Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Mkuu mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu: 1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corp. au Tanganyika Arms na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao. 2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua, maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). 3. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. 4. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance form kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai (kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi). 5. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance form ya Forensic department, form yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya mtaa, kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. 6. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. 7. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho. Nitaendelea....
Duuuh... Hapo ndo umuhimu wa shortcut unapokuja
 
KUHUSU UTARATIBU WA KUMILIKI SILAHA KISHERIA

Mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu:

1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corporation, Tanganyika Arms au central police station na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao kwa utunzaji. Kama ni silaha ya urithi basi kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichoridhia wewe kumilikishwa silaha hiyo (wakati huo silaha inayotakiwa kurithiwa ikiwa mikononi mwa moja ya hizo sehemu nilizotaja hapo juu).

2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua.

3. Fomu yako itatakiwa ipate maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). Hapa inaweza kuchukua siku chache tu au muda mrefu. Itategemea na UCHESHI wako.

4. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. Hapa ni suala la dakika chache tu na uchakavu kidogo.

5. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance certificate kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai. Kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi japo kuna uwezekano pia wa kupata majibu siku hiyo hiyo. Na kwa ujumla hapa hapana usumbufu wowote. Kuna malipo kidogo utalipia. Kama sikosei ni Tshs. 3,000/= au 5,000/=.

6. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance certificate ya Forensic department, fomu yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya serikali ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. Kama nilivyokwishasema hapa ndipo nyaraka zinaweza kukaa muda mrefu zaidi nadhani kuliko kwingine pote (hata miezi kadhaa) kwa sababu vikao vya kamati ufanyika mara moja moja.

7. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. Huku kwa kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu na pia kwa Mkurugenzi nyaraka hazikai sana.

8. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho.

9. Ukishalipia hicho kibali utaenda wizara ya mambo ya ndani makao makuu (kwa watu wa Dsm) ili ukaandikiwe kitabu cha kumiliki silaha kwa jina lako na pia chenye picha yako (Firearm Licence). Zoezi hili linahitaji muda mfupi tu siku hiyo hiyo.

10. Utachukua kitabu chako na kwenda ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa ili uandikiwe kibali cha kukuruhusu kununua risasi (haichukui muda-dakika chache).

11. Utaenda ulipohifadhi silaha yako (Mzinga, Tanganyika Arms au central police station) ukiwa na leseni yako na pia kibali cha kununulia risasi na hivyo kukabidhiwa silaha yako na pia kuuziwa risasi kwa idadi iliyokubaliwa kwenye kibali. Hapa utatakiwa kulipia storage charges za hiyo silaha tangu ulipoiacha hapo hadi siku hiyo unapotaka kuichukua.

12. Baada ya kupata leseni ya umiliki wa silaha kila mwaka (kuanzia Julai hadi Septemba) unatakiwa kulipia leseni yako. Baada ya Septemba utatakiwa kulipa na faini.

Kwa mtu anaebadilisha kunakuwa hakuna mlolongo mrefu kama hapo juu. Ataandika covering letter kwenda kwa kamanda wa wilaya anayoishi akiwa na vielelezo vyote vya silaha mpya na ya zamani. Lakini hakutakuwa na haja ya muhtasari wa vikao vya kamati za ulinzi na usalama vya ngazi ya kata na pia wilaya ambavyo ndivyo vinavyosababisha zoezi zima kuchukua muda mrefu na pia usumbufu usio wa lazima (hasa huku ngazi ya mtaa na kata kwani kama mjuavyo kila mtu anataka nafasi yake imwezeshe kupata mboga ya nyumbani na pia jioni kujenda heshima baa).

Angalizo: Mimi siyo polisi na wala siko ofisi zinazohusika kutoa leseni za umiliki wa silaha. Nilichoandika ndicho ninachofahamu kwa upande wangu kama mdau wa kawaida. Hivyo kunaweza kukawa na masahihisho fulani kwenye maelezo yangu kutoka kwa wenye ufahamu zaidi. Hata hivyo naamini kama masahihisho yapo basi yatakuwa si makubwa sana.
 
Habari wanaJF,

Jana asubuhi kuna maofisa wa polisi walikuwa clouds fm wanaelekeza utaratibu wa kuweza kumiliki silaha kihalali, lkn kwa bahati mbaya nilikuta kipindi kiko mwisho hivyo basi naomba kwa mnaojua mtujuze ni utaratibu upi mtu afuate ili aweze kumiliki silaha kihalali.

Pia naomba tupate tafasiri/tofauti ya haya maneno Bunduki, bastola, pisto.
"Kuwa na demu , F.F.U utamiliki bila vurugu"
 
KUHUSU UTARATIBU WA KUMILIKI SILAHA KISHERIA

Mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu:

1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corporation, Tanganyika Arms au central police station na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao kwa utunzaji. Kama ni silaha ya urithi basi kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichoridhia wewe kumilikishwa silaha hiyo (wakati huo silaha inayotakiwa kurithiwa ikiwa mikononi mwa moja ya hizo sehemu nilizotaja hapo juu).

2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua.

3. Fomu yako itatakiwa ipate maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). Hapa inaweza kuchukua siku chache tu au muda mrefu. Itategemea na UCHESHI wako.

4. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. Hapa ni suala la dakika chache tu na uchakavu kidogo.

5. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance certificate kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai. Kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi japo kuna uwezekano pia wa kupata majibu siku hiyo hiyo. Na kwa ujumla hapa hapana usumbufu wowote. Kuna malipo kidogo utalipia. Kama sikosei ni Tshs. 3,000/= au 5,000/=.

6. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance certificate ya Forensic department, fomu yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya serikali ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. Kama nilivyokwishasema hapa ndipo nyaraka zinaweza kukaa muda mrefu zaidi nadhani kuliko kwingine pote (hata miezi kadhaa) kwa sababu vikao vya kamati ufanyika mara moja moja.

7. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. Huku kwa kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu na pia kwa Mkurugenzi nyaraka hazikai sana.

8. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho.

9. Ukishalipia hicho kibali utaenda wizara ya mambo ya ndani makao makuu (kwa watu wa Dsm) ili ukaandikiwe kitabu cha kumiliki silaha kwa jina lako na pia chenye picha yako (Firearm Licence). Zoezi hili linahitaji muda mfupi tu siku hiyo hiyo.

10. Utachukua kitabu chako na kwenda ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa ili uandikiwe kibali cha kukuruhusu kununua risasi (haichukui muda-dakika chache).

11. Utaenda ulipohifadhi silaha yako (Mzinga, Tanganyika Arms au central police station) ukiwa na leseni yako na pia kibali cha kununulia silaha na hivyo kukabidhiwa silaha yako na pia kuuziwa risasi kwa idadi iliyokubaliwa kwenye kibali. Hapa utatakiwa kulipia storage charges za hiyo silaha tangu ulipoiacha hapo hadi siku hiyo unapotaka kuichukua.

12. Baada ya kupata leseni ya umiliki wa silaha kila mwaka (kuanzia Julai hadi Septemba) unatakiwa kulipia leseni yako. Baada ya Septemba utatakiwa kulipa na faini.

Kwa mtu anaebadilisha kunakuwa hakuna mlolongo mrefu kama hapo juu. Ataandika covering letter kwenda kwa kamanda wa wilaya anayoishi akiwa na vielelezo vyote vya silaha mpya na ya zamani. Lakini hakutakuwa na haja ya muhtasari wa vikao vya kamati za ulinzi na usalama vya ngazi ya kata na pia wilaya ambavyo ndivyo vinavyosababisha zoezi zima kuchukua muda mrefu na pia usumbufu usio wa lazima (hasa huku ngazi ya mtaa na kata kwani kama mjuavyo kila mtu anataka nafasi yake imwezeshe kupata mboga ya nyumbani na pia jioni kujenda heshima baa).

Angalizo: Mimi siyo polisi na wala siko ofisi zinazohusika kutoa leseni za umiliki wa silaha. Nilichoandika ndicho ninachofahamu kwa upande wangu kama mdau wa kawaida. Hivyo kunaweza kukawa na masahihisho fulani kwenye maelezo yangu kutoka kwa wenye ufahamu zaidi. Hata hivyo naamini kama masahihisho yapo basi yatakuwa si makubwa sana.
Yani unailipia kabla ya kupewa vibali? Au sijaelewa
 
Ahsante kwa maelekezo.

Ndiyo. Unalipia kwanza. Kumbuka muuzaji wa silaha na mtoa leseni au kibali cha kumiliki ni taasisi mbili au watu tofauti. Hauwezi kupewa kibali cha kumiliki kitu ambacho haujakilipia. Nadhani ikitokea umenunua na bahati mbaya ukanyimwa kibali kuna utaratibu wa kurudi kwa muuzaji na kurudishiwa hela yako.
 
Anhaaa hapo ndo tatizo langu lilipokuwa. Nmekuelewa bingwaaa.
 
Poa. Uzuri ukishailipia silaha hiyo muuzaji anachukulia kwamba hiyo tayari ni mali yako. Hivyo ukikosa kibali na ukawajulisha wauzaji kwamba umekosa kibali wanaweza kupata mteja mwingine wakakuunganisha nae mkafanya biashara. Au wewe mwenyewe ukimpata mtu anaeweza kuinunua mnakwenda nae huko silaha ilipohifadhiwa na kuuziana kwa mkataba. Japo sina hakika lakini naona bado kuna uwezekano wa hawa wauzaji kukurudishia pesa yako on the spot hata kama wao au wewe msipopata mteja mwingine wa haraka haraka wa kuinunua. Ni asset isiyooza.
 
Pistol ni kiingereza,tafsiri yake ni bastola.
Bunduki ni Kama, rifle, short gun ,AK47 na n. k.
Nimekuelezea kadri ya uelewa wangu.

Mkuu masahihisho kidogo tu: ni shotgun badala ya short gun. Hata bastola ni aina mojawapo ya short guns japo siyo shotgun.
 
Poa. Uzuri ukishailipia silaha hiyo muuzaji anachukulia kwamba hiyo tayari ni mali yako. Hivyo ukikosa kibali na ukawajulisha wauzaji kwamba umekosa kibali wanaweza kupata mteja mwingine wakakuunganisha nae mkafanya biashara. Au wewe mwenyewe ukimpata mtu anaeweza kuinunua mnakwenda nae huko silaha ilipohifadhiwa na kuuziana kwa mkataba. Japo sina hakika lakini naona bado kuna uwezekano wa hawa wauzaji kukurudishia pesa yako on the spot hata kama wao au wewe msipopata mteja mwingine wa haraka haraka wa kuinunua. Ni asset isiyooza.
Anhaaaa OK. Ila kumbe mlolongo ni complicated kiasi hiki!! Ni mgumu.
 
Mimi nionavyo kutokana na unyeti wa suala lenyewe la umiliki wa silaha utaratibu hauko complicated kwani unasaidia kuhakikisha kwamba silaha inaangukia katika mikono salama.

Kinachosababisha process ionekane ngumu ni kama nilivyosema awali kwamba kwenye ngazi ya ofisi ya mtaa na pia ngazi ya kata kuna kaurasimu fulani kanakopelekea utoaji wa kitu kidogo ili kupitishwa kwa fomu zako na kupata muhtasari. Na hawa wakikutilia ngumu hauendi popote kwa sababu ndiyo wanaokutambua vizuri mtaani kwako.

Sehemu nyingine inayochangia ni ngazi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambako muda mrefu unapita bila vikao vya kupitia hayo maombi. Kwingine hakuna usumbufu kivile.

Pia tabia zetu mtaani tunapoishi usaidia mambo kwenda kirahisi kwani nyendo zako zinakuwa hazitiliwi shaka na hivyo kujihakikishia kupata leseni ya umilikaji wa silaha bila longolongo nyingi.
 
KUHUSU UTARATIBU WA KUMILIKI SILAHA KISHERIA

Mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu:

1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corporation, Tanganyika Arms au central police station na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao kwa utunzaji. Kama ni silaha ya urithi basi kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichoridhia wewe kumilikishwa silaha hiyo (wakati huo silaha inayotakiwa kurithiwa ikiwa mikononi mwa moja ya hizo sehemu nilizotaja hapo juu).

