Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Hata mie nitaitafuta Mwaka huu maana kuna wahuni wanaanza fatilia maisha ya watu
 
Hii mimi bora nisimiliki maana mtu akiniibia demu wangu tu namtawanya ubongo.
 
Ukiipata tayari be care, siku ukipoteza kwa namna yoyote ile kimbilia kituo cha polisi, gari acha nyumbani, mkanda acha nyumbani maana utawekwa Lupango kidogo kwa ajili ya kulisaidia jeshi.
Kama kuna ulazima sana miliki, kama si sana bora utafute njia mbadala ya kujilinda ili usiwe mtumwa wa bastola.
 
Mkuu Si kila kitu tunaweza share hapa,kutokana na unyeti wake naomba ufike kwa mtu mwenye cheo cha msajili wa silaha pale polisi makao makuu ghorofa ya 5 utapata majibu yote.
Kwa nini iwe siri? Ni utaratibu umewekwa kisheria hivyo kama unajua hukatazwi kushare info. Ninavyofahamu ni kwamba unanunua silaha halafu unaenda polisi unapewa fomu ya maombi ya kumiliki silaha kisha unaenda kwenye kamati ulinzi na usalama ya serikali ya mtaa ,,huko watakuhoji na kisha watakujadili kama unafaa kupewa kibali au la kwani wao ndio wanaokufahamu. Baada ya hapo watakupa copy ya muhtasari ambayo utaambatanisha na ile form kisha kuipeleka polisi wataichukua tayari kuipeleka kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya .Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakupa taarifa ya tarehe unayotakiwa kwenda kuhojiwa .kamati ya wilaya ikishapitisha maombi yako ,inayapeleka kamati ya mkoa huko watakujadili kisha kupitisha au kukataa. Wakikubali,makao makuu ya polisi yanakupa kibali. Ikumbukwe kwamba baada ya kununua silaha hutakiwi kuondoka nayo toka pale dukani isipokuwa tu baada ya kupata kibali,hivyo unapaswa kuiacha pale au kuomba askari polisi wa kwenda kuichukua na kuihifadhi polisi mpaka utakapopata kibali.
 
Nenda kwenye maduka ya Tanganyika Arms yaliyo mkoani kwako au kama uko Dar unaweza kwenda kununua pale makao makuu ya jeshi Upanga.

Hapo watakutajia aina mbalimbali na kukupa uzishike na kuzikagua.

Kama kuna ambayo utaipenda unatakiwa kulipia full amount lakini huchukui silaha.

Baada ya hapo wanakupa fomu 1in 4 copies, ambayo utaenda nayo Serikali ya mtaa wako, Kamati ya usalama wa mtaa itakaa na kukujadili kama unastahili kupewa kibali na kama wameridhika Watasaini na kuzifoward hizo fomu katika Kamati ya Usalama ya Wilaya ambapo watazipitia na kukujadili tena na kama wameridhika na maelezo yako watazifoward katika Kamati ya Usalama ya mkoani na wao watakaa na kukuuta watakujadili tena na wataridhika basi na wao watazipeleka Central Police Station.

Kila Stage itakapopitia copy moja ya hizo fomu hubaki huko kwa kumbukumbu. Vile vile Uzito mkubwa uko katika mapendekezo ya kamati ya Usalama ya Mtaa na Wilaya, Zikipita stage hiyo na taifani hakuna shida kwa sababu hawakufahamu.

Baada ya fomu kufika CPS wao watakuita na kama wameridhika na recommendation za ngazi zote watatoa idhini ya wewe kwenda kuchukua hiyo silaha yako uliyoilipia, Pamoja na kutabu cha silaha hiyo ambapo kitatumika wakati wa ukaguzi wa Silaha unaofanyika kila mwaka.

Process nzima kuanzia ulipolipia hadi kukabidhiwa silaha kuna wengine imewachukua zaidi ya mwaka na wengine hata miezi 2 inategemeana na kujulikana kwako.

ANGALIZO: Bastola ni silaha ya kuua mtu siyo silaha ya kupewa kila mtu awe anaimiliki na ajibebe mfukoni kwenda nayo kwenye baa kutishia watu, hivyo Huko kwenye kuomba kibali si kila aombaye hupata. Labda silaha za kuwindia tu.

Nimeandika kadri zijuavyo, hivyo wataalamu wengine wataongezea. Kama kuna sehemu nimekosea nisahihishwe.
Umekwiva Mkuu..upo njema sana
 
Mchakato huanza kwa kuinunua kutoka Duka la Silaha na kwa hapa Dsm yapo Mawili tu Moja pale Pembeni mwa Diamond Jubilee na Lingine Pembeni mwa TRA ya karibu na Station!

Ukinunua unapewa risiti bila ya Silaha husika na unapewa Muda wa Miezi Sita kufuatilia vibali

Mchakato wa Vibali unaanzia Serikali ya Mtaa Mpaka kwa Mkuu wa Wilaya ambako Kamati ya Ulinzi na Usalama itaketi na kukujadili na ukishathibitishwa ndio itaenda kwa Jeshi la Polisi na ukishathibitishwa unapewa Document ya Umiliki ambayo ndio utaitumia kuonesha Kwny Duka la Silaha ili upewe Silaha yako.

