Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Sawa mkuu ila huo ni uwezo wako wa kufikiri
Hunijui sikujui mazingira yamekuathiri
Hii tabia ya kuhisi kumwambia mtu sikujui hunijui kama unamtisha humu jf ungekuwa wa kutisha usingeuliza humu vitu vidogo hivyo hujui hata zinapatikanaje harafu unataka uogopwe
 
Rafiki Mambo
Ya kujilinda juzi nimesumbuliwa na vibaka Kama siyo karate wangeninyanganya simu na gari wangenyofoa vitu

Kaka utaratibu ni kununua kwanza then unaomba kibali cha kumiliki silaha. Mimi nipo kwenye hatua hizo lakini ni ngumu sana siku hizi na kuna urasimu sana. Nimenunua silaha toka July pale Tanganyika Rifle, nikajaziwa fomu pale nikaenda kwa kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya mtaa na kata walinitembelea nyumbani kukagua na kurithika kisha walisaini na kuniidhinishia. Mwezi huohuo nikawakilisha kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Nilifika polisi Wilaya nikajaza fomu , nikaenda polisi makao makuu nikachukuliwa alama za vidole na kurudisha fomu wilayani, zikaenda kwa afisa usalama wa wilaya kazipitia kwa sasa zipo chini ya mkuu wa wilaya fulani alkini amezikalia hadi leo. Anapaswa apange tarehe ya mimi kuitwa kuhojiwa laini hadi leo hajafanya hivyo ni miezi mitano sasa. Ikitoka hapo inabidi iende mkoani napo nadhani itakaa mwaka mzima. Ingawa nafahamu umuhimu wa vetting kuhakikisha kuwa anayemiliki silaha anastahili bila kuiweka silaha kwenye mikono isiyostahili ila muda inayochukua kulifanya hilo inasikitisha sana ni muda mrefu sana. Mimi nimetumia tshs 6,500,000 kununua silaha tu, pesa zimelala pale Tanganyika Rifles sijapata kibali na wala sitegemei kupata chini ya mwaka mmoja bila sababu za msingi. There is something wrong somewhere!!!!
 
Naomba mwenye ufahamu vigezo jin
umiliki silaha maduka yanayouza Bei na Aina ya silaha nzuri Bastoral inayobebeka kirahisi na ya kisasa walau risasi 15
Gobole lipo kwa bei sawa na bure.
 
Wakinichelewesha naenda mahakamani labda niambiwe Sina sifa niwe kichaa
Mpk hapo hau qualify kupata mkuu,maana kama uvumilivu wa hizo process umekushinda hata Judgement yako kwenye matumizi ya silaha yatakua na mashaka.
 
Nenda Upanga kwenye Makao Makuu ya Jeshi ukachague aina ya silaha na uilipie. Utapewa risiti ambayo utaenda nayo kituo kikubwa cha Polisi na utapewa fomu ambayo itatakiwa kujazwa na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji wa Kata, DC Pamoja na RC_baada ya kukamilika unazirejesha kwa RPC na utaitwa kuhojiwa, wakijiridhisha utapewa maelekezo ya nini cha kufanya, ila fingerprints na hati ya Uraia mwema itakuhusu
 
Vibali havitolewi hadi 2025 hivyo vumilieni.
Hakuna shortcut mtaliwa hela na hao wanaojiita usalama wa wilaya......
Utapita huko utakwama kwa Mkuu wa Mkoa
 
Hii tabia ya kuhisi kumwambia mtu sikujui hunijui kama unamtisha humu jf ungekuwa wa kutisha usingeuliza humu vitu vidogo hivyo hujui hata zinapatikanaje harafu unataka uogopwe
Mkuu sijakutisha ila nyie wasomi hamtaki sie wakulima wa bamia tukidunduliza nasi tumiliki mguu wa kuku
Nimeuliza vitu vidogo ufahamu wangu ndio ulipoishia nahtaji kufahamu zaidi
 
Aisee mkuu ukiipata kwa shortcut(na yenyewe kama utafanikiwa) siku kikinuka ndipo utaelewa maana ya "Mgambo wanaruka na kukanyagana".
Sio short cut ya kumiliki kinyemela short cut ya wazee kunywa soda
 
Back
Top Bottom