2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua.

3. Fomu yako itatakiwa ipate maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). Hapa inaweza kuchukua siku chache tu au muda mrefu. Itategemea na UCHESHI wako.

4. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. Hapa ni suala la dakika chache tu na uchakavu kidogo.

5. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance certificate kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai. Kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi japo kuna uwezekano pia wa kupata majibu siku hiyo hiyo. Na kwa ujumla hapa hapana usumbufu wowote. Kuna malipo kidogo utalipia. Kama sikosei ni Tshs. 3,000/= au 5,000/=.

6. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance certificate ya Forensic department, fomu yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya serikali ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. Kama nilivyokwishasema hapa ndipo nyaraka zinaweza kukaa muda mrefu zaidi nadhani kuliko kwingine pote (hata miezi kadhaa) kwa sababu vikao vya kamati ufanyika mara moja moja.

7. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. Huku kwa kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu na pia kwa Mkurugenzi nyaraka hazikai sana.

8. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho.

9. Ukishalipia hicho kibali utaenda wizara ya mambo ya ndani makao makuu (kwa watu wa Dsm) ili ukaandikiwe kitabu cha kumiliki silaha kwa jina lako na pia chenye picha yako (Firearm Licence). Zoezi hili linahitaji muda mfupi tu siku hiyo hiyo.

10. Utachukua kitabu chako na kwenda ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa ili uandikiwe kibali cha kukuruhusu kununua risasi (haichukui muda-dakika chache).

11. Utaenda ulipohifadhi silaha yako (Mzinga, Tanganyika Arms au central police station) ukiwa na leseni yako na pia kibali cha kununulia risasi na hivyo kukabidhiwa silaha yako na pia kuuziwa risasi kwa idadi iliyokubaliwa kwenye kibali. Hapa utatakiwa kulipia storage charges za hiyo silaha tangu ulipoiacha hapo hadi siku hiyo unapotaka kuichukua.

12. Baada ya kupata leseni ya umiliki wa silaha kila mwaka (kuanzia Julai hadi Septemba) unatakiwa kulipia leseni yako. Baada ya Septemba utatakiwa kulipa na faini.

Kwa mtu anaebadilisha kunakuwa hakuna mlolongo mrefu kama hapo juu. Ataandika covering letter kwenda kwa kamanda wa wilaya anayoishi akiwa na vielelezo vyote vya silaha mpya na ya zamani. Lakini hakutakuwa na haja ya muhtasari wa vikao vya kamati za ulinzi na usalama vya ngazi ya kata na pia wilaya ambavyo ndivyo vinavyosababisha zoezi zima kuchukua muda mrefu na pia usumbufu usio wa lazima (hasa huku ngazi ya mtaa na kata kwani kama mjuavyo kila mtu anataka nafasi yake imwezeshe kupata mboga ya nyumbani na pia jioni kujenda heshima baa).

Angalizo: Mimi siyo polisi na wala siko ofisi zinazohusika kutoa leseni za umiliki wa silaha. Nilichoandika ndicho ninachofahamu kwa upande wangu kama mdau wa kawaida. Hivyo kunaweza kukawa na masahihisho fulani kwenye maelezo yangu kutoka kwa wenye ufahamu zaidi. Hata hivyo naamini kama masahihisho yapo basi yatakuwa si makubwa sana.
Kwa mlolongo huo itabidi uandae milioni kumi ya urithi wa nyumba ya baba yako tuntufe ili uhonge ndo ufanikiwe hilo zoez
 
Milioni kumi si kweli mkuu. Ukishanunua silaha yako hautakiwi kutoa rushwa sehemu yoyote kwani kutoa rushwa ni kosa kisheria. Labda utoe takrima hapo ni sawa. Ukitoa takrima ya laki moja ngazi ya mtaa na laki nyingine ngazi ya kata mchezo unakuwa umeisha. Kwa hiyo jumla ya takrima itakuwa kati ya 200,000/= na 250,000/=.
 
