vibaka tu labda upewe ya goroka si yenye risasi za kuua mtu
 
Vibali havitolewi hadi 2025 hivyo vumilieni.
Hakuna shortcut mtaliwa hela na hao wanaojiita usalama wa wilaya......
Utapita huko utakwama kwa Mkuu wa Mkoa

Sio kweli! Siku hizi watu hawamalizi hata mwaka wanapata’ wapo ninaowafahamu
 
Duuu kumbe hivi vidude vina gharama hivi? Kuna jamaa alinambia pistol ni kuanzia laki 5 hadi nane inapatikana kumbe haikuwa sahihi?
 
Hatua ya kwanza ni kwenda kununua silaha yenyewe,maduka kwa Dar ni Tanganyika Arms karibu na Stesheni na Duka la Jeshi Ngome,ukishalipia unaiacha palepale dukani lakini unapewa forms za kuanza kuzijaza na risiti ya silaha yako,ukitoka pale unaenda Police HQ kitengo cha IB,pale watakuchukua finger prints nia ni kuona kama ulishawahi kuwa na record za uhalifu,baada ya siku 3 ndio watakupa clearance certificate (hii ni barua ambayo inaku-clear kwamba hawajakukuta na criminal record yoyote).Gharama ya kulipia hapo Polisi ili kupata hiyo Clearance Report ilikuwa ni tsh 2000 mwaka 2015,sijui sasa ni tsh ngapi.
 
ukipata hiyo Clearance Report ya Polisi ndio unaanza mchakato wa kupeleka form zako Serikali ya Mtaa,huko Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa itakuhoji na kukujazia sehemu wanayotakiwa kujaza wakiambatanisha na muhtasari wa kikao cha Kamati yao,kikubwa huko andaa pesa ya chai ya kuwapa
 
ukitoka mtaa unaipeleka form kata yako,nako huko utaratibu ni huohuo wataijaza nako andaa chai yao maana bila chai hawakufanyii haraka
 
ukitoka hapo unaipeleka kwa OCD wa eneo lako nae anaijaza,chai iwe mbele kama tai,akiijaza OCS unaiacha hapo,wao wataipeleka Idara ya Usalama wa Taifa ya Wilaya nao wataijaza lakini watakuita kwa mahojiano kidogo,kisha wataijaza na kuirudisha Polisi then Polisi wataipeleka kwa Mkuu wa Wilaya uliopo,huko itakaa mpaka kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya kitakapoitishwa ndio mtaitwa waombaji wote siku hiyo kwa kuhojiwa,mimi yangu ilikuwa ni Kinondoni na tulihojiwa na Bwana mdogo Ally Happi akiwa DC pale
 
kwa kifupi mlolongo ni huo,ikitoka Wilaya inapelekwa mkoani mpaka hatua ya mwisho unapopewa kibali,ni mlolongo ulionichukua mwaka mmoja na miezi 10 mpaka nakuja kukamilisha,sijui kwa sasa kama kuna unafuu,haya kazi ni kwako
 
Kama kuna kituo cha polisi apo karibu nenda watakupa maelekezo yote
 
Kuinunua ndugu yangu ni kama vile kununua suruali dukani ila kuichukua ni nafuu kupata visa ya USA kuliko kupata kibali cha kuimiliki, cyo kwa zama hizi kama haukupata silaha kwenye utawala wa jk basi sahau kimiliki iyo kitu, kuna jamaa zangu wana kwenda mwaka wa3 hkna cha kibali wala nini, wamebakiza kuzitembelea silaha zao pale Tanganyika Arms na kuonyeshana2 kama watoto wadogo yangu hii!
 


Huo ndo utaratibu lakini ukiufuata utasubiri sana. Kuna watu nawafahamu wamepata silaha hata miezi 2 haifiki. Weka pesa mezani kila kitu kinapelekwa fasta na utaratibu hauvunjwi.
 
Dunia hii ya sasa kutaka kumiliki bunduki kwa kigezo cha kujilinda dhidi ya wezi na wanyang'anyi ni udhaifu tu,
labda kama ni kwa sababu zingine za show off na kutisha raia mtaani.

Waharifu wakiamua kufanya yao wanafanya tu hata kama unamiliki mitungi ya nyuklia au makombora ya masafa marefu.
.
.
Hizo pesa na nguvu inayotumika kufuatilia umiliki ni vema zitumike kujiongezea kipato zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…