Zipo aina mbalimbali za Silaha kutegemea Kiwango ha Pesa yako na uhodari na uzoefu wako wa kujenga Shabaha kwa kuwa kuna zingine Zina hitaji uzoefu

Ushauri wangu kwako Kama huna strong reasons usihangaike kuimiliki kwa kuwa baada ya Muda Mfupi hugeuka kuwa Mzigo na inaweza hata ikapelekea kukupeleka Gerezani!

Mie Nina cha kwangu cha Miaka Mingi kiasi lakin kwa Mazingira yangu naanza kuhisi Mzigo na hasa kadri umri unavyoyoyoma maana Siku hizi Silaha yenyewe ndio bidhaa inayotafutwa na Wahalifu wakupore wakati zamani wakagundua una Silaha ya Moto ndio wanakulalia Mbali ( Mchakato wa Maombi huanzia Serikali ya Mtaani kwako ambapo Wajumbe wengi ni Watu wa Vijiweni hivyo ukianza tu Mchakato Mtaa Mzima unajua)

Ukinunua na ukakosa Vibali Basi wanakurudishia Fedha yako kwa kukata kiasi kidogo sana cha charge ya usumbufu!

Zile Nzuri bei yake inaanzia 2Million-4.5 Million kutegemea aina. Wataalam ( Mie ni User sio Mtaalam) wanasema kwa Mazingira yetu za Turkey na Italy ni more njema zaid
Paragraph ya mwisho umepatia sana Mkuu
 
Nenda kwenye maduka ya Tanganyika Arms yaliyo mkoani kwako au kama uko Dar unaweza kwenda kununua pale makao makuu ya jeshi Upanga.

Hapo watakutajia aina mbalimbali na kukupa uzishike na kuzikagua.

Kama kuna ambayo utaipenda unatakiwa kulipia full amount lakini huchukui silaha.

Baada ya hapo wanakupa fomu 1in 4 copies, ambayo utaenda nayo Serikali ya mtaa wako, Kamati ya usalama wa mtaa itakaa na kukujadili kama unastahili kupewa kibali na kama wameridhika Watasaini na kuzifoward hizo fomu katika Kamati ya Usalama ya Wilaya ambapo watazipitia na kukujadili tena na kama wameridhika na maelezo yako watazifoward katika Kamati ya Usalama ya mkoani na wao watakaa na kukuuta watakujadili tena na wataridhika basi na wao watazipeleka Central Police Station.

Kila Stage itakapopitia copy moja ya hizo fomu hubaki huko kwa kumbukumbu. Vile vile Uzito mkubwa uko katika mapendekezo ya kamati ya Usalama ya Mtaa na Wilaya, Zikipita stage hiyo na taifani hakuna shida kwa sababu hawakufahamu.

Baada ya fomu kufika CPS wao watakuita na kama wameridhika na recommendation za ngazi zote watatoa idhini ya wewe kwenda kuchukua hiyo silaha yako uliyoilipia, Pamoja na kutabu cha silaha hiyo ambapo kitatumika wakati wa ukaguzi wa Silaha unaofanyika kila mwaka.

Process nzima kuanzia ulipolipia hadi kukabidhiwa silaha kuna wengine imewachukua zaidi ya mwaka na wengine hata miezi 2 inategemeana na kujulikana kwako.

ANGALIZO: Bastola ni silaha ya kuua mtu siyo silaha ya kupewa kila mtu awe anaimiliki na ajibebe mfukoni kwenda nayo kwenye baa kutishia watu, hivyo Huko kwenye kuomba kibali si kila aombaye hupata. Labda silaha za kuwindia tu.

Nimeandika kadri zijuavyo, hivyo wataalamu wengine wataongezea. Kama kuna sehemu nimekosea nisahihishwe.
tatizo letu kubwa ni ujinga wa kihalaiki
 
hizi process mbona ndefu sana aisee!!
kwa kusoma tu nishachoka je nikianza kufuatilia je??
 
Habari zenu wakuu

Ni siku nyingi Sana zimepita nikiwa Kama mtanzania nimekuwa napata shauku ya kumiliki siraha kwaajili ya usalama wangu binafsi; Ila bado sijafahamu njia gani/nianzia wapi na kiasi gani niandae ili kufanikisha lengo naomba Msaada mnijuze.
image_search_1521210139247.jpg
 
Habari zenu wakuu

Ni siku nyingi Sana zimepita nikiwa Kama mtanzania nimekuwa napata shauku ya kumiliki siraha kwaajili ya usalama wangu binafsi; Ila bado sijafahamu njia gani/nianzia wapi na kiasi gani niandae ili kufanikisha lengo naomba Msaada mnijuze. View attachment 716921
Soma post namba 1 hapo juu
 
Ndugu yangu, mshale wa kisasa ni more effective na efficent kuliko bastola. Na hauna matata kisheria unaweza kumiliki bila kibali, na ni mzuri sana kwa kupambana na majambazi na wezi, very silence! Ukikaa mahali na mishale yako ukifyautua hawezi kujua uko wapi, tofauti na bastola( Labda iwe na silencer) Lakini unatakiwa kujua namna ya kuutumia, Ushauri tu.
Kaka naweza kupata wapi huo upinde na mishale ya kisasa? Niko interested.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom