HOJA Taratibu za kupata Samia Scholarship zipoje? Iweje nipate division ya 1.5 nikose na wenye 1.9 wapate?

HOJA Taratibu za kupata Samia Scholarship zipoje? Iweje nipate division ya 1.5 nikose na wenye 1.9 wapate?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Shukuru kwa kila jambo linalokukuta huwezi jua nini kitatokea baada ya wewe kupata hio scholar

Waswahili wanasema BAHATI YA MWENZIO USIILALIE MLANGO WAZI
 
Wachangiaji wengi naona wanatema pumba tupu!

Bahati?Jinsia?Awamu?Subira?

Kama ni mambo ya awamu,kwa nini waliofaulu kwa kiwango cha juu zaidi wakosekane batch ya kwanza?

Ni siasa za Baba kanituma hizo,vimemo vinatembea.
Unaweza kukuta Tanzania nzima wanafunzi waliopata 1.5 PCB hawafiki mia,then kuna mjinga huko juu eti anadai dogo hajatimiza vigezo!
 
Maisha ni vita mjomba.
Usiumize sana ndonga hii Dunia haina usawa.

Relax, fanya application vyuo vipo vingi tu na kwa ufaulu wako utapata chuo chochote uende ukasome kwa hasira na makali yaleyale.
Tanzania kuendelea tusubiri kwanza Mataifa mengine yoooote yamalize hatua za maendeleo, ndipo na sisi tuanze upya. Kwa sasa tunawaza siasa na maujinga tu.

Vitu vingine tunalazimisha kufanana ila hatuwezi.
 
Habari, ninaandika uzi huu nikiwa na maumivu makubwa moyoni. Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2026, nikiwa nimesoma mchepuo wa PCB katika shule ya serikali.

Katika matokeo yangu ya kidato cha nne nilipata Division One ya pointi 7, na kutokana na juhudi zangu nilichaguliwa kuendelea na kidato cha tano katika shule ya serikali. Niliendelea kujituma kwa bidii katika masomo yangu, na kwa msaada wa Mungu nilifanikiwa kupata Division One ya pointi 5 katika kidato cha sita, nikiwa na alama za Physics B, Chemistry A na Biology B.

Hata hivyo, katika orodha iliyotolewa jana ya waliochaguliwa, jina langu halipo. Kinachoniumiza zaidi ni kuona baadhi ya watu wenye Division One ya pointi 9 wamejumuishwa huku mimi nikiwa nimepata matokeo bora zaidi.

Hali hii imeniumiza sana, kwani nimejitahidi kwa muda mrefu na nilikuwa na matumaini makubwa. Naomba mamlaka husika zifanye mapitio na kutoa ufafanuzi ili kuhakikisha mchakato unakuwa wa haki na wenye kuzingatia sifa za waombaji.
Duuh pole mwanangu!
 

Achana Na Malalamiko,,Butua Upande Mwingine Wa Ramani Ili Maisha Yapate Kusonga...
###MaishaHayanaHuruma###
###MaishaHayahitajiKutiaHuruma###
​
 
Una kadi? Namaanisha kitambulisho cha Taifa. Maana sehemu nyingi huwa kinasaidia sana kuthibitisha uraia wako
 
Daah kazi kweli kweli jana tumetoka kuliongelea hili maana baadhi ya vijana waliofanya vizuri wanakosa wanapata wengine wenye matokeo ya kawaida kabisa vigezo vyao havipo wazi wanachaguana wenyewe tu huko na watoto wao...
Mwanafunzi upo sahihi kuzungumzia kwa mifano ili wahusika watolee majibu sio hawa walioferi shule..
 
Ndoto za wengi zinaharibiwa kisa upuuzi
Kuna tofauti kati ya visingizio na kutimiza lengo
Vijana wanahangaika kutarajia kitu fulani Alf wanakuja na mengn
 
Kitu kikishakua kinashikiliwa na Mtanzania lazima kuwe na janja janja, pole sana kijana,
Usikate tamaa omba na sehemu zingine ufaulu wako mzuri sana
 
Pole kwa yaliyokusibu,

Samia scholarships wanatoa nafasi kwa wahitimu kwa kuwa rank kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho katika idadi wanayohitaji katika vigezo vikuu viwili ambavyo ni jinsia na uhitaji maalum.

Mfano kwa mwaka husika ,kama scholarship itatolewa kwa wahitimu 700, the first 350 wavulana na 350 wasichana watakuwa ranked separately kwa jinsia na kati yao watu wenye uhitaji maalum watapewa kipaumbele .

So kwa case yako zingatia jinsia yako. Competition ya mwaka husika, na kama unauhitaji maalum.

Pia usipolidhishwa na machaguo waeza enda pale Tazara ofisi za Helsb watakupa maelezo zaidi
 
Back
Top Bottom