Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Kwahiyo sababu picha hakupiga yeye ndio uhalalishe wewe kuzitumia baada ya yeye kuleta hii story humu? Jaribu kuwa na Akili basi kijana. We huelewi hata kufanya transcription kutoka kwenye SL kuja TL ni kazi ngumu na ambayo mwandishi anastahili credits zake halafu wewe unachukulia tu simpo?? Acha Upumbavu wa dhahiri kiasi hicho.
 
Hivi Hana kazi nyingine za kufanya huyu Hadi awe anakopy habari na kuziuza buku jero?
Mbona atafika mbinguni kachoka sana
 
Ni hovyo kweli yani hata story ya yoga alijifanyaga yake na kutoza watu ili kupata updates baada ya yoga ku stop updates na yeye aka stop, heri mleta mada ana share humu free Kwa wote kujifunza Sasa huyu mwizi anatoza wengine
Niliona twitter yeye anabadili heading tu ila content zinafanana na baada ya kusoma huku kaenda twitter chapu kuandika
 
Hatari sana
 
Boss tuendelee usijibu negative comments
Watu tunafatilia tuwekee vitu leo weekend muda wa kusoma upo
Naunga mkono asijibu hoja mbovu za huyo ndimu, in short ni troublemaker !
Sio kwenye uzi huu tu amekua mtatanishi bali ni nyuzi nyingi.

Ukitaka kujua anacopy ona comment alivyo ijibia , ipo mbali sana . Hii inaonyesha anaufutilia huu uzi.
 
Ingekuwa sikuheshim
Ingekuwa sikuheshumu ningekujibu. Hebu leo acha shetani apitie mbali.
 
Ingekuwa sikuheshim

Ingekuwa sikuheshumu ningekujibu. Hebu leo acha shetani apitie mbali.
Kama hukopi hii story huku na kuipakapaka rangi kwa viswaga vyako uchwara kabla ya kuipaste kwenye telegram yako mbona story haiendelei kule sasa? Iendeleze tuone hiyo creativity yako unayojitapa nayo sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
20


Akiwa nchini mexico bibiye Rosa hakujua Aldrich Ames ni jasusi. Lakini baadaye alikuja kugundua kwamba huyu bwana ake mpya ni spy na ameoa hii ilileta mtafaruku kidogo , kutokana na shinikizo la huyu mchepuko Aldrich alimwahidi angemuacha mkewe Nancy kwa talaka. Lakini utaratibu wa kuchukua maamuzi ya kumtaliki Nancy yalikuwa ni ya gharama sana ukilinganisha na kiasi Cha mshahara wa afisa huyo as per CIA salary scale alikuwa akipokea tu Dola elfu kama arobaini na kidogo kwa mwaka kipindi hicho. Kutokana na huyu Rosa kuwa ni mwanamke wa matanuzi , Aldrich alimwahidi angeacha kazi CIA na kuamua kutafuta kazi yenye mshahara mkubwa ku meet standard za mrembo huyo . Maamuzi haya ya kumsikiliza huyu mchepuko yalimgharimu maisha yake yote........




Turudi kwa bwana SUNBEAM..

Ubalozi wa Russia au Soviet ulikuwa maeneo ya Kensington palace gardens viungani mwa Jiji la London. Nyumba aliyofikia Oleg na familia yake haikuwa mbali sana na ofisi za ubalozi wa Soviet .
Ilikuwa ni nyumba yenye vyumba viwili mitaa hiyo ya Kensington .
Siku chache baada ya kufika alitembea Hadi mtaa wa nyuma ya ubalozi wake akiwa amevaa kofia ambayo sio rahisi kutambulika hadi kwenye kibanda Cha simu . Alibonyeza namba kadhaa alizokuwa Nazo alizopewa na guscott miaka michache nyuma akiwa Copenhagen. Baada ya ku dial hizo namba,alisikia upande wa pili wa simu sauti ikisema "hello , welcome to London, ,thank you for calling. We look forward to seeing you...." Hii ilikuwa ni sauti ilyorekodiwa ya bwana guscott ikimkaribisha Oleg London na rekodi ile ilitaka wakutane mwezi July tarehe nne.
Sasa ni rasmi Oleg alikuwa mikononi mwa M16 ndani ya uingereza .
Mkewe na wanawe wali adapt maisha ya uingereza kwa haraka sana.
Kipindi Oleg anawasili aliyempokea alikuwa ni balozi ambaye alikuwa ni secretary wa ubalozi huo wa Soviet aliyeitwa Arkadi Vasilyevich guk . Huyu bwana aliwasili hapo ubalozini miaka miwili nyuma. Mkomunisti kindakindaki na Cha pombe wa vodka ile mbaya. Hapo London alikuwa anakula na kunywa made in Russia peke Yake.
Alitambulishwa kwa wafanyakazi wenzake wa hapo ubalozini na orientation za hapa na pale.
Baadaye Oleg alikuja kugundua huu ubalozi ni ofisi yenye manungu, kujipendekeza,masengenyo, vinyongo na wivu na kila aina ya ushenzi miongoni mwa wafanyakazi wake wote aliowakuta .

Baadaye Bwana Oleg alianza harakati namna ya kuwasiliana na M16 ,na hatimaye tarehe nne July akapiga Tena namba zile alizopiga mara ya kwanza ila kwenye kibanda tofauti Cha simu . Na mara hii bwana Geoffrey guscott alipokea . Walipanga kukutana mchana huo eneo ambalo sio rahisi kwa manjagu wa KGB kuwepo . Walipanga kukutana kwenye hotel ya holiday inn mtaa wa Sloane. Na kweli Oleg alifika na kumuona guscott aliyekuwa amekaa na mwanamama mmoja wa makamu kidogo. Huyu mama alijulikana kama Veronica price. Walisalimiana na Kisha wakasimama na kutoka wakienda moja kwa Moja nje ya hotel hiyo kupitia mlango wa nyuma. Oleg aliwafuata pasipo kusema neno.nyuma ya hotel kulikuwa na park ya magari . Kulikuwa na gari inasubiri hapo ikiwa imepakiwa tokea hapo usiku wa jana yake aina ya ford wakaingia ndani ya gari Hilo lililokuwa na plate number ambazo sio rahisi ku track. Guscott na Oleg walikaa siti za nyuma wakaanza maongezi wakijuliana Hali ,huku mwanamama Veronica price akiendesha. Walikuwa wakiongea ki Russia pasipo huyo mama kujua Nini wanaongea. Veronica price aliendelea ku drive gari Hadi Bayswater zilipokuwa nyumba kadhaa . Nyumba hizi zilichaguliwa kama safe house na M16 kwa ajili ya bwana Oleg. Zilikuwa umbali wa mwendo wa gari masaa mawili kutoka ubalozi wa Soviet hapo London.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…