Haah haha mkuu kutoa au kupokea rushwa ni kosa kisheria kwa nchi gani?au unazungumzia hii danganyika ambayo hata mkuu wa kaya na mjomba wake mkwere wanakula rushwa. We fanya uchunguz wa hyo makitu ukirud utanipa mrejesho
 
Juzi walikuwa clouds wakihamasisha watu wakanunue silaha kwa njia halali, ila mlolongo wake sasa daaah
 
Mkuu mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu:

1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corporation, Tanganyika Arms au central police station na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao kwa utunzaji. Kama ni silaha ya urithi basi kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichoridhia wewe kumilikishwa silaha hiyo (wakati huo silaha inayotakiwa kurithiwa ikiwa mikononi mwa moja ya hizo sehemu nilizotaja hapo juu).

2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua.

3. Fomu yako itatakiwa ipate maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). Hapa inaweza kuchukua siku chache tu au muda mrefu. Itategemea na UCHESHI wako.

4. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. Hapa ni suala la dakika chache tu na uchakavu kidogo.

5. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance certificate kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai. Kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi japo kuna uwezekano pia wa kupata majibu siku hiyo hiyo. Na kwa ujumla hapa hapana usumbufu wowote. Kuna malipo kidogo utalipia. Kama sikosei ni Tshs. 3,000/= au 5,000/=.

6. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance certificate ya Forensic department, fomu yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya serikali ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. Kama nilivyokwishasema hapa ndipo nyaraka zinaweza kukaa muda mrefu zaidi nadhani kuliko kwingine pote (hata miezi kadhaa) kwa sababu vikao vya kamati ufanyika mara moja moja.

7. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. Huku kwa kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu na pia kwa Mkurugenzi nyaraka hazikai sana.

8. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho.

9. Ukishalipia hicho kibali utaenda wizara ya mambo ya ndani makao makuu (kwa watu wa Dsm) ili ukaandikiwe kitabu cha kumiliki silaha kwa jina lako na pia chenye picha yako (Firearm Licence). Zoezi hili linahitaji muda mfupi tu siku hiyo hiyo.

10. Utachukua kitabu chako na kwenda ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa ili uandikiwe kibali cha kukuruhusu kununua risasi (haichukui muda-dakika chache).

11. Utaenda ulipohifadhi silaha yako (Mzinga au Tanganyika Arms au central police station) ukiwa na leseni yako na pia kibali cha kununulia risasi na hivyo kukabidhiwa silaha yako na pia kuuziwa risasi kwa idadi iliyokubaliwa kwenye kibali. Hapa utatakiwa kulipia storage charges za hiyo silaha tangu ulipoiacha hapo hadi siku hiyo unapotaka kuichukua.

12. Baada ya kupata leseni ya umiliki wa silaha kila mwaka (kuanzia Julai hadi Septemba) unatakiwa kulipia leseni yako. Baada ya Septemba utatakiwa kulipa na faini.

Kwa mtu anaebadilisha kunakuwa hakuna mlolongo mrefu kama hapo juu. Ataandika covering letter kwenda kwa kamanda wa wilaya anayoishi akiwa na vielelezo vyote vya silaha mpya na ya zamani. Lakini hakutakuwa na haja ya muhtasari wa vikao vya kamati za ulinzi na usalama vya ngazi ya kata na pia wilaya ambavyo ndivyo vinavyosababisha zoezi zima kuchukua muda mrefu na pia usumbufu usio wa lazima (hasa huku ngazi ya mtaa na kata kwani kama mjuavyo kila mtu anataka nafasi yake imwezeshe kupata mboga ya nyumbani na pia jioni kujenda heshima baa).

Angalizo: Mimi siyo polisi na wala siko ofisi zinazohusika kutoa leseni za umiliki wa silaha. Nilichoandika ndicho ninachofahamu kwa upande wangu kama mdau wa kawaida. Hivyo kunaweza kukawa na masahihisho fulani kwenye maelezo yangu kutoka kwa wenye ufahamu zaidi. Hata hivyo naamini kama masahihisho yapo basi yatakuwa si makubwa sana.
Ha ha haaa Nyaka One, upo ndg yangu? Long time hatujaonana
 
Burundi ziko so cheap ila ukishaipata utaishi kama unaoga uchi nje maana jamaa zetu wakikuotea no mercy
 
Back
Top Bottom