Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

11

Jioni Moja tarehe 2 November 1973 , Oleg na mkewe pasua kichwa Yelena ndio kwanza walikuwa wamemaliza dinner,wakasikia mlango ukigongwa . Kwenda kufungua mlango ,Oleg hakuamini alikuwa ni rafiki yake wa siku nyingi bwana stanislav kaplan. alishtuka na vilevile aliogopa kwa wakati mmoja. kwa furaha wanaume Hawa wawili walipeana mikono na kusalimiana kwa furaha akimsihi kuingia ndani.Laiti Oleg laiti angejua bwana stanislav hakuwa peke yake. mkewe alihis kitu kisicho Cha kawaida kwa mgeni wa wakati ule.
Basi bwana Oleg alimkaribisha stanislav na glass ya whiskey na kumtambulisha kwa Yelena na Convo za hapa na pale. Stanislav alimwelezea Oleg kwa Sasa (wakati huo) anafanya kazi kwenye shirika la bima la Canada na amekuja hapo Denmark kwa ajili ya mpenzi wake mdanish. Bwana Oleg alimcheki rafiki yake usoni kwa maelezo aliyokuwa anayatoa ,Kisha akacheki na mkono ambao Stan alikuwa ameshika glass ya whiskey akatambua jambo kwa huyu rafiki yake anamficha. Jasusi ni jasusi tu. Oleg alitambua best yake anamwongopea. Huyu stanislav alitumwa. Stanislav akaendelea kumweleza Oleg jinsi alivyoondoka Czechoslovakia na kutimkia Bulgaria Hadi kufika Canada kupitia ufaransa.
Oleg akawa anapata tu baadhi ya hints kutoka kwa maelezo ya best yake. Baada ya kumaliza whisky alinyanyuka Ili kuondoka na kumwambia kama wangeweza kuonana kwenye mgahawa mmoja hapo mjini Copenhagen waweze kuongea kesho .oleg akakubali.
Na kweli bwana Oleg alifika ila kwa kuchelewa kwenye appointment akijihakikishia hakuwa anafuatiliwa kwa Siri( he was wrong ). stanislav alifika wa kwanza akimsubiri rafiki yake kwenye meza iliyokuwa karibu na dirisha la vioo. Wakawa wanapiga stori mbili tatu , hususan uvamizi wa urusi nchini Czechoslovakia na yaliyoendelea huko na mambo mengine mengi .wakati Hawa marafiki wakiwa wanaongea upande wa pili kachero wa M16 mike Stokes ( muda huo alijifanya kama mtalii akijifanya anasoma tourist guide book[emoji39][emoji39][emoji1]). Alikuwa akiwafuatilia kwa karibu akiwa amekaa kwenye meza iliyo nje ya mkahawa wa jirani ng'ambo ya pili ya barabara . Kumbuka stanislav na Oleg walikuwa wamekaa kwenye meza iliyopo karibu na dirisha hivyo kwa mtu aliye nje ilikuwa rahisi kuwaona kwa uzuri.
Lengo la stanislav ni kujua maoni ya rafiki yake kuhusu nchi yake kuvamiwa na jinsi yeye anavyoshirikiana na mashirika ya kijasusi ya west. Hapa bwana Oleg alikuwa anafanyiwa assessment ya kitaalamu sana . maana taarifa zake A to Z. wanazo. Baada ya kupata mlo wakapeana mikono kuagana na mwishowe stanislav akatokomea kwenye umati wa watu. Hakukuwa na mazungumzo seriously sana waliyoongea au ahadi zozote walizoahidiana . Ila bwana oleg tokea hapo akawa vigilant kuliko kawaida . kwamba Alihisi rafiki yake ametumika kumpima imani kuhusiana na kufanya kazi na idara za ujasusi za west.

stokes na stanislav walikutana hotelini jijini hapo Copenhagen Ili kupeana debriefing za mchakato wao wote na mwisho stokes akaruka kwa ndege Hadi London kupeleka report kwa partner wake guscott na kuchambua vilivyo. kazi nyingine akaachiwa bwana bromhead hapo Denmark.
Ilikuja kubainika kupitia manjagu wa PET kisha wakawatonya M16, Bwana Oleg Huwa anacheza mchezo wa badminton kila asubuhi na mrembo mmoja hivi kwenye kiwanja kimoja kilichopo pembezoni mwa mji kidogo. Huyu mrembo alibainika kwa jina la Ana.
Hivyo bwana bromhead akaamua kufanyia kazi hizi report za ujasusi na kuingia field. Na kweli bwana bromhead akajitosa Hadi kwenye kitongoji hicho asubuhi Moja na kumuona Oleg akiwa na mrembo huyo wakiingia ndani ya kiwanja kimoja.Aliwafuatulia kwa Siri akiwa ndani ya gari ambalo alilitoa namba zile za diplomatic na kuweka private number Ili asiweze kugundulika. Na kweli aliweza kumuona Oleg Gordievsky akiwa na mrembo huyo. bromhead na Oleg kwa mara nyingine tena waliweza kuonana na Oleg hakushtuka alishawahi mwona kwenye hafla kadhaa . Baada ya michezo kumalizika na maongezi ya hapa na pale bromhead akaomba wakutane sehemu wazungumze . Oleg alikubali ila kwa sharti sehemu iwe private kidogo. Wakapendekeza wakutane kwenye hotel Moja inayoitwa Østerport hotel iliyo karibu na railroad inayoelekea zilipo ofisi za ubalozi baada ya siku tatu.. Baada ya kuachana na kuagana , bromhead alipofika ofisini direct akanyanyua simu akawatonya M16 huko London mpango wake kukutana na Oleg privately.
Oleg naye alipofika ofisini mwake naye akamwambia balozi boss wake bwana mogilevchik kwamba Kuna afisa mwenzake mfanyakazi wa ubalozi wa uingereza kamwalika kwenye lunch. Boss wake hakuwa na jibu . Hii taarifa ikafika Moscow Hadi kwa bwana Dimitri Yakushin boss wao. Na kweli naye akamruhusu bwana Oleg asikatae mwaliko aende . maana waliona hii kwao ni chance ya kumtumia bromhead kupata infos za western countries hususan uingereza. Nao upande wa kina bromhead walikuwa na lao kichwani.
 
Mpaka hapa hii story imeandikwa na washinda vita, acha niendelee kuburudika....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…