A
Anonymous
Guest
Habari, ninaandika uzi huu nikiwa na maumivu makubwa moyoni. Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2026, nikiwa nimesoma mchepuo wa PCB katika shule ya serikali.
Katika matokeo yangu ya kidato cha nne nilipata Division One ya pointi 7, na kutokana na juhudi zangu nilichaguliwa kuendelea na kidato cha tano katika shule ya serikali. Niliendelea kujituma kwa bidii katika masomo yangu, na kwa msaada wa Mungu nilifanikiwa kupata Division One ya pointi 5 katika kidato cha sita, nikiwa na alama za Physics B, Chemistry A na Biology B.
Hata hivyo, katika orodha iliyotolewa jana ya waliochaguliwa, jina langu halipo. Kinachoniumiza zaidi ni kuona baadhi ya watu wenye Division One ya pointi 9 wamejumuishwa huku mimi nikiwa nimepata matokeo bora zaidi.
Hali hii imeniumiza sana, kwani nimejitahidi kwa muda mrefu na nilikuwa na matumaini makubwa. Naomba mamlaka husika zifanye mapitio na kutoa ufafanuzi ili kuhakikisha mchakato unakuwa wa haki na wenye kuzingatia sifa za waombaji.